Siku 30 Nzito za Maisha Yangu. ooh, Glory to God!!!

Kwa wanaokumbuka, Miss Judith aliibukia rasmi na Mijadala ya SAMUNGE, aka Kwa Babu!
Japokuwa alionyesha kumnyanyapaa babu siku hizo, mwenyewe kwasasa amemkubali baada ya Ripoti ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa ripoti rasmi kuonyesha kuwa dawa ya Babu inatibu UKIMWI!
Kwahiyo Mchungaji MWASAPILE ndiyo ilikuwa NITOKE VIPI ya Miss Judith!

...DAH!!!...mzee PJ una - - connect the dots - - - mpaka kieleweke 'mbele ya kasisi,' he he! safi sana!
 
Nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya unayotegemea kuyaanza hapo baadae, na umechukua uamuzi mzuri kwani maisha haya inabidi mtu uanze kujipanga na mapema. Kwa kweli wapo watu watakao kudhihaki lakini usirudi nyuma uamuzi wako ni mzuri nipo pamoja na wewe nakuunga mkono kwa uamuzi wako uliouchukua. Siku zote pokea pongezi na ushauri lakini mwisho wa siku fuata nafsi yako inataka nini.

Kuna mmoja wetu amesema hakuelewi kwa kusema unataka kumtaarifu huyo mheshimiwa mtarajiwa na ukatoa mchanganuo wa ratiba yako kulikisha kwenye tamati jambo hilo. Ila napenda nichukue fursa hii kumfahamisha yeye na wengineo kuwa sisi wanaume tunaweza tukawa tunataka kuwaoa wapenzi wetu lakini wao wanakuwa hawajawa tayari na pindi wakihisi ni muda muafaka ni jukumu lao kututaarifu. Kwahiyo hilo mie kwangu halina tatizo kabisa.

Mwisho kabisa nakushauri umwelekee Mungu wako kabla ya kutoa uamuzi huo ikiwa jambo hilo lina kheri basi mwombe Mungu akufanyie wepesi na ikiwa kuna shari basi Mungu akuepushie kwa njia ambayo itakupa faraja na kutokujuta kupoteza muda wako wa takribani miaka mitano katika uhusiano. Nina imani kuwa Mungu atakuongoza kwenye maamuzi na njia sahihi kabisa. Dua zangu zipo pamoja na wewe.

Wasalam,

Mohammed.
 
Ni maamuzi mazito kweli, hasa kwa hulka ya kike.
Nakutakia kila la heri katika kile unachokitamani.
Na nakuombea uwe tayari kukabidhiana na lolote utakalokutana nalo,
Manake, yawezekana huyo kaka hakufikirii tena wewe, labda moyoni kashamweka mtu mwingine.

Manake pia ulivyoipangilia hiyo, dah..................
Afu mwanamke ana haiba yake bwana Judy..................
Punguza kujiamini kupita kiasi..............
Uwe na kaaibu ka kike kidogo........ha ha ha ha.
All the best mamito.
 
https://www.jamiiforums.com/members/miss-judith.html 17th January 2011 01:

icon1.png
Hebu Sikieni Furaha Yangu

leo nimepata furaha kubwa sana. kuna mkaka mmoja aliwahi kuniapproach miaka ya nyuma akitaka kunichumbia na aliniambia ukweli kuwa alishadivorce na alipata mtoto mmoja kabla ya hiyo talaka. siku moja nikampa mtihani kuwa ampigie mtalaka wake simu mbele yangu amwambie kuwa licha ya talaka yao, anaomba wazae mtoto mmoja zaidi kwani hapendi kuwa na watoto na wanawake tofauti. alisita sana kwani alisema mtalaka wake ana maneno makali sana tena saa nyingine ya kashfa na angeweza kumtukana. baada ya kumhakikishia kuwa kama atamtukana nitamkubalia ombi lake palepale, alikubali.

alipompigia, mkewe alikuwa tofauti na alivyomtarajia. alicheka kwanza kwa mzaha, baadaye akamuuliza "leo una nini wewe, kitu gani kimekupata hadi unafikiria hivyo? natamani nikuone leo nijue kilichokupata!" walipokata simu alishangaa sana kwa maongezi yale, nilimwambia kuwa Mungu akishaunganisha watu huwa hawawezi kutengana, nikamwambia aendelee kumpigia simu kama hizo na amtafute ila akimkataa, tutakubaliana kuoana. sasa leo kanipigia simu anasema kuwa kakubali kuzaa naye! wow. God is at work! i am soooooo happy wapendwa.

jamani ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANDAMU ASIKITENGANISHE please!!!!!!!!!!!!!​

JUDITH...
Are you sure si huyu jamaa aliyekuwa anataka kunanihii mara ya kwanza?

  • Thanks
Reactions: Mbu
haya mama.....!

JF CONTRADICTORY MODEL WOMAN OF THE SEASON.....!

msalimie shossi kokote uendako
 
17th January 2011 01:

icon1.png
Hebu Sikieni Furaha Yangu

leo nimepata furaha kubwa sana. kuna mkaka mmoja aliwahi kuniapproach miaka ya nyuma akitaka kunichumbia na aliniambia ukweli kuwa alishadivorce na alipata mtoto mmoja kabla ya hiyo talaka. siku moja nikampa mtihani kuwa ampigie mtalaka wake simu mbele yangu amwambie kuwa licha ya talaka yao, anaomba wazae mtoto mmoja zaidi kwani hapendi kuwa na watoto na wanawake tofauti. alisita sana kwani alisema mtalaka wake ana maneno makali sana tena saa nyingine ya kashfa na angeweza kumtukana. baada ya kumhakikishia kuwa kama atamtukana nitamkubalia ombi lake palepale, alikubali.

alipompigia, mkewe alikuwa tofauti na alivyomtarajia. alicheka kwanza kwa mzaha, baadaye akamuuliza "leo una nini wewe, kitu gani kimekupata hadi unafikiria hivyo? natamani nikuone leo nijue kilichokupata!" walipokata simu alishangaa sana kwa maongezi yale, nilimwambia kuwa Mungu akishaunganisha watu huwa hawawezi kutengana, nikamwambia aendelee kumpigia simu kama hizo na amtafute ila akimkataa, tutakubaliana kuoana. sasa leo kanipigia simu anasema kuwa kakubali kuzaa naye! wow. God is at work! i am soooooo happy wapendwa.

jamani ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANDAMU ASIKITENGANISHE please!!!!!!!!!!!!!
JUDITH...
Are you sure si huyu jamaa aliyekuwa anataka kunanihii mara ya kwanza?

...khaaa!? msukule?
Miss Judith ana ushawishi wa ajabu!

PJ mie husali usiku na mchana kuniepushia mw'mke kama huyu.
Anyway,...bado namuombea heri kwenye azma yake ya uchumba mpaka ndoa na huyo kaka.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Hongera sana miss Judith kwa hatua uliyofikia, nipo pamoja nawe kimaombi katika kufikia lengo lako Be blessed!!
 
...khaaa!? msukule?
Miss Judith ana ushawishi wa ajabu!

PJ mie husali usiku na mchana kuniepushia mw'mke kama huyu.
Anyway,...bado namuombea heri kwenye azma yake ya uchumba mpaka ndoa na huyo kaka.

Mbu kaka angu, wala usiwaogope wanawake kama hawa.
Mtu kama Miss Judy kuna shule fulani za maisha wakipitia wanaelemika na kuwa wanawake wazuri tu. Tena bora na wenye hekima na unyenyekevu mkubwa.

Ni wakati tu, na mtu kujitambua kwamba ana tatizo na anahitaji tiba.
Dah, yahitajika hekima na unyenyekevu, wakati mwingine hata kujifanya mjinga ili uweze kwenda sawa na mwanaume Judy.

Maombi ni silaha ya ziada, lakini hekima, busara na UNYENYEKEVU ni silaha kubwa sana. Misimamo inayopita kiasi ni adui mkubwa wa mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume.

Haina maana kwamba usiombe hapana, omba tena kwa bidii, lakini mahusiano ingawa siwezi kusema nina uzoefu katika hilo,
Lakini ni mambo ya kimwili na yanahitaji akili za kichwani aidi ya rohoni.

So Judy muombe Mungu akufinyange, akuumbie moyo wa kike.
 
Nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya unayotegemea kuyaanza hapo baadae, na umechukua uamuzi mzuri kwani maisha haya inabidi mtu uanze kujipanga na mapema. Kwa kweli wapo watu watakao kudhihaki lakini usirudi nyuma uamuzi wako ni mzuri nipo pamoja na wewe nakuunga mkono kwa uamuzi wako uliouchukua. Siku zote pokea pongezi na ushauri lakini mwisho wa siku fuata nafsi yako inataka nini.

Kuna mmoja wetu amesema hakuelewi kwa kusema unataka kumtaarifu huyo mheshimiwa mtarajiwa na ukatoa mchanganuo wa ratiba yako kulikisha kwenye tamati jambo hilo. Ila napenda nichukue fursa hii kumfahamisha yeye na wengineo kuwa sisi wanaume tunaweza tukawa tunataka kuwaoa wapenzi wetu lakini wao wanakuwa hawajawa tayari na pindi wakihisi ni muda muafaka ni jukumu lao kututaarifu. Kwahiyo hilo mie kwangu halina tatizo kabisa.

Mwisho kabisa nakushauri umwelekee Mungu wako kabla ya kutoa uamuzi huo ikiwa jambo hilo lina kheri basi mwombe Mungu akufanyie wepesi na ikiwa kuna shari basi Mungu akuepushie kwa njia ambayo itakupa faraja na kutokujuta kupoteza muda wako wa takribani miaka mitano katika uhusiano. Nina imani kuwa Mungu atakuongoza kwenye maamuzi na njia sahihi kabisa. Dua zangu zipo pamoja na wewe.

Wasalam,

Mohammed.

mpendwa kaka Mohamed,

asante kwa dua zako na ushauri wako murua. kwa kweli JF nimeishaifahamu vya kutosha na siwezi kutetereka kwa jambo nyeti la maisha yangu kama hili.

asante pia kwa kuongeza ufafanuzi kuhusu ratiba ninayoipendekeza hadi kuhitimisha mchakato huu. ni ufafanuzi mzuri sana na ni wa kweli. aliponitaka hiyo 2006 mimi nilimpenda sana ila sikuwa tayari na namshukuru kwa uaminifu wake, hajawahi kukata tamaa ya kunisihi tufikie ndoa na hajapata kupunguza mapenzi yake kwangu. na kwa kweli sijawahi hata kusikia tetesi kuwa amewahi katafuta msichana mwingine kwa miaka yote hiyo mitano! japo yaweza kuwa si kweli lakini uvumilivu wake na mapenzi yake ni ya hali ya juu sana kwangu.

mawasiliano kati yangu na huyu kijana yako hai sana na hata huwa tunafanya baadhi ya mambo mtu anaweza akatucheka. mfano kuna mwezi mmoja aliwahi kuchukua mshahara wake wote akaenda kuu-deposit kwenye akaunti yangu bila kuniambia. kwa kuwa ndiye rafiiki yangu mkubwa, nlimdokeza kuwa nimekuta salio langu benki kubwa kuliko nilivyotarajia. nilipomueleza hivyo, alitoa mfukoni deposit slip ya bank na salary slip na kunipatia nizisome. lahaula! aliniwekea mshahara mzima wa ule mwezi bila kubakisha hata senti moja kwa ajili ya matumizi yake mwezi ule! nilipomuuliza kwa nini kafanya vile akanijibu kwa mzaha kuwa "haha, its my pleasure!!" loh, nilijiuliza sana nitamsaidiaje kuukabili ule mwezi hasa nikizingatia ni rafiki yangu. nami nikaamua kitu kimoja, mshahara wangu ulipoingia, niliuchukua wote na na nikaambatanisha na salary slip na kumwekea kwenye account yake!

kwa mafano huo mmoja, ni wazi kuwa mapenzi yetu ni hai na ile kutumia neno "kumteua" haina maana kuwa nitaenda tu kumkurupusha kuwa njoo unioe! jamani, mambo mengine tujaribu kutafakari kiutu uzima

ubarikiwe sana mpendwa
 
Mbu kaka angu, wala usiwaogope wanawake kama hawa.
Mtu kama Miss Judy kuna shule fulani za maisha wakipitia wanaelemika na kuwa wanawake wazuri tu. Tena bora na wenye hekima na unyenyekevu mkubwa.

Ni wakati tu, na mtu kujitambua kwamba ana tatizo na anahitaji tiba.
Dah, yahitajika hekima na unyenyekevu, wakati mwingine hata kujifanya mjinga ili uweze kwenda sawa na mwanaume Judy.

Maombi ni silaha ya ziada, lakini hekima, busara na UNYENYEKEVU ni silaha kubwa sana. Misimamo inayopita kiasi ni adui mkubwa wa mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume.

Haina maana kwamba usiombe hapana, omba tena kwa bidii, lakini mahusiano ingawa siwezi kusema nina uzoefu katika hilo,
Lakini ni mambo ya kimwili na yanahitaji akili za kichwani aidi ya rohoni.

So Judy muombe Mungu akufinyange, akuumbie moyo wa kike.

Umempa ushauri mzuri sana ambao naamini anahitajika kuufanyia kazi kwa bidii
Otherwise atakuwa anahatarisha amani ndani ya nyumba yake mpya anayoitarajia
All the best Miss Judith.
 
Hicho Kidume kitakachoingia kwenye huo mtego wako atakua kajimaliza kabsaa:israel::israel:Mi naona kama anaolewa yeye?
 
Kila la kheri dia usinikose kwenye kibao kata :mwaaah::mwaaah:

haha

wewe tena? siwezi kukusahau kwa hilo, ondoa shaka kabisa

Ni maamuzi mazito kweli, hasa kwa hulka ya kike.
Nakutakia kila la heri katika kile unachokitamani.
Na nakuombea uwe tayari kukabidhiana na lolote utakalokutana nalo,
Manake, yawezekana huyo kaka hakufikirii tena wewe, labda moyoni kashamweka mtu mwingine.

Manake pia ulivyoipangilia hiyo, dah..................
Afu mwanamke ana haiba yake bwana Judy..................
Punguza kujiamini kupita kiasi..............
Uwe na kaaibu ka kike kidogo........ha ha ha ha.
All the best mamito.

asante mpendwa kwa ushauri

ila naona nawe umenaswa na mtego ule ule ulionasa wengine. huwezi kwenda kwenye mazungumzo kama hayo bila kuwa na mapendekezo yako mwenyewe, ndio maana nasema "...kama mambo yataenda kama ninavyoomba..." mimi si mwanamke wa kuburuzwa tu. kama ningeuwa hivyo basi labda ningeolewa ahiyo miaka mitano iliyopita! na huenda nisingekuwa hivi nilivyo leo hii, so mimi ni mtu wa kushaurianana kujadiliana lipi linawezekana na lipi lisilowezekana na nnaamini ni haki na wajibu wa wanawake wote kwa waume zao na hata wachumba wao.

hata hivyo asante,

Hongera sana miss Judith kwa hatua uliyofikia, nipo pamoja nawe kimaombi katika kufikia lengo lako Be blessed!!

asanye katavi, ubarikiwe sana
 
Mbu kaka angu, wala usiwaogope wanawake kama hawa.
Mtu kama Miss Judy kuna shule fulani za maisha wakipitia wanaelemika na kuwa wanawake wazuri tu. Tena bora na wenye hekima na unyenyekevu mkubwa.

Ni wakati tu, na mtu kujitambua kwamba ana tatizo na anahitaji tiba.
Dah, yahitajika hekima na unyenyekevu, wakati mwingine hata kujifanya mjinga ili uweze kwenda sawa na mwanaume Judy.

Maombi ni silaha ya ziada, lakini hekima, busara na UNYENYEKEVU ni silaha kubwa sana. Misimamo inayopita kiasi ni adui mkubwa wa mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume.

Haina maana kwamba usiombe hapana, omba tena kwa bidii, lakini mahusiano ingawa siwezi kusema nina uzoefu katika hilo,
Lakini ni mambo ya kimwili na yanahitaji akili za kichwani aidi ya rohoni.

So Judy muombe Mungu akufinyange, akuumbie moyo wa kike.

ushauri mzuri sana mpendwa, asante na nitaufanyia kazi

ubarikiwe sana
 
Hicho Kidume kitakachoingia kwenye huo mtego wako atakua kajimaliza kabsaa:israel::israel:Mi naona kama anaolewa yeye?

hahah, maoni mengine bwana!

anyway, thanks for a comment
 
Umempa ushauri mzuri sana ambao naamini anahitajika kuufanyia kazi kwa bidii
Otherwise atakuwa anahatarisha amani ndani ya nyumba yake mpya anayoitarajia
All the best Miss Judith.

nashukuru sana mpendwa kwa dua

ubarikiwe sana
 
mpendwa kaka Mohamed,
kwangu.

mawasiliano kati yangu na huyu kijana yako hai sana na hata huwa tunafanya baadhi ya mambo mtu anaweza akatucheka. mfano kuna mwezi mmoja aliwahi kuchukua mshahara wake wote akaenda kuu-deposit kwenye akaunti yangu bila kuniambia. kwa kuwa ndiye rafiiki yangu mkubwa, nlimdokeza kuwa nimekuta salio langu benki kubwa kuliko nilivyotarajia. nilipomueleza hivyo, alitoa mfukoni deposit slip ya bank na salary slip na kunipatia nizisome. lahaula! aliniwekea mshahara mzima wa ule mwezi bila kubakisha hata senti moja kwa ajili ya matumizi yake mwezi ule! nilipomuuliza kwa nini kafanya vile akanijibu kwa mzaha kuwa "haha, its my pleasure!!" loh, nilijiuliza sana nitamsaidiaje kuukabili ule mwezi hasa nikizingatia ni rafiki yangu. nami nikaamua kitu kimoja, mshahara wangu ulipoingia, niliuchukua wote na na nikaambatanisha na salary slip na kumwekea kwenye account yake!

kwa mafano huo mmoja, ni wazi kuwa mapenzi yetu ni hai na ile kutumia neno "kumteua" haina maana kuwa nitaenda tu kumkurupusha kuwa njoo unioe! jamani, mambo mengine tujaribu kutafakari kiutu uzima

ubarikiwe sana mpendwa

Mshahara....Mshahara...mShahara...money ....money....money!..money-love!...gooooosh!

Mapenzi ya fedha na vitu haya!
Yaani hii michezo ya HELA ndio umeona mfano mzuri wa kueleza kwenye PUBLIC?...My hairs!
Nilitegemea kuwa ungesema anawaheshimu wazazi wako, au wakati mmojawapoa anaumwa mnatunzana, au the way mnavyobehave katika matatizo mengineyo ya social?

Sasa asingekuwa na kazi angekufurahisha na nini?....Wasanii wakubwa nyie NA hayo maigizo yenu ya payslip!
Acheni comediez za kwenye video hizo!...
Anywayz, hii ni script nzuri sana ambayo akiipata film-maker ataamka tajiri kama RIZ-1.
To my view, umebakiza siku 29 kuingia kwenye heart-break na heart-attack!
 
wapendwa,

niko chumani kwangu saa hizi na nahisi pumzi zinataka kukauka. nina mchanganyiko wa wasiwasi na matumaini, japo najiamini kwa hili ninalotarajia kulifanya, lakini tashwishi na mchecheto vinanizinga, nimeona niwashirikishe huenda nikapata tafu japo kidogo!!

ni kwamba baada ya siku 30 zijazo yaani jumatano ya tarehe 1 june 2011, nitamuarifu rasmi kijana mmoja kuwa nimemteua kuwa mchumba wangu!!!

ni uamuzi mgumu na mzito sana kwangu mimi binafsi. kijana huyu nimemfahamu tangu mwaka 2006 alipoanza kunitaka mapenzi, tumezunguka naye sana katika mitaa ya mapenzi huku nikihakikisha kuwa anaupata moyo wangu kikamilifu japo mwili wangu sikumruhusu kuufunua. kwa kweli tumehangaika naye sana na tumewahi "kukosana" naye mara kadhaa kisha tunarudiana. natumaini mnanielewa vyema ninaongea nini hasa ninaposema "kukosana"

baada ya misukosuko yote, hatimaye alinielewa vyema nami nikamuelewa, sasa kila kilichokuwa kinazuia sisi kuwa mwili mmoja kimeondoshwa kwa neema za Mungu. nimeamua kuwa June mosi nitamthibitishia kuwa ndiye mume wa ndoto zangu. naam, mume wa ujana wangu! kama hatakuwa na objection, siku ya jumamosi ya tarehe 4 June, nitamtambulisha nyumbani kwetu na kumtaka naye apange siku ya kunipeleka na kunitambulisha kwao. kama mambo yataenda kama ninavyoomba, ndoa itafungwa mwezi october au novemba 2011!!

sasa nadhani mnaweza kuuhisi wakati niliomo ni wa aina gani.

naomba maombi yenu wote tuweze kuvuka salama. mimi naanza maombi mazito mfululizo kumkabidhi Mungu siku hizi zote 30 (and beyond) aziratibu mwenyewe kwa kadiri ya wingi wa rehema na fadhili zake

Mungu awabariki sana

mpenzi wenu Miss Judith (Mrs mtarajiwa)

Glory to God!

Mhhh kwa mtindo huu wewe ndo unamuoa huyo kijana.

Kila la kheri kadi ya mchango usisahau kuniletea nikuchangie.
 
All the best Miss Judith Mungu afanikishe hitaji lako, siku zote ukimuomba Mungu mkate hawezi kukupa jiwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom