Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 918
wapendwa,
niko chumani kwangu saa hizi na nahisi pumzi zinataka kukauka. nina mchanganyiko wa wasiwasi na matumaini, japo najiamini kwa hili ninalotarajia kulifanya, lakini tashwishi na mchecheto vinanizinga, nimeona niwashirikishe huenda nikapata tafu japo kidogo!!
ni kwamba baada ya siku 30 zijazo yaani jumatano ya tarehe 1 june 2011, nitamuarifu rasmi kijana mmoja kuwa nimemteua kuwa mchumba wangu!!!
ni uamuzi mgumu na mzito sana kwangu mimi binafsi. kijana huyu nimemfahamu tangu mwaka 2006 alipoanza kunitaka mapenzi, tumezunguka naye sana katika mitaa ya mapenzi huku nikihakikisha kuwa anaupata moyo wangu kikamilifu japo mwili wangu sikumruhusu kuufunua. kwa kweli tumehangaika naye sana na tumewahi "kukosana" naye mara kadhaa kisha tunarudiana. natumaini mnanielewa vyema ninaongea nini hasa ninaposema "kukosana"
baada ya misukosuko yote, hatimaye alinielewa vyema nami nikamuelewa, sasa kila kilichokuwa kinazuia sisi kuwa mwili mmoja kimeondoshwa kwa neema za Mungu. nimeamua kuwa June mosi nitamthibitishia kuwa ndiye mume wa ndoto zangu. naam, mume wa ujana wangu! kama hatakuwa na objection, siku ya jumamosi ya tarehe 4 June, nitamtambulisha nyumbani kwetu na kumtaka naye apange siku ya kunipeleka na kunitambulisha kwao. kama mambo yataenda kama ninavyoomba, ndoa itafungwa mwezi october au novemba 2011!!
sasa nadhani mnaweza kuuhisi wakati niliomo ni wa aina gani.
naomba maombi yenu wote tuweze kuvuka salama. mimi naanza maombi mazito mfululizo kumkabidhi Mungu siku hizi zote 30 (and beyond) aziratibu mwenyewe kwa kadiri ya wingi wa rehema na fadhili zake
Mungu awabariki sana
mpenzi wenu Miss Judith (Mrs mtarajiwa)
Glory to God!