Annina
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 437
- 57
Kwa wale waliobahatika kufika katika ofisi za balozi zetu katika nchi mbalimbali watakubaliana nami kwamba hali inasikitisha. Pamoja na uchache wa maafisa, uwezo wao kitaaluma pia ni wa kutilia shaka. Nchi karibu zote sasa zimeachana na political diplomat na kujiunga na economic diplomat, hii ina maana maafisa ubalozi wanatakiwa kuwa na uelewa wa hali ya juu katika masuala ya biashara na uchumi katika ngazi ya kimataifa. Kweli Tanzania haina watu makini katika fani hii wanaoweza kutumika huko? Hatuhitaji timu kubwa ubalozini ili kufanikisha agenda (kama tuna agenda), tunahitaji watu wenye sifa za kuwa huko. Nchi nyingine nafasi za ubalozi wanapewa watu wenye uwezo wa hali ya juu, mfano Korea huwezi kuwa diplomat mpaka ufikie viwango vilivyowekwa ikiwa ni pamoja na kufanya mitihani na kuandika mada mbalimbali za kiuchumi, mwisho wa siku wanapeleka watu wenye sifa ili kutetea agenda yao. Naomba anaejua sifa za diplomats wa Tanzania (hata kama hazifuatwi) anijulishe. Asante sana,Annina