Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Maafisa utumishi wa Tanzania wengi hawajua katiba wala sheria nje ya sheria za utumishi. Kwa hivi karibuni maswali mengi yamekuwa yakiibuka kuhusu uteuzi wa viongozi. Inaonekana wazi kwamba wanaopitisha majina kwenda kwa Mhe. Rais siyo wajuzi wa katiba wala sheria ni maafisa utumishi.
Nimeona mjadala wa uhalali wa solicitor General unaoendele katika mtandao wa X, sheria ilitaka awe amefanya kazi ya uwakili miaka kumi na tano ila yeye ameteuliwa akiwa na uzoefu usiofika miaka kumi. Nani alimshauri Rais amteue? Hao maafisa utumishi waliopitisha jalada lake kwa KM kiongozi walisoma sheria ?
Naamini ofisi ya KATIBU Mkuu Kiongozi ikiweka kitengo cha vetting chenye wajuzi wa sheria wapitie na kumshauri itasaidia sana kupata wafu wenye quality na wanapozingatia sheria.
Contrary kama uteuzi ulikuwa sahihi basi wanasheria wawe wepesi kuandaa majibu na kuondoa upotoshaji mitandaoni. Kukaa kimya kunafanya watu waamini hakuna ufuataji wa sheria wa mamlaka za uteuzi.