SIBUKA TV-Dr lwaitama amshauri mkapa kutojihusisha....

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Dr lwaitama akiongea kwenye Sibuka Tv,muda huu amesema kama angepewa nafasi ya kumshauri Rais Mstaafu Bwm,kwa udogo wake angemshauri BWM asijihusishe na Siasa ndogo ndogo labda angejihusisha na uchaguzi wa kiti cha Urais.
 
Mkapa natarajiwa kuja Shinyanga kwa ajili ya uchaguzi wa vitongoji!!
 
Aende kwenye siasa za nje anakopenda. Aliapa kutoshiriki local alipostaafu!!
 
Ukiona mtu aliyethubutu kupiga dili akiwa ikulu anafanya kazi ya siasa ndogo kama za uchaguzi wa vijimbo jua njaa imepiga hodi....
 
Ukiona mtu aliyethubutu kupiga dili akiwa ikulu anafanya kazi ya siasa ndogo kama za uchaguzi wa vijimbo jua njaa imepiga hodi....
Hana njaa huyu ila ana vitu anataka kuvificha kupitia kwa viongozi aliowaweka mwenyewe, hao watamvika ka nguo wajameni!
 
Mkapa hata siasa za urais hatakiwi kujihusisha. Tunakosea sana tunapowaacha marais wastaafu kufanya siasa za vyama. Kimsingi, hata kama ili mtu awe sharti atokee chama fulani, lakini sanctity ya urais inabeba dhamana zaidi ya chama. Kwa hiyo, ni bora anapostaafu asijihusishe na masuala ya vyama ili kulinda heshima ya urais.

CCM wanapingana na dhana hii, lakini wakumbuke kuwa kuna wakati rais mstaafu wa chama chao anaweza kujihusisha na siasa za kupingana na rais aliye ikulu, kama Kambarage alivyoonekana kufanya akazua tafrani. Utamu wa kumtumia Mkapa unalingana na uchungu wa Mkapa kuamua kupingana na chama chake. Ili kuokoa heshima ya wote, chama na Mkapa mwenyewe ni bora akae pembeni.
 
Dr lwaitama akiongea kwenye Sibuka Tv,muda huu amesema kama angepewa nafasi ya kumshauri Rais Mstaafu Bwm,kwa udogo wake angemshauri BWM asijihusishe na Siasa ndogo ndogo labda angejihusisha na uchaguzi wa kiti cha Urais.

Ni ushauri mzuri kwa Mkapa kuufanyia kazi, Arumeru imemuabisha sana.
 
hivi mradi wake wa clinton foundation umefia wapi au kahamishia lushoto?
 
Back
Top Bottom