upupu
JF-Expert Member
- Apr 15, 2008
- 614
- 197
Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu mlimani imeingia katika wakati mgumu baada ya vyama vya siasa na mafisadi kuingilia katika uchaguzi huo. Hadi kufikia sasa mgombea mmoja raia wa kigeni ambaye ameonekana ni tishio kwa chama tawala na mafisadi kuanza kutishiwa na kisha kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana yeye na kambi yake nzima ya kampeni.
Mambo yanayowezekana kuwa sababu ya yeye kusimamishwa ni pamoja na kuhoji matumizi ya hela za mradi wa MLIMANI CITY pamoja na kauli zake za kuwa wagombea wengine ni makada wa CCM, na kwamba yeye hata kuwa tayari kuendeshwa na wanasiasa
NADHANI MKANDALA ANATUMIWA SANA NA CHAMA TAWALA KUTIMIZA MALENGO YAKE, NA PENGINE ANAHONGWA HELA NYINGI SANA KATIKA HILI, NA YEYE BILA KUFIKIRI ANATII, HAJUI KUWA ANAJISHUSHIA HESHIMA YAKE, HATHAMINIKI TENA, SASA HIVI KWENYE JAMII YA CHUO NI KAMA MWEHU.
NAE ACHUNGUZWE KAMA FISADI