Nakubaliana na Dorothy Semu Vijana wa Siku Hizi ni Legelege Wanaopenda kubembelezwa hasa Wavulana, Wamekosa Somo la Siasa na JKT!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,031
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo amesema enzi zetu tulifundishwa somo la Siasa Primary hadi Secondary school kwahiyo tulielewa maana ya Siasa na wale walioamua kuwa Wanasiasa walifanya hivyo kwa dhati ya mioyo yao

Lakini vijana wa Leo ni Legelege wasiojua Wajibu Wao na Wanapenda kubembelezwa kwa kila jambo

Dorothy amesema hayo pale Chuo Kikuu cha DSM

Nakubaliana na Dorothy Semu kwa 100% na Vijana wa Leo Ndio hawa wanajiita CHAWA

Ramadan Kareem!
 
View: https://youtu.be/GviVxNkF0Zs?si=4eZ4wDxGAKPj8gZE
Dorothy Semu namkubali sana!
P
 
Hili jambo kila siku nalisema hapa, Chanzo kikubwa cha jamii kupotea ni Ulegelege uliopitiliza wa watoto wetu wa kiume.
Mtoto wa kiume anaogopa kufata fursa mkoa jirani au nchi jirani, na hana sababu za msingi.
Wanataka vitu vya kupewa bure tu.
Kutwa yupo chini ya kwapa za mama yake.
Namashukuru sana mzee wangu, Japo mwanzo tulikua tunamuona mnoko kumbe alikua anatufundisha.
 
Hahahaha, hawa waliopitia JKT ndio wameifikisha nchi hapa ilipo.
Lakini hawa hawa waliopitia JKT ndio mababu, mabibi, mababa na mamama wa hawa legelege.

Analopaswa kujua huyu mama kuanzia leo, generation hujengwa na sio kutokea kwa bahati mbaya, wenye akili na ufahamu hutengeneza na kulinda mipango yao juu ya generation hata tano zijazo.
Wakulaumiwa ni hao hao waliopitia JKT kushindwa kuelewa Taifa linahitaji generations nyingi mbele zinazoandaliwa.
 
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo amesema enzi zetu tulifundishwa somo la Siasa Primary hadi Secondary school kwahiyo tulielewa maana ya Siasa na wale walioamua kuwa Wanasiasa walifanya hivyo kwa dhati ya mioyo yao
Enzi hizo wasomi wachache wanafunzwa kuwa maisha yako serikalini na siasa tu na walifanikiwa
Sasa hivi mavyuo yote wanamaliza unawapeleka wapi kwenye siasa ajira ? Hazipo vikongwe bibi kizee vikina Dorothy kiongozi wa ACT Wazalendo vimekaba namba upinzani na vikongwe vibabu akina Mbowe na Lisu vimekaba namba na CCM vikongwe vimekaba namba hizo siasa wanaenda wapi?

Ajira hamna zinejaa vikongwe serikalini

Naona anadhihaki kizazi cha sasa vikongwe wote kama yeye vyama vyote vya siasa waachie ngazi waone kama vijana hawawezi

Vyama vyote vya siasa vimejaa vibibi na vibabu vya miaka hiyo anaongea huyu Dorothy vijana waingilie wapi kushika nafasi? Kila chama kuwe tawala au upinzani vibabu na vibibi vitupu vya miaka ya huyu Dorothy kurudi nyuma

Ujinga mtupu kaongea
Kikongwe huyo apishe vijana aone kama hawawezi
 
Kwa hiyo zidumu fikra za mwenyekiti na chama kushika hatamu viendelee kufundishwa mashuleni?
 
Sijui nini kimetokea, lakini ni kweli vijana hawataki shida kabisa. Hausikii tena vijana wa sekondari waki organize kudai haki zao, wale wa vyuo vikuu ndio kabisaa! Kumepoa kama shule za msingi tu.

Sijui ni chanjo wanazopigwa huko mashuleni, au mitaala inawajaza hofu ya kuhoji mamlaka, au ndio maisha yamekuwa bora?. Ila ni kweli vijana wamekuwa wazembe wazembe mno.
 
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo amesema enzi zetu tulifundishwa somo la Siasa Primary hadi Secondary school kwahiyo tulielewa maana ya Siasa na wale walioamua kuwa Wanasiasa walifanya hivyo kwa dhati ya mioyo yao

Lakini vijana wa Leo ni Legelege wasiojua Wajibu Wao na Wanapenda kubembelezwa kwa kila jambo

Dorothy amesema hayo pale Chuo Kikuu cha DSM

Nakubaliana na Dorothy Semu kwa 100% na Vijana wa Leo Ndio hawa wanajiita CHAWA

Ramadan Kareem!
Paschal Mayyala, Steve Nyerere, Lucas Mwashambwa ni vijana wa leo?
 
Nafikiri arudi afanye home work yake vizuri. Wanaifisadi na kuharibu nchi hii ni wanasiasa wakishirikiana na wafanyabiashara wengi kwa kufanya ufisadi kila leo.

Hawa ndio waliopiya JKT na kusoma hiyo siasa anayosema.
JK, Kinana, Makamba, Rostanm, Bashe labda Abdul pekee ndiyo hajapitia JK
 
Sijui nini kimetokea, lakini ni kweli vijana hawataki shida kabisa. Hausikii tena vijana wa sekondari waki organize kudai haki zao, wale wa vyuo vikuu ndio kabisaa! Kumepoa kama shule za msingi tu.

Sijui ni chanjo wanazopigwa huko mashuleni, au mitaala inawajaza hofu ya kuhoji mamlaka, au ndio maisha yamekuwa bora?. Ila ni kweli vijana wamekuwa wazembe wazembe mno.
Wanatishwa na wazazi wao
 
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo amesema enzi zetu tulifundishwa somo la Siasa Primary hadi Secondary school kwahiyo tulielewa maana ya Siasa na wale walioamua kuwa Wanasiasa walifanya hivyo kwa dhati ya mioyo yao

Lakini vijana wa Leo ni Legelege wasiojua Wajibu Wao na Wanapenda kubembelezwa kwa kila jambo

Dorothy amesema hayo pale Chuo Kikuu cha DSM

Nakubaliana na Dorothy Semu kwa 100% na Vijana wa Leo Ndio hawa wanajiita CHAWA

Ramadan Kareem!
kwenye debe vijana huwa ni wakakamavu sana, atakutana nao vizuri sana akijichanganya 2025...
 
Sijui nini kimetokea, lakini ni kweli vijana hawataki shida kabisa. Hausikii tena vijana wa sekondari waki organize kudai haki zao, wale wa vyuo vikuu ndio kabisaa! Kumepoa kama shule za msingi tu.

Sijui ni chanjo wanazopigwa huko mashuleni, au mitaala inawajaza hofu ya kuhoji mamlaka, au ndio maisha yamekuwa bora?. Ila ni kweli vijana wamekuwa wazembe wazembe mno.
Fursa zimekuwa chache kwa vijana ajira pia ni kipengele Kuna vijana kibao wanamaliza vyuoni huko wanaufaulu mzuri serikali inawaambia waende veta wakati wao walikuwa wakibebwa tu wengi wao wamekuja kujiendeleza shule baada ya kuwa wazee wengi wao walikuwa wakichukuliwa hata darasa la saba kuingizwa

Ndio Hawa wengi walikuwa vyeti feki
 
Back
Top Bottom