Siasa ndiyo chanzo kikuu cha shida ya Umeme na Maji Tanzania

Dibwi Method

Member
Nov 22, 2021
31
28
UHABA WA MAJI KUPELEKEA MGAWO MPYA WA UMEME?
Kwa wale wasiofahamu, uhaba wa maji nchini unaodaiwa kutokana na ukame uliosababishwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu (mabadiliko ya Tabia ya nchi), una madhara ya moja kwa moja kwenye upatikanaji wa umeme hapa nchini.

Hii ni kutokana na maji kuwa miongoni mwa vyanzo vikuu vinavyozalisha umeme wa Tanesco kupitia mabwawa mbalimbali yaliyotapakaa hapa nchini. Kutokana na kutegemeana huku, Sauti Kubwa inatabiri kurejea kwa mgawo wa umeme nchini kwani ni suala la muda tu kabla vina vya maji havijapungua na kusababisha kupungua kwa uzalishaji umeme.

“Mtu mwelevu hujifunza kupitia makosa ya mwenzake, Mjinga hungoja mpaka yamkute ndo ajifunze!”

TUNAKWAMA WAPI?
Tarehe 29 Machi, 2022, makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilisema:

SIASA CHANZO MATATIZO YA UMEME TANZANIA
Waziri wa Nishati wa Tanzania, January Makamba amesema hivi karibuni kuwa matatizo ya kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini Tanzania yataendelea hadi hapo ukarabati wa miundombinu ya kusafirisha nishati hiyo utakapomalizika.

Kauli hiyo inaonyesha jinsi tatizo la umeme nchini Tanzania lilivyo kubwa na jinsi ambavyo ahadi zilizotolewa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) kuhusu tatizo la umeme kuwa historia zilivyokuwa na siasa au tatizo la umeme kutumika kukidhi malengo ya kisiasa.

Mgombea urais wa CCM, John Magufuli (sasa marehemu) alisema kwenye kampeni za uchaguzi mwaka 2015 kwamba kama angechaguliwa, kukatika kwa umeme kungesahaulika.

Lakini sasa waziri Makamba anasema ni wajibu wake kuwaambia wananchi ukweli kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme nchini Tanzania: "Hatutawadanganya Watanzania kuhusu yaliyopo, tukifanya hivyo, tutakuja kuumbuka huko mbele na hatutazitendea haki nafasi tulizopewa," Gazeti la Mwananchi limemnukuu Makamba akisema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, Alhamisi, 24 Machi kuhusu mafanikio ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya mwaka mmoja.

Pamoja na ukweli mchungu wa kauli ya Makamba, ni wazi kuwa si Watanzania wengi watakaoshangazwa nayo. Kukatika kwa umeme mara kwa mara ni tatizo ambalo limezoeleka nchini Tanzania kiasi kwamba si tukio kubwa la kuripotiwa na vyombo vya habari hasa vya kimataifa pale linapotokea.

Linganisha na hali ilivyo katika nchi jirani ya Kenya. Tarehe 11 Januari mwaka huu wa 2022 umeme ulikatika kwa saa kadhaa katika nchi nzima ya Kenya baada ya njia ya umeme yenye msongo mkubwa kati ya Nairobi na bwawa la kufua umeme la Kiambere kupata hitilafu.

Tukio hilo liliripotiwa si tu na vyombo vya habari vya ndani lakini pia na vyombo vya habari vya kimataifa. Ilikuwa ni mara ya tatu ndani ya miaka minne kwa tatizo kama hilo kutokea. Vyombo vya habari vilitangaza kuwa tukio kama hilo lilitokea kwa mara ya mwisho mwezi Mei mwaka 2020. Baada ya tukio hilo viongozi waandamizi tisa wa kampuni ya Kenya Power inayosambaza umeme nchini Kenya walifikishwa mahakamani kwa kushindwa kuzuia uharibifu wa njia ya umeme. Kwa hapa nchini Tanzania kama kuna kazi ngumu anayoweza kupewa mtu kuifanya ni kuhesabu mara ngapi umeme unakatika nchini Tanzania kwa mwezi au hata kwa juma moja. Hakika ni kazi ngumu.

Na waziri Makamba anasema chanzo cha kukatika kwa umeme mara kwa mara ni miundombinu mibovu ya kusambaza umeme ambayo haikufanyiwa matengenezo kwa miaka mingi.

Februari 15, 2022 wakati akijibu hoja za wabunge katika mkutano wa 16 wa Bunge mjini Dodoma, waziri Makamba alielezea kwa kina kuhusu tatizo na hatua ambazo serikali inazichukua kulitatua.

Lakini baadhi ya wabunge walikataa maelezo ya waziri wakidai kuwa kuna jambo lililofichika nyuma ya pazia kuhusu tatizo la umeme. Walidai kuwa kuwa kipindi ambacho Makamba anasema miundombinu ya umeme ilikuwa haifanyiwi ukarabati umeme ulikuwa haukatiki hovyo.

SIASA KATIKA SEKTA YA UMEME TANZANIA
Kukatika kwa umeme ni matokeo ya siasa ambazo zimesababisha maamuzi makubwa ya kitaalam yafanyike kisiasa.

Hata mjadala mkali kuhusu umeme uliotikisa Bunge la Januari, 2022 nao ulikuwa wa kisiasa zaidi. Ulitawaliwa na mashambulizi ya kisiasa ya mojamoja na vijembe dhidi ya waziri Makamba kana kwamba waziri huyo ndiye chanzo cha kukatika kwa umeme.

Baadhi ya wabunge walitaka kuonesha kuwa tatizo la kukatika kwa umeme lilikuwa limekwisha ila limerudi tu baada ya waziri Makamba kuanza kuongoza wizara ya Nishati, suala ambalo si kweli.

Ilivyo bahati, takwimu alizotoa mbunge wa Viti Maalamu, Jesca Kishoa wakati akichangia bungeni zilionesha kuwa tatizo la kukatika kwa umeme halijawahi kwisha. Mbunge Kishoa alisoma bungeni taarifa ya mwaka 2018 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) iliyoonesha kuwa mwaka 2017 umeme ulikatika mara 2,844 nchini Tanzania. Hii inamaanisha mwaka 2017 umeme ulikatika takribani mara saba kwa siku. Hiki ndiyo kipindi ambacho baadhi ya wabunge wanadai umeme ulikuwa haukatiki.

Siasa katika sekta ya umeme nchini Tanzania hazikuanza mwaka huu. Zilianza tangu wawekezaji binafsi waliporuhusiwa kuzalisha umeme mwanzoni mwa miaka ya 1990. Baadhi ya kampuni za wazalishaji binafsi wa umeme (Independent Power Producers) zilizoingia Tanzania zilikuwa ni IPTL, Richmond na Dowans. Wengi wa wazalishaji hawa huru walihusishwa na siasa za chama tawala, CCM. Lakini kuja kwao kuligubikwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa mwanzoni mwa 2008. Hata hivyo Lowassa akizungumza Bungeni kabla ya kujiuzulu, alilalamika kuwa alionewa kwa kutuhumiwa na kuhukumiwa bila kusikilizwa, hivyo alijiuzulu ma maslahi ya chama chake na serikali.

Ni wazi kuwa siasa zilichochewa na sekta hiyo kuwa chanzo kikubwa za cha fedha za dhuluma kwa wanasiasa waroho na wasiokuwa waaminifu. Hata vita vya kisiasa vilivyopiganwa bungeni Januari, 2022 zinaonyesha zinaweza kuhusishwa na hisia za ulaji wa fedha za umma katika sekta ya umeme.

Matokeo ya maamuzi kufanyika kisiasa ni kuwa mikataba yenye kasoro iliyoingiwa kati ya serikali na wazalishaji huru wa umeme ilifanya shirika la umeme nchini Tanzania, Tanesco, linunue umeme kwa bei za juu kutoka kwa wazalishaji hao. Jambo hili lilisababisha gharama kubwa za uendeshaji zilizozuia ukarabati wa miundombinu wa mara kwa mara. Majaribio ya serikali kuvunja mikataba yalisababisha kesi za muda mrefu mahakamani.

Fursa adimu
Tanzania ilishindwa kutumia ipasavyo fursa adimu ya kurekebisha sekta ya umeme nchini (eletricity sector reforms) mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Nchi ya jirani ya Kenya iliyoitumia fursa hii vizuri iliondokana na matatizo ya kukatika umeme kila siku. Kenya ilichukua hatua za haraka kutenganisha shughuli za uzalishaji wa umeme na zile za usafirishaji na ugavi.

Mwaka 1998 serikali ya Kenya iliunda shirika la uzalishaji umeme, KenGen na kuuza asilimia 30 ya hisa zake za KenGen kwa wananchi kupitia Soko la Hisa. Shirika hili ambalo linazalisha asilimia 65 ya umeme nchini Kenya linajiendesha kwa ufanisi mkubwa kwa sababu linawajibika kwa wanahisa walio wengi zaidi.

Kuundwa kwa KenGen kuliondoa majukumu ya kuzalisha umeme kutoka kwa shirika la Kenya Power ambalo kazi yake kubwa ni ugavi wa umeme. Kenya Power inanunua umeme kutoka KenGen na kuuza kwa watumiaji. Kenya Power nayo iko katika soko la hisa la Nairobi.

Kama hiyo haitoshi, katika jitihada za kuiondolea Kenya Power mzigo wa kujenga, kuendesha na kukarabati miundombinu ya gridi ya taifa, serikali ya Kenya iliunda shirika la Kenya Electric Transmmission Company (Ketraco) mwaka 2008. Kazi yake kubwa ni kupanga, kuchora, kujenga, kuendesha na kukarabati njia kuu zenye msongo mkubwa zinazosafirisha umeme katika gridi ya taifa na kati ya mkoa na mkoa.

Majukumu haya yanagharamiwa na serikali kwa kutumia pesa za kodi ya wananchi na mikopo ya riba nafuu kutoka kwa hisani. Nia ni kuondoa mzigo wa kugharamia ujenzi wa miundombinu mikubwa kutoka kwa Kenya Power na kupunguza bei ya umeme kwa walaji.

Kabla ya hapo ilibidi Kenya Power iwapelekee walaji gharama zote za kujenga na kukarabati miundombinu ya usafirishaji wa umeme kwenye njia kuu za gridi ya taifa. Kwa sasa Kenya Power imebaki na miundombinu inayosambaza umeme majumbani, kwenye ofisi na viwandani.

Muundo huu umefanya mfumo wa usafirishaji umeme nchini Kenya kuwa wa ufanisi mkubwa na umepunguza tatizo la kukatika umeme.

Pia sheria za Kenya zimeruhusu watumiaji wakubwa wa umeme kama vile viwanda kununua umeme moja kwa moja kutoka KenGen. Hii imepunguza tatizo la Kenya Power kuelemewa na mahitaji hasa wakati wa kilele cha matumizi ya umeme. Ripoti mbalimbali zinasema tatizo kubwa la mashirika ya umeme ya umma nchini Kenya kwa miaka ijayo itakuwa ni uhitaji unaopungua, si kuelemewa kwa miundombinu ya usambazaji.

Pamoja na yote hayo Kenya haijamaliza matatizo yake ya umeme. Lakini kuna ufanisi unaoonekana uliofanikishwa na kufanya maamuzi kitaalam na si kisiasa.

Kwa nini Tanzania isijifunze kutoka Kenya?
Isivyo bahati, Tanzania imeshindwa kujifunza kutoka Kenya na nchi nyingine za jirani. Wataalamu wamekuwa wakishauri kuhusu ulazima wa kuligawa shirika la Tanesco vipande vitatu kupunguza mzigo na gharama za uendeshaji na kuleta ufanisi na tija.

Wataalamu wanasema upungufu katika usafirishaji na ugavi wa umeme yataisha au kupungua kwa kiwangokikubwa pale yatakapoundwa mashirika tofauti ya kushughulika na kazi hizo kama ilivyo kwa Ketraco na Power Kenya. Lakini serikali badi haijakubaliana na hoja hiyo ambayo pia imewahi kujitokeza pia katika mijadala ya Bunge. Wakati akijibu hoja za wabunge Februari 15, 2022 Waziri Makamba aliyataja badhi ya matatizo ya usafirishaji wa umeme.

Alisema njia za umeme zenye msongo mdogo wa 33kV ambazo zinatakiwa zibebe umeme mdogo kupeleka mitaani katika umbali usiozidi kilometa 100 ndizo zinazosafirisha umeme wa msongo mkubwa kwa kilometa zaidi ya 1,000. Kwa mfano njia ya msongo mkubwa ya Dodoma-Kongwa-Mpwapwa-Gairo-Kiteto yenye umbali wa kilometa 1,600 inabebwa na laini ya umeme ya 33kV jambo ambalo ni sababu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara. Njia ya umeme ya 11kV inayopaswa kupeleka umeme majumbani ndani ya kilometa 30 ndiyo inayopeleka umeme Lindi kutoka Dar es Salaam, umbali wa zaidi ya kilometa 100. "Katika hali hii umeme lazima utakuwa unstable [usio wa uhakika]," alisema Makamba. Makamba aliongeza kuwa wizara yake imeshapata Dola za Kimarekani bilioni 1.9 za kukarabati na kujenga miundombinu mipya ya umeme nchini. "Tunaomba muda...tuvumiliane, tupeane muda."

Machi 24 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja wa Rais Samia Bwana Makamba ameomba Watanzania waipe serikali angalau miaka miwili kuijenga upya miundombinu ya kusafirisha umeme.

Ni hakika kuwa katika suala la umeme nchini Tanzania, muda utaongea. Waziri Makamba anaonekana kuwa ana nia nzuri ya kuboresha upatikanaji wa umeme nchini.

Lakini kama siasa hazitakwisha na kama shirika moja tu la Tanesco litaendelea kubeba mzigo wote wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, waziri mwingine wa Nishati anaweza akarudia maneno ya "tupeane muda" miaka kumi ijayo.

Kukatika kwa umeme nchini Tanzania si tatizo lililoanza jana na ambalo ufumbuzi wake utakuja kwa kuijaza Tanesco 'mapesa'. Tatizo la umeme Tanzania ni la miaka mingi na linatakiwa liangaliwe kwa upana wake na uzito unaostahili.

Uzalishaji wa umeme si tatizo Tanzania
Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, yaani "energy mix." Ina uwezo wa kuzalisha umeme wa maji kwa zaidi ya 4,000MW na umeme wa jotoardhi (geothemal) kwa takribani 5,000MW. Asilimia 10 ya nchi ya Tanzania inafaa kuzalisha umeme wa upepo. Mradi wa kuzalisha umeme kw anguvu ya upepo mkoani Singida haukuwahi kuanza. Nchi nzima inafaa kuzalisha umeme wa jua. Uwepo wa gesi asilia wa zaidi ya futi za ujazo trilioni 60 unamaanisha kuwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme kutoka gesi asilia haupimiki. Ifahamike kuwa kwa sasa Tanzania inategemea gesi asilia kuzalisha umeme wake kwa kiasi kikubwa kuliko nishati nyingine yoyote japo bado kuna fursa ya kuongeza uzalishaji huo.

Upatikanaji wa madini ya urani nao pia unaipa Tanzania nafasi ya kuzalisha umeme wa nyuklia kama serikali ikitaka. Tafiti zilizothibitishwa zinaonesha kuwa kuna madini ya urani katika mikoa ya Ruvuma, Dodoma, Singida, Manyara na Arusha japo hayajaanza kuchumbwa.

Kwa kifupi Tanzania haitakiwi kuwa na matatizo ya umeme. Inatakiwa iuze umeme nchi za nje. Lakini rasilimali kama hizi huwa haziwezi kuifaidisha nchi kama siasa zake hazikidhi mahitaji na kuleta tija kwa manufaa ya watu wake.

UHABA WA MAJI
Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linakadiria kwamba tatizo la uhaba wa maji, litakuwa moja ya janga kubwa duniani katika muongo mmoja ujao. Hata Ripoti ya tano ya tathimini ya mabadiliko ya tabia nchi ya mwaka 2015 ilionya kuhusu upungufu wa rasilimali ya maji duniani. Huenda sasa athari zimeanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Afrika Mashariki kama Somalia, Ethiopia mashariki na kati, maeneo ya Pwani ya Kenya na Tanzania, likiwemo jiji la Dar es Salaaam. Jiji hilo linalokadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 6 linapitia kwenye majaribu ya uhaba wa maji katika kipindi cha hivi karibuni huku upatikanaji wa maji ukipungua mpaka asilimia 64%, kwa mujibu wa mamlaka za mkoa huku mahitaji halisi ya maji ya jiji hilo kwa siku ni lita zaidi ya milioni 450.

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka ni kwamba kiwango cha uzalishaji maji katika mitambo ya Ruvu juu na chini inayotumika kusambaza maji katika jiji hilo na maeneo ya Pwani kimepungua kutoka lita milioni 466 kwa siku mpaka 300.

Hali hii inakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tangu Mamkala ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) itoe tathimini yake ikisema jiji hilo linajitosheleza kwa maji kwa karibu asilimia 96. Kulikoni sasa?

Nini kimetokea na kwanini kina kipungue?
Kupungua kwa kina cha maji kunakotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bwana Makalla kunatokana na upungufu wa mvua ambao pamoja na sababu zingine unahusishwa pia na athari za moja kwa moja za mabadiliko ya tabia nchi.

Na upungufu huu haugusi jiji hili pekee, karibu maeneo mengi ya nchi hiyo japo makali yake hayawezi kufanana. Kwa mujibu wa hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara ya maji kwa mwaka huu wa fedha hadi kufikia Aprili, 2022 hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini ilipungua kwa kutoka asilimia 86.5 hadi 86.

Mkuu wa mkoa anasema hakuna hila katika upungufu huo wa maji. “Hakuna makusudi yoyote iliyofanyika labda tuweze kukosa maji, suala ni mvua, ni kwamba kina cha maji kimeshuka’, alisema na kuongeza, ‘Upatikanaji wa maji katika chanjo ni asilimia 64% sio mia kwa mia, kwa hiyo kwa vyovyote vile lazima kutakuwa na kamgao ka maji kwa sababu maji hayapatikani inavyotakiwa’.

Makali ya mgao yanonekana. Harusi Masanja, mkazi wa Salasala anasema ‘Ninapoishi ni mita chache kutoka tanki kubwa la maji la DAWASA, lakini nyumbani hatuna maji, na haijaanza jana na sijui itaisha lini’.

Cop27 kuiokoa Dar es salaam na miji mingine Afrika?
Viongozi wa dunia wakiwa sehemu ya waalikwa 200 wanajiandaa kukutana mwezi ujao huko Misri katika mkutano wa 27 wa mabadiliko ya tabia nchi (COP27) chini ya Umoja wa Mataifa.

Ni moja ya mikutano ya kilele ya Umoja wa mataifa inayoangazia namna ya kupunguza joto duniani ili kuondoa athari zake, ikiwemo ukame na kupunguza vina vya maji.

Ingawa matokeo yake si ya haraka, nchi zinazoendelea kama Tanzania zinatarajiwa kuwekewa mipango ya fedha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari zake.

Mwaka 2009, nchi zilizoendelea zilijitolea kutoa dola bilioni 100 kwa mwaka, ifikapo mwaka 2020, kwa nchi zinazoendelea ili kuzisaidia kupunguza utoaji wa gesi hizo na kujiandaa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Fedha hizi ni kupunguza shughuli zinazochangia ongezo la joto duniani. Jiji kama Dar es salaam litakuwa moja ya mnufaika kama hilo litafanyiwa kazi ipasavyo. Hata kama litakua ni la muda mrefu.

Kwa mujibu wa DAWASA, hatua za sasa za muda mfupi, mradi wa kigamboni utakua msaada ukitarajia kupunguza uhaba wa maji hasa katika wilaya za Ilala na Kigamboni.

Wakati ikiendelea kusubiri kina cha maji kiongezeke kwenye mitambo yake kwa "kudra za mvua" mambo mengine ambayo yanatajwa kufanywa na Dawasa sasa ni kutumia visima virefu zaidi ya 170 vilivyopo ambavyo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amepanga kuvitembelea ijumaa hii​
 
Hatuna great thinker wizarani, Makamba wasiliana na heche miaka miwili tatizo la umeme litamalizwa na upepo na jua
 
Wataalamu wamehamia kwenye kusifia kila kitu, hawatumii utaalamu wao kushauri bali wao ndo wanashauriwa na Wanasiasa wafanye nini. NI UJINGA MTUPU!!

Hii tabia ya Mama ametoa maelekezo siielewi kiukweli, ni kwamba ukiwa Rais unajua mambo yote?

Nilitegemea 'kusikia kuwa Wataalamu wamekaa na Mhe. Rais tukakubaliana kuwa...'

Ina maana Wataalamu wa Tanzania badala ya kushauri ni nini kifanyike, wao ndo wanashauriwa na kuelekezwa wafanye nini!

Umuhimu wa wataalamu ni nini? Maana wamekuwa kama Maaskari, wanapewa amri tu, akili zao ziko kwenye vyeti..wakishaajiriwa wanageuka kuwa _zidumu fikra za Chama Cha Mapinduzi.

Wananchi ndo tunaoumia, wao maumivu yao yanaishia kwenye televisheni tu.
 
"Hakuna kichaka ambacho makada wengi wa CCM wameiba pesa za umma Kama kichaka Cha umeme" John Heche

Nchi imejaa wapumbavu tu hii Dunia inapitia kipindi kigumu Cha mabadiliko ya tabia ya nchi wakati huo huo serikali ya mazwazwa wa Tanzakiza ina jenga chanzo Cha umeme wa maji.

Mzee kikwete alitudanganya wazi wazi Watanzania kuhusu umeme wa gesi mwisho hakuna lolote upigaji tu ndo umejaa
 
Africa tumelogwa nn au ni wajinga wajinga wengi ndo wanatuongoza yaani bado tunategemea vyanzo vile vile vya maji na umeme😀😀dar kunakuwaje na shida ya maji wakati kuna bahari ya hindi, au mwanza si kuna ziwa victiroria au tunasubiri msaada EU, Kutandaza mabomba ambayo yatasaidia kupata maji kwa matumizi ya nyumbani na kilimo, tunaishi kizamani sana, pesa za walipa kodi wanazibania kama zao vile ili wazipige badala ya kufanyia development projects, maza faka africans leaders
 
Ta

Tatizo Tanzania kuna viongozi wameunda system zao ambazo hawataki kuingiliwa wala kushauliwa , na wanajiona wenyewe tu ndo wanaweza kuongoza nchi, sema marais wote waliotuongoza ni wamichongo tu kila siku shida ya maji na vyanzo vipo kibao , eti yanategemea vyanzo vile vile kama majinga😀😀wakati kuna mito, mabwawa, maziwa na bahari , je nchi za majangwani wasemaje na utasikia Tanzania kuna njaa eti kisa hakuna mvua😀😀aisee hatuna viongozi tunawapigaji tu ,
 
Du,ndefu sana, anyway ngoja,, watanzania hatupendi kusoma makala ndefu
 
Wanakuwa wamepiga percent zao tu hao, wakishachukua chao sisi tunabaki na mgawo..hii nchi tukisubiri kuletewa kila kitu kwa mapenzi ya watawala, kiama itafika tukiwa bado gizani!
 
Ta

Tatizo Tanzania kuna viongozi wameunda system zao ambazo hawataki kuingiliwa wala kushauliwa , na wanajiona wenyewe tu ndo wanaweza kuongoza nchi, sema marais wote waliotuongoza ni wamichongo tu kila siku shida ya maji na vyanzo vipo kibao , eti yanategemea vyanzo vile vile kama majinga😀😀wakati kuna mito, mabwawa, maziwa na bahari , je nchi za majangwani wasemaje na utasikia Tanzania kuna njaa eti kisa hakuna mvua😀😀aisee hatuna viongozi tunawapigaji tu ,
Katiba mpya ndo njia pekee ya Tanzania kusonga mbele kimaendeleo.

Hii tabia ya kutegemea 'huruma' ya kiongozi katika kutimiza wajibu wao ndo inatuponza! TUDAI KATIBA MPYA KWA NAMNA YOYOTE ILE!!
 
Africa tumelogwa nn au ni wajinga wajinga wengi ndo wanatuongoza yaani bado tunategemea vyanzo vile vile vya maji na umeme😀😀dar kunakuwaje na shida ya maji wakati kuna bahari ya hindi, au mwanza si kuna ziwa victiroria au tunasubiri msaada EU, Kutandaza mabomba ambayo yatasaidia kupata maji kwa matumizi ya nyumbani na kilimo, tunaishi kizamani sana, pesa za walipa kodi wanazibania kama zao vile ili wazipige badala ya kufanyia development projects, maza faka africans leaders
Mifumo mibovu ndo anguko letu, wanasiasa wamekuwa wakija na miradi ambayo wanajua fika kuwa itakwama, lakini wanaendelea nayo tu kwakuwa wana asilimia zao ndani yake.
 
Du,ndefu sana, anyway ngoja,, watanzania hatupendi kusoma makala ndefu
Apo ndipo tunapopigiwa, kwenye kusoma Watanzania wengi wanafichiwa maharifa, hekima,ukweli na miongozo ya kimsingi juu ya mstakabali wa nchi yetu.
Soma mpaka mwisho utojuta
 
Back
Top Bottom