Si zaidi katika historia ya muungano bali ni katika wimbo huu wa Western Jazz

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,924
30,273
SI ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MUUNGANO BALI NI KATIKA WIMBO HUU WA WESTERN JAZZ BAND 1964

Ilikuwa nawasha gari langu usiku nikaliegeshe kwa walinzi mtaa wa pili.
Gari limewaka na radio inasema.

Nimeshtuka naisikia sauti ya rafiki yangu Juma Mnonji anahojiwa kuhusu maisha ya Ahmed Kipande Band Leader wa Iliyokuwa Kilwa Jazz.

Majina yanayomtoka ni majina ya watu niliowajua toka udogoni hadi nakuwa kijana na akili zangu.

Ahmed Kipande, Juma Mnonji anamwita Amadi, Hassan "Kichwa" Shabani, Duncan Njilima, Ndume na dada yetu Pili Abeid.

Nimezima gari nisikilize radio kwa utulivu.

Hayo yote niliyoandika hapo juu yote yana historia na kufungamana na maisha yangu ya udogoni.

Juma Mnonji anahadithia anamweleza Ahmad Kipande mpiga saxophone na clarinet katika Kilwa Jazz lini aliasisi Kilwa Jazz.

Kilwa Jazz iliasisiwa mwshoni mwa miaka ya 1950 Mtaa wa Gogo nyumbani kwa akina Abdul Kigunya.

Nimeitaja nyumba kwa anuani ya Abdul Kigunya kwa kuwa Abdul ni rika langu tukicheza pamoja.

Hii nyumba ilikuwa ya mama yake.

Nyumba hii ilikuwa jirani sana na nyumba ya mmoja wa baba zangu wadogo Mzee Abdallah.

Sisi watoto wa mtaani tukisikia Kilwa wanafanya mazoezi na walikuwa wakifanya nyakat za usiku kama saa moja hivi basi sote tutajazana nje dirishani tunachungulia ndani.

Siku ya pili nyimbo zote tunaziimba.

Nawakumbuka rafiki zangu hawa niliouwanao wengi waetangulia mbele ya haki, Abbas Mwamba na nduguye Kurwa, Abdul Kigunya, Hamza Msanga Mapesa, Selemani na ndugye Kibira, Gopi, Mohamed Kitunguu na nduguye Ali ''Nakioze'' Hussein.

Juma Mnonji anamweleza mtangazaji anamwambia Kilwa Jazz ilianzishwa Mtaa wa Gogo nyumbani kwa Mama mmoja kutoka Kilwa.

Juma Mnonji anaendelea na simulizi yake anamtaja Hassan Kichwa mpiga lead guitar wa Kilwa Jazz na Ndume muimbaji.

Jina la kwanza la Ndume silifahamu.

Ndume nitakuja kukutananae ukubwani miaka ya 1970 sote tukiwa wafanyakazi wa East African Cargo Handling Services.

Hassan Kichwa ni mume wa dada yetu Pili Abeid.

Mdogo wake Dada Pili, Juma "Spencer" Abeid ni rika langu na mchezo wetu mmoja na nyumba zetu jirani.

Nikimfuata Spencer nyumbani kwao namkuta Hassan Kichwa na guitar lake anapiga.

Mimi umri wangu miaka 12 mwaka huo 1964 Tanganyika na Zanzibar zinaungana.

Juma Mnonji anaendelea na simulizi sasa anaeleza ilikuwaje nyimbo hii ikatungwa.

Juma Mnonji anaeleza kuwa ilikuwa kawaida ya Kilwa Jazz kutunga nyimbo zinazoakisi hotuba za Mwalimu Nyerere kama juhudi za kuwahamasisha wananchi katika maendeleo.

Kilwa Jazz Band ndiyo waliopiga nyimbo ya uhuru wa Tanganyika mwaka wa 1961 ambayo Juma Mnonji kaeleza kuwa ilikuwa dua ya kuiombea nchi:

''Ewe Mola tunakuomba ibariki Tanganyika,
Tanganyika na jiranI zake,
Uhuru tumeshaupata lakini nyoyo zina shaka,
Wenzetu bado wateseka,
Wakoloni wamewashika,
Eee mama.''

Nyimbo hii ilikuwa na mashairi ya kuomba msaada kwa Mungu kuwa nchi nyingine zilizokuwa chini ya ukoloni zikomboke.

Naikumbuka sana nyimbo hii kwani ilikuwa katika maktaba ya baba yangu na ni zile santuri kubwa za 78 RPM.

Sasa siku hiyo ya kutia saini makubaliano ya muungano dada yetu Pili Abeid akamwambia mumewe Hassan Kichwa kuwa Kilwa Jazz Band lazima itunge wimbo wa muungano.

Wimbo wa muungano uliokuja kurekodiwa na Western Jazz Band na haukuwa wimbo waliotunga wao.

Huu ni mwimbo wa bendi ya Orchestre Bantou kutoka Congo Brazzaville iliyokuwa na mpigaji guitar hodari sana Papa Noel.

Hilo guitar ambalo linasika katika nyimbo hii ya Western Jazz Band limepigwa na Duncan Njilima ambae amefariki majuma machache yaliyopita.

Juma Mnonji alieleza kuwa Kilwa Jazz Band walikuja kumchukua Duncan Njilima aje kupigia kwao kwa sababu Hassan Kichwa lau alikuwa ''soloist,'' hodari lakini alielemea zaidi katika mipigo ya Cha Cha.

Wakati ule vijana wengi wakipenda Pachanga ambayo Duncan Njilima alikuwa bingwa kana unavyosikia anavyomuiga Papa Noel.

Kwangu mimi muungano haukunigusa hapa kama nilivyoguswa na hii nyimbo ya muungano na watu hawa niliowataja hapa, watu ambao nikiwaona katika mitaa ya Kariakoo ya 1960s.

Iko siku nimepita Mtaa wa Mchikichi nje ya Kumekucha Auction Mart.
Huu ulikuwa mnada maarufu wa Mzee Hamza Kumekucha.

Pale niliona baadhi ya vyombo vya Kilwa Jazz Band vikisubiriwa kupigwa mnada.

Nakumbuka katika siku zake za mwisho kumuona Ahmed Kipande wakati huo mgonjwa kapooza lakini anaweza kujikongoja akipita Mtaa wa Sikukuu akitembea kwa miguu.

Mtaa wa pili tu kutoka mtaa hhu ni Mtaa wa Gogo ambapo Ahmed Kipande alianzisha Kilwa Jazz.

''Nyerere na Karume wastahili kusifiwa na wananchi wote wa Tanzania kwa kutuletea muungano wa Tanzania.''
 
Nazitafuta sana hizo 78 rpm, huwa nazinunua moja elfu 5. Kama unamfahamu mtu mwenye nazo anitafute kwa 0714829688. Shukrani sana. .

Historia nyingi za Africa zinaanza na mkoloni, tumesahau kuwa tungeweza kupata historia hizi kwenye mapokeao kama santuri. Kuna santuri za 78 nyingi zina nyimbo za kilimo, nyimbo za sifa kwa machifu, historia ya kabila flani nk. .
 
Gily,
Gallotone, Johannesburg wajaribu hawa ndiyo wakirekodi miziki mingi ya Afrika katika 1950s.
 
Si unajua walishaacha uzalishaji zaidi ya miaka 45 iliyopita
Kampuni nazotafuta Gallotone, HMV AMC and LON series, Mzuri, Jambo, Columbia, Hits, Mwangaza, CMS, Trobadour, HABARI, Tropic, TREK, TOM TOM, OPIKA, FURAHA, RADIO ETC. .

Nalenga kuzitafuta ambazo ziko majumbani mwa watu. .
 
Sikuwa na taarifa hizo.

Ningependa sana kufahamu santuri ulizonazo na wanamuziki wake.

Baba yangu alikuwa na collection kubwa sana ya toka Septet Habanero, Louis Armstrong, Alma Cogan, OK Jazz, Ngoma etc.
 
SI ZAIDI KATIKA HISTORIA YA MUUNGANO BALI NI KATIKA WIMBO HUU WA WESTERN JAZZ BAND 1964

Ilikuwa nawasha gari langu usiku nikaliegeshe kwa walinzi mtaa wa pili.
Gari limewaka na radio inasema.

Nimeshtuka naisikia sauti ya rafiki yangu Juma Mnonji anahojiwa kuhusu maisha ya Ahmed Kipande Band Leader wa Iliyokuwa Kilwa Jazz.

Majina yanayomtoka ni majina ya watu niliowajua toka udogoni hadi nakuwa kijana na akili zangu.

Ahmed Kipande, Juma Mnonji anamwita Amadi, Hassan "Kichwa" Shabani, Duncan Njilima, Ndume na dada yetu Pili Abeid.

Nimezima gari nisikilize radio kwa utulivu.

Hayo yote niliyoandika hapo juu yote yana historia na kufungamana na maisha yangu ya udogoni.

Juma Mnonji anahadithia anamweleza Ahmad Kipande mpiga saxophone na clarinet katika Kilwa Jazz lini aliasisi Kilwa Jazz.

Kilwa Jazz iliasisiwa mwshoni mwa miaka ya 1950 Mtaa wa Gogo nyumbani kwa akina Abdul Kigunya.

Nimeitaja nyumba kwa anuani ya Abdul Kigunya kwa kuwa Abdul ni rika langu tukicheza pamoja.

Hii nyumba ilikuwa ya mama yake.

Nyumba hii ilikuwa jirani sana na nyumba ya mmoja wa baba zangu wadogo Mzee Abdallah.

Sisi watoto wa mtaani tukisikia Kilwa wanafanya mazoezi na walikuwa wakifanya nyakat za usiku kama saa moja hivi basi sote tutajazana nje dirishani tunachungulia ndani.

Siku ya pili nyimbo zote tunaziimba.

Nawakumbuka rafiki zangu hawa niliouwanao wengi waetangulia mbele ya haki, Abbas Mwamba na nduguye Kurwa, Abdul Kigunya, Hamza Msanga Mapesa, Selemani na ndugye Kibira, Gopi, Mohamed Kitunguu na nduguye Ali ''Nakioze'' Hussein.

Juma Mnonji anamweleza mtangazaji anamwambia Kilwa Jazz ilianzishwa Mtaa wa Gogo nyumbani kwa Mama mmoja kutoka Kilwa.

Juma Mnonji anaendelea na simulizi yake anamtaja Hassan Kichwa mpiga lead guitar wa Kilwa Jazz na Ndume muimbaji.

Jina la kwanza la Ndume silifahamu.

Ndume nitakuja kukutananae ukubwani miaka ya 1970 sote tukiwa wafanyakazi wa East African Cargo Handling Services.

Hassan Kichwa ni mume wa dada yetu Pili Abeid.

Mdogo wake Dada Pili, Juma "Spencer" Abeid ni rika langu na mchezo wetu mmoja na nyumba zetu jirani.

Nikimfuata Spencer nyumbani kwao namkuta Hassan Kichwa na guitar lake anapiga.

Mimi umri wangu miaka 12 mwaka huo 1964 Tanganyika na Zanzibar zinaungana.

Juma Mnonji anaendelea na simulizi sasa anaeleza ilikuwaje nyimbo hii ikatungwa.

Juma Mnonji anaeleza kuwa ilikuwa kawaida ya Kilwa Jazz kutunga nyimbo zinazoakisi hotuba za Mwalimu Nyerere kama juhudi za kuwahamasisha wananchi katika maendeleo.

Kilwa Jazz Band ndiyo waliopiga nyimbo ya uhuru wa Tanganyika mwaka wa 1961 ambayo Juma Mnonji kaeleza kuwa ilikuwa dua ya kuiombea nchi:

''Ewe Mola tunakuomba ibariki Tanganyika,
Tanganyika na jiranI zake,
Uhuru tumeshaupata lakini nyoyo zina shaka,
Wenzetu bado wateseka,
Wakoloni wamewashika,
Eee mama.''

Nyimbo hii ilikuwa na mashairi ya kuomba msaada kwa Mungu kuwa nchi nyingine zilizokuwa chini ya ukoloni zikomboke.

Naikumbuka sana nyimbo hii kwani ilikuwa katika maktaba ya baba yangu na ni zile santuri kubwa za 78 RPM.

Sasa siku hiyo ya kutia saini makubaliano ya muungano dada yetu Pili Abeid akamwambia mumewe Hassan Kichwa kuwa Kilwa Jazz Band lazima itunge wimbo wa muungano.

Wimbo wa muungano uliokuja kurekodiwa na Western Jazz Band na haukuwa wimbo waliotunga wao.

Huu ni mwimbo wa bendi ya Orchestre Bantou kutoka Congo Brazzaville iliyokuwa na mpigaji guitar hodari sana Papa Noel.

Hilo guitar ambalo linasika katika nyimbo hii ya Western Jazz Band limepigwa na Duncan Njilima ambae amefariki majuma machache yaliyopita.

Juma Mnonji alieleza kuwa Kilwa Jazz Band walikuja kumchukua Duncan Njilima aje kupigia kwao kwa sababu Hassan Kichwa lau alikuwa ''soloist,'' hodari lakini alielemea zaidi katika mipigo ya Cha Cha.

Wakati ule vijana wengi wakipenda Pachanga ambayo Duncan Njilima alikuwa bingwa kana unavyosikia anavyomuiga Papa Noel.

Kwangu mimi muungano haukunigusa hapa kama nilivyoguswa na hii nyimbo ya muungano na watu hawa niliowataja hapa, watu ambao nikiwaona katika mitaa ya Kariakoo ya 1960s.

Iko siku nimepita Mtaa wa Mchikichi nje ya Kumekucha Auction Mart.
Huu ulikuwa mnada maarufu wa Mzee Hamza Kumekucha.

Pale niliona baadhi ya vyombo vya Kilwa Jazz Band vikisubiriwa kupigwa mnada.

Nakumbuka katika siku zake za mwisho kumuona Ahmed Kipande wakati huo mgonjwa kapooza lakini anaweza kujikongoja akipita Mtaa wa Sikukuu akitembea kwa miguu.

Mtaa wa pili tu kutoka mtaa hhu ni Mtaa wa Gogo ambapo Ahmed Kipande alianzisha Kilwa Jazz.

''Nyerere na Karume wastahili kusifiwa na wananchi wote wa Tanzania kwa kutuletea muungano wa Tanzania.''
Inatia shaka kuona mwandishi mkongwe kama unavyojinasibu kutokujua tofauti ya umoja na wingi.

Wimbo vs Nyimbo.
 
Lukubuzo mimi najinasibu?
Najinasibu vipi?

Kuhusu "wimbo" na "nyimbo" nimeulizwa mara nyingi na nimeeleza.

Mimi nazungumza Kiswahili cha Pwani ambacho ni tofauti na Kiswahili kinachosemwa na watu wenye asili ya Bara.

Watu wa Bara wanasema "wimbo."
Sisi watu wa Pwani tunatamka "nyimbo."

Hakuna wingi wala umoja.
Watu wa Pwani wanasema "upungufu" watu wa Bara ni "mapungufu."

Halikadhalika "saa" na "masaa."

Hili lilikuwa jambo la kuniuliza tu kuwa kwa nini nasema "nyimbo" badala ya "wimbo" ningekufahamisha.

Hapakuwa na haja ya kuja na suala la kujinasibu.
Labda nikuulize una tatizo na uandishi wa Mohamed Said?
 
Gily,
Sikuwa na taarifa hizo.

Ningependa sana kufahamu santuri ulizonazo na wanamuziki wake.

Baba yangu alikuwa na collection kubwa sana ya toka Septet Habanero, Louis Armstrong, Alma Cogan, OK Jazz, Ngoma etc.
Mie nina East African music only na ndio huwa nazitafuta. Hao Septeto pia wako kwenye GV series HMV. Za kizungu na za kutoka mikoa mingine sinazo na sijapenda kuzitafuta hizo. Nikipita kwenye santuri zangu nikiwa nimetulia nitakutumia sound clips baadhi ya hizo nilizonazo. Thank you. .
 
kizungu na za kutoka mikoa mingine sinazo na sijapenda kuzitafuta hizo. Nikipita kwenye santuri zangu nikiwa nimetulia nitakutumia sound clips baadhi ya hizo nilizonazo. Thank you. .
[/QUOTE]
Gily,

Lukubuzo mimi najinasibu?
Najinasibu vipi?

Kuhusu "wimbo" na "nyimbo" nimeulizwa mara nyingi na nimeeleza.

Mimi nazungumza Kiswahili cha Pwani ambacho ni tofauti na Kiswahili kinachosemwa na watu wenye asili ya Bara.

Watu wa Bara wanasema "wimbo."
Sisi watu wa Pwani tunatamka "nyimbo."

Hakuna wingi wala umoja.
Watu wa Pwani wanasema "upungufu" watu wa Bara ni "mapungufu."

Halikadhalika "saa" na "masaa."

Hili lilikuwa jambo la kuniuliza tu kuwa kwa nini nasema "nyimbo" badala ya "wimbo" ningekufahamisha.

Hapakuwa na haja ya kuja na suala la kujinasibu.
Labda nikuulize una tatizo na uandishi wa Mohamed Said?
Hapo sio ubara wala upwani. Hapa tunazungumzia kiswahili sanifu cha BAKITA.
 
Hapo sio ubara wala upwani.Hapa tunazungumzia kiswahili sanifu cha BAKITA.
Luku...
Mimi kwa bahati mbaya si mtu wa kukubali kitu kwa kuwa tu kimetoka kwa watu fulani wanaoaminika.

Sasa ingawa umewataja BAKITA mimi bado msimamo wangu ni ule ule wa kukizungumza Kiswahili kama nilivyowakuta wazee wangu wakikizungumza.

"Mapungufu," inawezekana kwako ni Kiswahili sanifu lakini kwangu "masaa," na mfano wa hayo ni Kiswahili cha watu wa Bara.

Usiamini kila unacholetewa.

Ningeamini historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981)leo mngekuwa bado mnasoma historia yenye upungufu mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom