Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,519
- 86,070
Kuna kitu kinaniumiza kichwa sana, nimejaribu kunywa maji na kumeza dawa imeshindikana, nauliza tu; kama nikikuudhi nisamehe; Eti ile kauli mbiu ya mwaka huu ya akina Magamba inayoenda kwa "Ari zaid, Nguvu Zaidi, Kasi Zaidi" bado ipo au ilikufa? Mukama simpati kwenye simu na Nape nae ka-block email yangu, ningewauliza, naombeni mnisaidie....Ipo? Na kama Ipo, je inatumika bado? maana sijaona kanga wala tisheti wala caps za kijani na njano zikiwaprinted kwa maandishi hayo kama kipindi kile kabla ya ngozi kugeuka kuwa gamba, nawakilisha