Si lazima mpaka wa nchi uwe katikati ya ziwa. Tutumie usomi wetu Tusimame kwenye ukweli

Watu mnaoongelea ramani badala ya kuongelea definition ya mpaka. Angalia mwenzutu Steven Sambali katuwekea ramani mbili zinazotofautiana kuhusu mpaka huo; sasa nyie wahubiri wa ramani mtasema ni upi mpaka sahihi? Hata Google wametumia dots kwenye mpaka ule kwa vile wanajua kuwa hauna uhakika. Tujadili sheria na mikataba zinazounda mkataba ule.
 
tunachoweza kufanya ni kuwataja wamalawi wote ambao wamekuwa wakiishi kwetu kama watanzania na pia wameshika au wanashika nyazifa mbalimbali serikalini kwani hao ndio silaha yao kubwa kumbuka kuwa na wingi wa jeshi au zana bora hakukuhakikishii ushindi isitoshe pamoja na matumizi yetu kuwa makubwa kuwashinda tumekuwa tukifanya usanii wakati wao wananunua zana sahihi kumbuka ufisadi wa helicopter mbovu za jeshi
 
Mleta mada, your point is......

Hamna hata tone la maji kwenye Ziwa Nyasa, na Watanzania mkidasa tone moja tu mmeingilia mamlaka halali ya nchi nyengine!Na wakitaka Malawi inaweza kuleta jeshi lake Mbeya kwenye maji yake, na kuwazuilia watu hata kuchota maji!

Hivi kokote kule duniani kuna mpaka unaoundwa na fukwe ya maji?

Nchi zenye migogoro ya kimaeneo ya bahari huko Asia (Ufilipino, Vietnam, China), wanawania visiwa (land) kwa sababu by default anaemiliki ardhi, ndie anaemiliki bahari pembezoni mwa visiwa hivyo. (sheria za kimataifa zinaamuru kuwa bahari iliyozunguka visiwa hivyo kwa maili kadhaa ni ya mwenye visiwa)

Haingii akilini kuwe na ziwa, kisha Hadi tone la mwisho la Ziwa Hilo ni eneo la nchi nyengine.
 
Yaani huyu naye atapata kitambulisho cha uraia. Sijui tufanyeje ili kuwatambua hawa mabwabwa waliojificha nchini kwetu? Kilosa watu walipiga kelele kwamba Mkulo ni m-Malawi nani awasikilize? Sasa ona wanavyojenga hoja za kuegemea upande wao! Mtoa hoja amejiweka wazi kabisa ni mmoja wa mabwabwa aliyejificha nchini mwetu! MODs naomba huyu bwana tumsalimishe kwa TISS haraka kabla hajazawadiwa u-RC! CCM mnawajibika kwa kubeba watu kama hawa!
 
Tuungane kwa lipi mkuu? Uzalendo upo hii? Kwa ajili ya nini? Acha tuconcetrate kwenye matatizo ya ndani! Hadi sasa mwangwi migomo, change ya rada, rushwa tanesco haujaisha. Acha kesi iende the Hague.
Yanapokuja masuala ya nchi uzalendo ni muhimu haijalishi ni hoja gani.Hoja yako ya kuilaumu serkali eti inataka kutusahaulisha matatizo ya nchi nadhani haina mantiki.Cha msingi tuungane wote tujue mwisho wa hili ni nini.Na inawezekana unaongea hayo maneno vile wewe hauishi kyela...
 
moja wapo ya akili fupi sana, unajua humu ndani kuna wamalawi wengi tuu ambao walilowea huku kwetu, tukawalisha tukawasafisha na kuwavisha nguo, wamepata akili na elimu sasa wamekuwa mashushushu wa nchi yao...unapoongelea suala la mipaka ya nchi ya tz, hasa kuhusu ziwa nyasa, usilinganishe kabisa na natron au tanganyika...kwasababu natron hatujawahi kuwa na ugomvi na kenya...utofauti wake na nyasa ni kwamba, nyasa imekuwa kwenye mtafaruku tangu tupate uhuru, na mtafaruku huo haujawahi kutatuliwa....hivyo kusema kwamba kwasababu natron mpaka haupo katikati basi na nyasa hivyohivyo ni upungufu wa akili, na inaonyesha wazi wewe si mtanzania, ni mmalawi unataka kutupiga changa la macho watz hapa.....je? kuna mtafaruku wowote tangu uhuru tuliwaipata na kenya kuhusu natron? au ziwa lingine lolote lile? hapana.....ila suala la nyasa lina mtafaruku na halijawahi kutatuliwa once and for all, sasa mmoja akisema anatafuta mafuta mle wakati suala halijatatuliwa ni uchokozi na dharau......tz tumekuwa tukitumia ziwa lile kwa muda, tumejenga bandari mle pale mbambabay na kyela, tumekuwa tukisafirisha bidhaa zetu kwa meli toka mbinga hadi ludewa hadi kyela, tumekuwa tukivua samaki tupendavyo hadi katikati ya ziwa,...sasa leo kwasababu kuna mafuta na wao kuona kuwa hatukutatua mgogoro ndo waseme ziwa lote lao, kwasababu sisi hatupo au wametudharau?......akili za mbayuwayu...

Attached intelligence,
 
Yaani huyu naye atapata kitambulisho cha uraia. Sijui tufanyeje ili kuwatambua hawa mabwabwa waliojificha nchini kwetu? Kilosa watu walipiga kelele kwamba Mkulo ni m-Malawi nani awasikilize? Sasa ona wanavyojenga hoja za kuegemea upande wao! Mtoa hoja amejiweka wazi kabisa ni mmoja wa mabwabwa aliyejificha nchini mwetu! MODs naomba huyu bwana tumsalimishe kwa TISS haraka kabla hajazawadiwa u-RC! CCM mnawajibika kwa kubeba watu kama hawa!

Hii nchi kwa Mara ya kwanza imetawaliwa na Mtanzania,waliopita wote si wa tz.
 
Fafanua, nani kajisema ana akili kubwa. Binafsi sijasema wanaounga au kipinga mkono haja ya Malawi wana akili kubwa au ndogo.

Nimeleta findings zangu na nitafurahi kama kuna mtu atazi-prove wrong.
maelezo yako ni evidence nzuri tu. tatizo ninaloliona mimi ni itakuwaje wananchi wa upande wa Tz waliokuwa wanatumia ziwa hilo miaka na dahari kama hawataendelea kulitumia tena kwa sababu tu lipo Malawi? Hapo ndipo panataka ufumbuzi
 
Kama si kweli wamalawi wanamiliki ziwa lote, iwe kihalali au kimagumashi through helligoland treaty nk, ni kwanini mpaka leo hii hili swala halijawa resolved? mkae kimya kila siku, mama Tibaijuka anaenda UN kuhusu Indian ocean huku kimya. Tuliposikia wanatafuta mafuta tunataka vita. Nakumbuka Chiligati akiwa waziri wa ardhi alitangaza kutuma wataalam kwenda kuweka mpaka na malawi. Iliishia wp? hebu kwanza watupe status ya hii kitu aisee. how many yrs needed 2 resolve? vita tukampige nani? those are our brothers jamani, tu maskini lkn tunawaza mauaji na matumizi kirahisirahisi.
 
uzalendo sawa, lakini tujiulize zaidi kwa kuchambua hoja iliyoletwa na uhalisia.
 
Yanapokuja masuala ya nchi uzalendo ni muhimu haijalishi ni hoja gani.Hoja yako ya kuilaumu serkali eti inataka kutusahaulisha matatizo ya nchi nadhani haina mantiki.Cha msingi tuungane wote tujue mwisho wa hili ni nini.Na inawezekana unaongea hayo maneno vile wewe hauishi kyela...
Sio suala la kuishi Kyela tu, mtoa mada hii alitakiwa kujua ni nchi gani ilianzisha chokochoko juu ya mgogoro huu wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania. Kinachofanywa na serikali ya Tanzania sasahivi ni kukanusha madai yanayotolewa na Serikali ya Malawi kwamba ziwa Nyasa liko ndani ya Malawi kwa asilimia mia moja (100%) na sio kuusahaulisha umma kuhusu maswala muhimu yanayoendelea ndani ya Tanzania. Nadhani huyu jamaa alitaka kutuonyesha kwamba na yeye pia ashishawahi kukalia dawati; ma-"coordinate" meengi hoja ya msingi zero..! Ukimfuatilia kwa undani unaweza kukuta kumbe ni m-Malawi aliyekuja kutuliza njaa yake bongo.
 
Sio suala la kuishi Kyela tu, mtoa mada hii alitakiwa kujua ni nchi gani ilianzisha chokochoko juu ya mgogoro huu wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania. Kinachofanywa na serikali ya Tanzania sasahivi ni kukanusha madai yanayotolewa na Serikali ya Malawi kwamba ziwa Nyasa liko ndani ya Malawi kwa asilimia mia moja (100%) na sio kuusahaulisha umma kuhusu maswala muhimu yanayoendelea ndani ya Tanzania. Nadhani huyu jamaa alitaka kutuonyesha kwamba na yeye pia ashishawahi kukalia dawati; ma-"coordinate" meengi hoja ya msingi zero..! Ukimfuatilia kwa undani unaweza kukuta kumbe ni m-Malawi aliyekuja kutuliza njaa yake bongo.



Naungana mkono na wewe mkuu,huyu mtoa hoja anataka kutuchanganya na jografia yake aliyojifunza VETA,hapa ishu siyo mpaka wa tanzania na malawi kuwa nusu kwa nusu ishu ni umiliki wa 100% wa ziwa nyasa kwa wamalawi. Kama yeye anapoint aende akake na wamalawi wenzake watupe coordinates zetu katika ziwa nyasa kwa kufuata uelewa wao wala sisi hatuna shida!Na si kweli kwamba tanzania tunapenda vita ,lakini majibu ya wamalawi na viongozi yao ndiyo yanatufanya na sisi tuwe alerted. Lakini siku zote wamalawi wamekuwa watu wa ajabu so sishangai,mwanzoni walikuwa upande mmoja na makaburu kipendi cha apartheid,wameshakorofishana na Mozambique kuhusu mpaka wa lziwa nyasa na walikuwa pamoja na wareno kipindi mozambique wanatafuta uhuru,wamehalalisha ushoga na wanaoana kila siku so hili la kutaka kuichokonoa Tanzania wala si kitu cha ajabu kwa mwenyekuwajua hawa mashoga vizuri.
 
Lengo ni sisi tutatafakari sana suala la mppaka wa Malawikwa mapana yake. Maana tunaweza kuwa tunaburuzwa kijanja

Tuumbuke ugomvi wa miezi michache iliyopita wakati Tanzania ilipoomba kuongezewa eneo la maji. Kumbukeni Zanzibar walimlaani sana mwenzao Shamhuna na Jussa alimponda sana Tiabijuka.

Kama ni suala la kuongezewa basi kwa nini kuongezewa huku hakukutaja maji ya ziwa Malawi na badala yake kulitaja Indian Ocean pake yake. Kumbuka kwamba unapoongezewa ni kwamba ulikuwa na sehemu, lakini kama hukuwa na sehemu basi huna cha kuongezewa. Hivyo, hata Wizara ya ardhi ilijua wazi kuwa water zone tuliyo nayo ni ile ya east na west hatuna chetu.

Ukiangalia Lake Natron, mpaka wa Tanzania upo kwenye coordinate (S2.58670 E36.00408). One point of this lake iko Kenya kwenye coordinate (S2.10114 E36.03787). Ncha ya ndani kabisa iliyoko Tanzania iko kwenye (S2.58670 E36.00408).

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kutoka mpakani kwenda ng'ambo ya Kenya ni 1.5km yaani kama kutoka Ubungo kwenye mataa hadi Kituo cha Utawala cha University of D'Salaam. Wakati kutoka mpakani kuja ncha ya mwisho ya ziwa kwa upande wa TZ ni 52.5km yaani kama kuanzia Mbezi_Louis hadi Ruvu bridge.

Kwa maana hiyo kwenye Lake Natron mpaka wa Kenye na Tanzania hauko katikati bali ratio yake yaani Tanzania:Kenye ni 35:1. Nime-calculate eneo nikakuta hii Lake Natron ina 554sq.km Kenye inachukua 1.6 sq.km na sisi tunachukua 552.4 sq. kms. Kwa maana hiyo sisi tunachukua 99.711% ya hilo ziwa lote na Kenya wanachukua 0.289% ya ziwa hilo.

Tuje kwenye Lake Turkana ambalo liko north of Kenya. The most northen point of this lake is at {N4.65145 E36.16082} yaani 23.2km ndani ya Ethiopia. WHile the most southern point is at coordinate {N2.40027 E36.55652} yaani 232km ndani ya Kenya. Hivyo utaona distance toka mpakani kwenda kwenye furthest point Kenya ina advantage kwa Ethiopia by 10:1.

Wakti huohuo kwa hili Lake Turkana, the closest point from South Sudan border ni {N4.62853 E35.94680} ambayo ni 5km toka joint boundary ya South Sudan, Kenya na Ethiopia. Hivyo riparian advantage Sudan inaweza kupata kwa Lake Turkana. Riparian ni eneo lililo karibu na ziwa au mto ambalo effect ya maji inafika.

hata ukiangalia border yetu kwenye Lake Victoria, humo mpaka wetu na Kenye na Uganda uko kwenye coordinate {S0.99426 E33.92751}. The eastmost point ya Kenya toka hapo ni {S0.27608 E34.85068} yaani 130km ndani ya Kenya.

Jinja is the most north part of Victoria in Uganda na iko kwenye coordinate {N0.49723 E33.36409} na kutokea hapo hadi pale kwenye common border ni 159km.

Sisi Tanzania the southmost part kwenye Lake Victoria iko kwenye coordinate {S3.08704 E32.77124} na hapo panaitwa Mabale. Kwa maana hiyo kutoka hapo hadi kwenye ile common border ni 265km.

Kwa maana hiyo ukipanga ratio ya Tanzania: Uganda: Kenya in terms of distance from border inakuwa hivi: {2.04:1.22:1}. Hivyo, umbali wetu toka mpakani ni mara mbili ya wenzetu Kenya na Uganda ambao wanakaribiana!


Hivyo, ile hoja kwamba mpaka huwa ni katikati ya maji yaani ziwa au bahari si hoja ya kudanganya watoto tena watoto ambao hata hawasomi atlas au ramani yoyote ya dunia hii.

Si rahisi kuleta hoja hii wakati ukijua kwamba mimi nimetaja maziwa matatu tu lakini kuna maziwa na bahari nyingi tu tu zikoshared na huwezi kusema mpaka uko katikati ya hilo ziwa.

Mipaka yote iwe iliyopita ziwani al la kulikuwa na treaty fulani iliyoiweka. Huwa tunasema sana Berlin Conference kuwa ndiyo iliyoweka mipaka huku Africa. Lakini tunaofuatilia history tunajua kwamba hata mipaka mingi ya Ulaya iliwekwa miaka 16 kabla ya hii Berlin Conference. Mipaka ya Ulaya iliwekwa kwenye Vienna Congress of 1815.

Hivyo tangu wakati huo kama hakuna updated ratification ya mipaka basi mipaka ilibaki hivyohivyo. Concept inabaki kwamba kama ukatikati ungekuwa ni hoja basi mifano niliyotoa ingekuwa yaani Natron, Trukana na Victoria ingefanya kazi.

Zaidi tukijikita na hoja hiyo, basi majirani zetu wawe na wasiwasi precedence ya Malawi, kwamba ukina mwenzi ananyolewa basi wewe tia maji.

Sikubaliani kabisa na ujanja huu wa kujifanya tunadai sana Lake Malawi hadi tusahau mambo ya msingi kumbe inaweza kuwa ni janja ya serikali tujione tuko wamoja wakijua suala hili litachukua muda mrefu na Tanzania hatuna haki hata chembe ya Lake Malawi halafu tusahau kabisa masuala ya Ulimboka, migomo ya walimu, madaktari, NSSF na maisha magumu kwa kila mtanzania.

Namalizia tena, si lazima mpaka wa ziwani uwe katikati ya maji kama tunavyoaminishwa. TUna akili na sisi tunasoma.

Mkuu Nikupataje,

Argument yako hapa ina walakini kwasababu premise uliyotumia kujenga hoja yako ni false.

Lazima utofautishe kati ya mpaka kuwa katikati ya ziwa na kugawana ziwa katikati. Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa.

Katika hoja yako umetumia muda wote kuonyesha inawezekana sehemu kubwa ya ziwa ikawa nchi moja na nchi nyingine ikawa na eneo dogo la ziwa. Kwa mgogoro huu hilo sio issue kabisa maana hata kwa kufuata madai ya TZ, bado ziwa Nyasa eneo kubwa litakuwa upande wa Malawi ukilinganisha na TZ na Msumbiji.

Tunachosema TZ ni kwamba pale ambapo ziwa linapita katikati ya nchi mbili, mpaka unakuwa katikati ya ziwa. Kwa mfano kaskazini mwa ziwa Nyasa, upande wa magharibi, eneo la TZ kwenye ziwa halizidi urefu wa km 60 upande wa TZ kutokea mto Songwe mpaka ncha ya mwisho ya ziwa kaskazini. Wakati kutoka mto songwe mpaka nchi ya mwisho kusini ya ziwa ni karibu km 800.

Kwa upande wa mashariki, kutoka mpakani hadi ncha ya kaskazini ni karibu km 300 na kwenda kusini karibu km 500 ambazo ziko upande wa Msumbiji.

Kwa kifupi ni kwamba ukianzia kaskazini, km 45 ziwa lote ni la TZ. Kuanzia km 45 kwenda kusini mpaka km kama 300 ziwa linagawiwa katikati kati ya TZ na Malawi. Kuanzia km 300 kwenda mpaka ncha ya mwisho kusini ziwa linagawiwa katikati kati ya Malawi na Msumbiji.

Tanzania itamiliki sehemu ndogo ya ziwa, ikifuatiwa na Msumbiji na Malawi inabaki na sehemu kubwa. Mpaka wa ziwa lazima uendane na mipaka ya nchi kavu. Ukisema ziwa lote liende upande mmoja bila kujali watu ambao wanaishi hayo maeneo, mbona dunia yote ingelikuwa ni ugomvi kila siku?

Mfano wako wa ziwa Natron uko wrong kwasababu sehemu ambayo inaongelewa mpaka kupita katikati ni ile tu sehemu ndogo ya juu ambayo inatenganisha TZ na kenya. Unanyosha mpaka wa nchi kavu kutoka upande mmoja wa ziwa kwenda mwingine.

Hapa kwenye Technology tunaita gabage in gabage out. Umetumia premise ambayo ina makosa katika kujenga hoja yako na kujikuta unapata conclusion ambayo ina makosa.
 
Lengo la Tanzania halitakiwi kuwa kutafuta uhalali wa mpaka ulipo. Kuna watanzania zaidi ya 600000 ambao maisha yao yanategemea ziwa Nyassa. Kwa hiyo tushajua kuwa mpaka unapita katikati, kitendo cha maisha ya watanzania kutegemea ziwa hilo ni sababu tosha ya mpaka kupita katikati, hatuhitaji sababu nyingine. Changamoto pekee ambayo tunatakiwa kuijadili ni jinsi ya kuwafanya wamalawi wakubaliane na hilo kidiplomasia. Hata hivyo ni lazima tuambiane ukweli kuwa options zote ziko mezani, hakuna option inayoachwa, lengo ni kuhakikisha watanzania wanaendelea na maisha yao kama jinsi walivyoishi enzi na enzi.
Kuingiza vilogic logic vya ajabu ajabu vinavyojustify ziwa lote lichukuliwe na malawi (herufi ndogo not a typo) ni kuwasaliti watanzania wanaoishi kwa kutegemea ziwa Nyassa.
 
Hapa suala ni kupata ukweli kupitia njia huru, huwezi ukasema ziwa ni la Malawi halafu ukategemea waTanzania watakaa kimya,
Hakujawahi kuwa na suluhisho la mpaka huu kwa kipindi chote
Hata ukiangalia ramani ya Nyasaland ya mwaka 1935, utaona kuwa mpaka ni katikati ya ziwa, sasa ni kwa nini sasa wamebadili au kwa nini watumie mkataba wa 1897 na si hiyo ramani inayoonesha mipaka kwa kipindi hicho
Hivyo, ni vyema kutatua tatizo sasa kwa jinsi yeyote, tukianzia diplomasia na baadae vita kama alivyosema Lowassa
 
nngu,

kama tumeamua kuondokana na tatizo la lake malawi basi toeni hoja ili tujue kinachotupeleka huko ni nini. Mimi ninavutwa na hoja kwamba lile ziwa si letu hata kwa sababu hizi ndogo nilizoeleza humu na kwenye thread zingine.

Lakini kichekesho kiko kwenu mnaotetea kuwa ziwa lile ni letu. Kichekesho ni jinsi ambavyo hata wenyewe mnaona wazi mlivyoparaganyika bila kuwa na hoja moja thabiti na mnajikuta mnatamka neno uzalendo lakini mkiulizwa kidogo tu kila mtu anajibu kwake.

Ona kama wewe unavyojibu. Unasema hayo maziwa niliyotaja yanatumika na nchi jirani. Mimi sijajenga hoja ynagu kwa msingi huo na hakika hukua na sababu za kuleta hilo wazo lako kama umesoma thread yangu vizuri.

Mimi nimesema kuwa kuna percentage kidogo kwenye zone za hizo lake hata kama ni 0.2%. Nimetoa mfano lake turkana ambako south sudan haiwezi kuleta ubishi kama mnaoleta kwamba na yenyewe ifaidike kwenye ziwa hilo kwa sababu tu iko kilometa tano toka lake natron.

Hoja yangu inabaki palepale kwamba concept ya mpaka kuwa katikati ya maji au wengine mnavyoitw nusu kwa nusu ni uongo.

Kama kuna anayesema ni ukweli basi aniumbue.

wewe sio mtanzania---wewe ni mercenary au puppet flani hivi...hoja yako ni kuwa tanzania tusitumie ziwa au ni nini...sasa kwa nini tulijenga banadari na tunavua for years dagaa watamu n.k up to the median line since time immemorial and all of a sudden jamaa wanasema the entire lake is theirs....ni ujirani gani mwema kiasi hiki wa muda wote huo? Go back to your country.... We are a free state not colonial any more
 
Back
Top Bottom