Si lazima mpaka wa nchi uwe katikati ya ziwa. Tutumie usomi wetu Tusimame kwenye ukweli

Nikupateje, Malawi walipopata uhuru walisema nchi mipaka ya nchi yao iko wapi? Au kwenye ulingo wa kimataifa Malawi wanaelezea eneo la nchi yao kivipi?

Jambo moja ambalo nina hakika nalo, rais wa sasa wa Malawi ni kibaraka mzuri sana wa wazungu and trade her family silver ili kuwaridhisha wazungu. Tangu ameingia madarakani anaonekana kufanya maamuzi ya haraka sana yenye msukumo wa wazungu. Hili la Lake Nyasa nalo amepata kiburi toka kwa waingereza.

Uzuri ni kwamba Malawi hawajawahi kugeuka kauli zao kabla na baada ya uhuru. Unachokisikia wakikisema sasa ndicho kilisemwa miaka yote.

Hayo ya kwamba wakoje na wazungu mimi siwaingilii kwani wana uhuru wa kuhusian na yeyote wanayeona ana manufaa kwao kama sisi tusivyoingiliwa na tunaoona wana manufaa kwetu.
 
Uzuri ni kwamba Malawi
hawajawahi kugeuka kauli zao kabla na baada ya uhuru. Unachokisikia
wakikisema sasa ndicho kilisemwa miaka yote.

Hayo ya kwamba wakoje na wazungu mimi siwaingilii kwani wana uhuru wa
kuhusian na yeyote wanayeona ana manufaa kwao kama sisi tusivyoingiliwa
na tunaoona wana manufaa kwetu.

malawi wako composed kwenye hili. sisi ndo hatujatulia. tunapayuka badala ya kujenga hoja.
 
Angaria hiyo Map then tuambie usomi wako unaonyesha mpaka uko wapi??


Lake Nyasa.jpg
Lengo ni sisi tutatafakari sana suala la mppaka wa Malawikwa mapana yake. Maana tunaweza kuwa tunaburuzwa kijanja

Tuumbuke ugomvi wa miezi michache iliyopita wakati Tanzania ilipoomba kuongezewa eneo la maji. Kumbukeni Zanzibar walimlaani sana mwenzao Shamhuna na Jussa alimponda sana Tiabijuka.

Kama ni suala la kuongezewa basi kwa nini kuongezewa huku hakukutaja maji ya ziwa Malawi na badala yake kulitaja Indian Ocean pake yake. Kumbuka kwamba unapoongezewa ni kwamba ulikuwa na sehemu, lakini kama hukuwa na sehemu basi huna cha kuongezewa. Hivyo, hata Wizara ya ardhi ilijua wazi kuwa water zone tuliyo nayo ni ile ya east na west hatuna chetu.

Ukiangalia Lake Natron, mpaka wa Tanzania upo kwenye coordinate (S2.58670 E36.00408). One point of this lake iko Kenya kwenye coordinate (S2.10114 E36.03787). Ncha ya ndani kabisa iliyoko Tanzania iko kwenye (S2.58670 E36.00408).

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba kutoka mpakani kwenda ng'ambo ya Kenya ni 1.5km yaani kama kutoka Ubungo kwenye mataa hadi Kituo cha Utawala cha University of D'Salaam. Wakati kutoka mpakani kuja ncha ya mwisho ya ziwa kwa upande wa TZ ni 52.5km yaani kama kuanzia Mbezi_Louis hadi Ruvu bridge.

Kwa maana hiyo kwenye Lake Natron mpaka wa Kenye na Tanzania hauko katikati bali ratio yake yaani Tanzania:Kenye ni 35:1. Nime-calculate eneo nikakuta hii Lake Natron ina 554sq.km Kenye inachukua 1.6 sq.km na sisi tunachukua 552.4 sq. kms. Kwa maana hiyo sisi tunachukua 99.711% ya hilo ziwa lote na Kenya wanachukua 0.289% ya ziwa hilo.

Tuje kwenye Lake Turkana ambalo liko north of Kenya. The most northen point of this lake is at {N4.65145 E36.16082} yaani 23.2km ndani ya Ethiopia. WHile the most southern point is at coordinate {N2.40027 E36.55652} yaani 232km ndani ya Kenya. Hivyo utaona distance toka mpakani kwenda kwenye furthest point Kenya ina advantage kwa Ethiopia by 10:1.

Wakti huohuo kwa hili Lake Turkana, the closest point from South Sudan border ni {N4.62853 E35.94680} ambayo ni 5km toka joint boundary ya South Sudan, Kenya na Ethiopia. Hivyo riparian advantage Sudan inaweza kupata kwa Lake Turkana. Riparian ni eneo lililo karibu na ziwa au mto ambalo effect ya maji inafika.

hata ukiangalia border yetu kwenye Lake Victoria, humo mpaka wetu na Kenye na Uganda uko kwenye coordinate {S0.99426 E33.92751}. The eastmost point ya Kenya toka hapo ni {S0.27608 E34.85068} yaani 130km ndani ya Kenya.

Jinja is the most north part of Victoria in Uganda na iko kwenye coordinate {N0.49723 E33.36409} na kutokea hapo hadi pale kwenye common border ni 159km.

Sisi Tanzania the southmost part kwenye Lake Victoria iko kwenye coordinate {S3.08704 E32.77124} na hapo panaitwa Mabale. Kwa maana hiyo kutoka hapo hadi kwenye ile common border ni 265km.

Kwa maana hiyo ukipanga ratio ya Tanzania: Uganda: Kenya in terms of distance from border inakuwa hivi: {2.04:1.22:1}. Hivyo, umbali wetu toka mpakani ni mara mbili ya wenzetu Kenya na Uganda ambao wanakaribiana!


Hivyo, ile hoja kwamba mpaka huwa ni katikati ya maji yaani ziwa au bahari si hoja ya kudanganya watoto tena watoto ambao hata hawasomi atlas au ramani yoyote ya dunia hii.

Si rahisi kuleta hoja hii wakati ukijua kwamba mimi nimetaja maziwa matatu tu lakini kuna maziwa na bahari nyingi tu tu zikoshared na huwezi kusema mpaka uko katikati ya hilo ziwa.

Mipaka yote iwe iliyopita ziwani al la kulikuwa na treaty fulani iliyoiweka. Huwa tunasema sana Berlin Conference kuwa ndiyo iliyoweka mipaka huku Africa. Lakini tunaofuatilia history tunajua kwamba hata mipaka mingi ya Ulaya iliwekwa miaka 16 kabla ya hii Berlin Conference. Mipaka ya Ulaya iliwekwa kwenye Vienna Congress of 1815.

Hivyo tangu wakati huo kama hakuna updated ratification ya mipaka basi mipaka ilibaki hivyohivyo. Concept inabaki kwamba kama ukatikati ungekuwa ni hoja basi mifano niliyotoa ingekuwa yaani Natron, Trukana na Victoria ingefanya kazi.

Zaidi tukijikita na hoja hiyo, basi majirani zetu wawe na wasiwasi precedence ya Malawi, kwamba ukina mwenzi ananyolewa basi wewe tia maji.

Sikubaliani kabisa na ujanja huu wa kujifanya tunadai sana Lake Malawi hadi tusahau mambo ya msingi kumbe inaweza kuwa ni janja ya serikali tujione tuko wamoja wakijua suala hili litachukua muda mrefu na Tanzania hatuna haki hata chembe ya Lake Malawi halafu tusahau kabisa masuala ya Ulimboka, migomo ya walimu, madaktari, NSSF na maisha magumu kwa kila mtanzania.

Namalizia tena, si lazima mpaka wa ziwani uwe katikati ya maji kama tunavyoaminishwa. TUna akili na sisi tunasoma.

UPDATE AS AT AUG 08, 2012 AT 14:26:

NImesoma post zote nikidhani kuna hoja inifanye niungane na wanaotofautiana na mimi. Nimeachana na hoja za humu nikanunua RAIA MWEMA ili nisome hotuba ya bernard Membe aliyotoa bungeni kuhusu hili suala la Malawi.

Wakati nanunua gazeti nilitumaini kabisa Membe atakuwa na hoja ya ku-convice kwani humu JF mnaongea tu kama mimi. Kwa wale waliosoma RAIA MWEMA wafungua attached paper kwenye ukurasa wa iv. Ndipo anaeleza msimamo wa Serikali kuhusu mpaka wa Ziwa Malawi.

Nakiri kwamba hata wakati naleta thread hii, nilitumaini Bernard Membe atakuwa ameongelea findings ambazo zingetushawishi na mimi nisingesita kuungana kwenye nia ya kukidhi madai haya ya Lake Malawi.

Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.

Siku moja nilifanya hesabu ubaoni nikapata jibu na baadaye nikaongeza madoido mwalimu akanikata maksi akasema "Kujitawaza kwingi mwisho unashika kinyesi". Naona ndugu yetu Waziri Membe kaingia katika mtego huu. Kwa nini nasema hivi? Ninanukuu majibu yake kama ifuatavyo:


****
Mheshimiwa Spika,
Lipo tatizo la muda mrefu kati yetu na nchi jirani ya Malawi linalohusiana na mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Tatizo lenyewe ni kwamba Malawi wanadai kwamba ziwa lote kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa mwaka 1890.

Mheshimiwa Spika,
Tanzania kwa upande wetu tunasema kuw ampaka wa kweli kati yetu na malawi unapita katikati ya ziwa hivyo kufanya
eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati Latitude digrii 9 na digrii 11 kuwa mali ya Tanzania kwa mujibu wa mkata huouo wa Heligoland wa mwaka 1890 ambao ulikubali kuwa kwa vile kuna maeneo ya mpaka ambayo hayana mantiki, pande zinazohusiana zikutane na kurekebisha. Aidha tunazo ramani ambazo waingereza wenyewe walipitisha mpaka katikati kama ulivyo mpaka kati ya Msumbiji na Malawi.
****

Nimemalizia hapa kwa sababu mengine yanayofuata ni diplomatic process. Sasa hapa tuchambue hotuba hii ya Membe. Binafsi nimeusoma mkataba wote wa Heligoland na wala si alichokisema Membe. Kama membe anataka kuikomboa Tanzania walau tupate sehemu ya Ziwa basi washauri wake wamempotosha kutumia mkataba ule ambao hautetei hoja yake hata kidogo.

Lakini pia Membe ni mmoja wa wanaodhani watanzania wa sasa hawajui kufukua mambo na ndiyo maana kwenye thread yangu nimesema tutumie usomi wetu. Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.

Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}.

Ukiangalia coordinate hizi maana yake ni kwamba Ziwa Malawi linaishia kwenye Latitude 9.49214. Sasa hapa Membe anasema eti ni kuanzia Latitude 9. Kwa maana hii ya Membe kama Ziwa ni letu kuanzia latitude 9 maana yake ni kwambaMmembe kafanya makosa kwa kulirefusha ziwa hili kwa umbali wa 54.4km kuelekea kaskazini!

Watu mnaotoka kusini hasa Mbeya mnafahamu sehemu iitwayo Matamba. Hapa coordinate zake ni { S9.01171 E34.09959}. Kwa mujibu wa Membe, hii Matamba ingekuwa imeguswa na Ziwa hili!

Hakika waliomletea Membe hizi data wamemvuruga kuliko kulietengeneza suala hili. Ziwa Malawi au Nyasa linaishia kwenye Latitude 9.49214 kama nilivyosema hapo juu. Hapa membe kadanganya Bunge na kadanganya watanzania kasi kwamba sijui sasa ni nani mwenye nguvu ya kulitetea hili.

Tuje sasa kwa upade wa kusini yaani unaotambuliwa na membe kama sehemu yaetu ya Ziwa. Membe anasema sisi mali yetu ni mpaka kwenye latitude 11. Sijui wangapi mmeona kosa hili la mwaka. Unaposema kwamba unaishia hapa kwenye Latitude 11, je mnaotetea hoja hii mnaelewa madhara yake? Kama hamyajui basi mimi nayasema hapa.

Kama Membe kasema Bungeni kwamba tunaishia kwenye Latitude 11 basi maana yake pale ni kaskazini ya sehemu iitwayo Liuli ambayo iko { S11.05023 E34.63908}. Kumbe, Mwanakijiji wa Liuli haruhusiwi kuvua samaki kwenye ziwa lile kwa sababu ni sehemu ya Malawi, kwa mujibu wa Waziri Bernard Membe!

Yaani mwanakijiji huyu wa Liuli, anakuwa amekiuka mpaka kwa kilomita 6.6 kwa mujibu wa Serikali anayoshiriki membe wala si kwa mujibu wa Serikali ya Malawi!

Nimeanza na mfano huo wa Liuli ambao najua wengine hampaju ahapo. Sasa tuje kwenye mfano ambao wengi mnaujua na mmeutumia kunipinga humu na kuniita mimi ni mmalawi.

Mfano wenyewe ni wa Mbamba Bay. Ndiyo maana nimesema kajipangeni hii kesi tutajikuta tunasambaratika tukidhani tunatetea huku tunajiangamiza. Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.

Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Mbamba Bay haiko katika eneo linalotambuliwa na Waziri Membe kwa latitude degree 0.30519!

Uki-convert hizi latitude kwenda kwenye kilomita basi maana yake Membe haitambui Mbamba Bay kwani iko 33.7km nje ya eneo ambalo Tanzania tunamiliki ziwa!

Waziri membe pia inaelekea kuwa hajui mpaka unavyopita pale Msumbiji. yeye anasema kule ni nunu kwa nusu lakini wote fungueni ramani muone kama hilo nalo lina ukweli. Mpaka wa Msumbiji ni nusu kwa nusu kuanzia kwenye latitude 11 had 13 lakini kuanzia hapo keuelea kule chini kusini ziwa lote liko sehemu ya Malawi na linaishia kwenye coordinate {S14.44635 E35.23539} ambako ni latitude 14.44635.

Ndiyo maana tangu mwanzo nimesema, tujenge hoja zinazojikita kwenye ukweli na tusishabikie mambo kama vile Simba na Yanga. Hapa hatufanyi ushabiki. Hapa tunasaidia kujenga na kupima hoja kama kweli tunaweza kuisaidia nchi yetu kupata sehemu ya ziwa hili.

Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
 
Wabongo akili zetu fupi sana ndio maana tunadhani america ni kwetu. na usomi wako hufai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi. hujiulizi kwa nini waligawana africa na wakatuacha tumegawanyika mpaka leo. kama wewe mchambuzi ungetoa two options kuungana kuwa nchi moja au zipigwe nchi ikishindwa basi iwe mkoa. msaliti mkubwa wewe hufai kukaaa hapa kwetu. unajua kilicho nyuma ya pazia wewe.
 
Hoja napa wamalawi Wanataka Eneo tu la ziwa mkiweza kukatisha maji kwa ndio safi watachimba Gesi kwa furaha. Note that.
basi jamaa hawajui kusoma alama za nyakati, kama wanapita humu nawashauri wakaangalie documentary ya blue gold world water wars
 
Back
Top Bottom