Shutuma nzito dhidi ya waigizaji wa bongo movie

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Tunapenda kupeleka shutuma hii kwa waigizaji wa bongo movie hasa episode za ndoa/mahusiano/mapenzi. Waigizaji hawa wamekuwa wakiingiza ubaya, ubabe, ufedhuli, kiburi, umalaya, wizi, utapeli, ushirikina, mauaji, matumizi ya dawa za kulevya, ndani ya mapenzi kitendo ambacho kimekuwa kikifundisha watazamaji ambao ni wake na waume za watu tabia chafu katika mahusiano na kupelekea baadhi yao kuiga tabia hizo kwenye mahusiano yao ama ndoa zao.

Mfano: Episode inamuonesha dada kaolewa na anamuheshimu mume wake, anakuja dada mwingine anamwambia usiheshimu wanaume hawana shukrani hawa sio ndugu zetu, twende tukajiuze.

Madhara yake ni kuwa, watazamaji wa kike walioko kwenye mahusiano huku wakiheshimu waume zao wanapotazama maudhui hayo wanaanza kujifunza ubaya na kupelekea ndoa zao kuvunjika.

Bongo Movie inatakiwa kufundisha mambo mema katika jamii na sio ubaya, ikiwa itaendelea kusambaza maudhui haya basi tutegemee kuona ndoa na mahusiano ya watu wengi yakivunjika kila kukicha na ubaya ndani ya jamii
 
kwan maisha haya si unatakiwa uwe na akili zako kichwani Vya kuona uone vya kusikia usikie na kujua nn ufanye na kipi usifanye
 
Back
Top Bottom