pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 691
- 878
"Tupo hapa kwaajili ya kumpongeza Mwanamke shupavu mwenye Utanzania na Uzalendo Samia Suluhu Hassan. Watu walikuwa wanasema Mlima Kilimanjaro haupo Tanzania, Kutokana na Royal Tour sasa hivi Watu wamejua Mlima Kilimanjaro upo Tanzania". Amesema Nangasu
Amesema ile ni filamu maalum ya kutanganza Nchi, Tamaduni na Mira zake. Sio bongo Movie. Tutegemee Wageni wengi sana. Tumpongeze na tumuunge Mkono Rais Samia. Tanzania ni miongoni mwa nchi Tisa zianzon tangaza royal tour. Nyingine baadhi ni New Zealand, Israeli, Jordan, Peru, Mexico, Rwanda, Poland nk
Wakati wa kuitangaza Royal Tour, Rais Samia alikutana na benki ya dunia baada ya muda yatazaa matunda. Wameahidi kuisaidia Tanzania.
Royal tour imeleta Ushawishi kwa vijana. Wanaongeza Ubunifu katika bidhaa zao ili kuvutia Wageni
"Tanzania hakuna mkoa usio na Utalii. Kila mkoa una kivutio. Hata amani ya Tanzania ni Utalii. Nchi nyingine Watu wanaamshwa na Mabomu ila sisi Asubuhi tunaamshwa na Mkojo" Amesema Nangasu.
Mama kaimarisha Uhusiano wa Kimataifa. Alikutana na Makamu wa Rais wa Marekani. Meya wa New York alisema ataitangaza Vizuri Tanzania, ndege zitaanza kutoka Marekani hadi Tanzania moja kwa Moja.
Sasa hivi Royal Tour inaoneshwa kwenye Channel 350 dunia kwa kupitia amazoni
Nampongeza mama mbunifu Rais Samia
Amesema Wanawake laki moja wana mkakati wa kuzunguka nchi nzima kutembelea Vivutio vya Utalii na Kuvitangaza. Kila Mtanzania Mwanamke ulipo Tumuunge Mkono Rais Samia afanye makubwa zaidi.
=====
KAMPENI YA ROYAL TOUR
Bila kumumung’unya maneno, Royal Tour ni ubunifu na jitihada kubwa za kutangaza fursa za Italie na uwekezaji nchini ambazo hazijawahi kutokea tangu tupate uhuru takribani miaka 60 iliyopita.
Sote tunafahamu namna ambavyo nchi jirani zimekuwa zikitumia mabilioni ya pesa kutangaza utalii wao duniani huku Tanzania ikiachwa nyuma hadi kupelekea baadhi ya watu huko nje kulaghaiwa kuwa Mlima Kilimanjaro na hata Serengeti ziko nchi jirani na siyo Tanzania.
Lakini kwa kupitia ushiriki wake kwenye Royal Tour, Rais Samia amewezesha kuitangaza Tanzania kimataifa na kupeperusha bendera ya nchi.
Ni vyema kusisitiza kuwa Royal Tour siyo movie kama zile zinazotengenezwa Hollywood au Bollywood au Nollywood au Bongo movie. Royal Tour ni makala malumu inayotoa fursa ya kipekee na mahsusi ya kuitangaza Tanzania ulimwenguni kama kitovu cha utalii na uwekezaji duniani.
Wakati watu wengine wanakaa ofisini kwenye viyoyozi, Rais Samia alifanya kazi ngumu kuongoza kurekodiwa kwa documentary hii porini na hata kushinda bila kula wakati mwingine kuhakikisha kuwa nchi yake aipendayo sana ya Tanzania inatangazwa ulimwenguni.
Kama alivyosema Rais Samia mwenyewe, gharama ya kurekodi fiamu ya Royal Tour na kuitangaza duniani zimelipiwa na michango kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali nje na néant ya sekta ya utalii nchini.
Nikiwa kama mdau wa utalii, natoa pongezi za dhati kwa jitihada binais za Rais Samia na mchango mkubwa wa wafanyabiashara na taasisi mbalimbali nchini zilizofanikisha Royal Tour na kuipaisha Tanzania kimataifa duniani.
Ni makala maalum inayohusisha Wakuu wa Nchi waliopo madarakani ili kuzieleza nchi zao na kuzitangaza kimataifa katika sekta mbalimbali.
Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa hive karibuni na Bi. Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Tanzania ni miongoni m’a nchi ya 9 kushiriki programu hii ya Royal Tour ambayo pia humpa nafasi kiongozi husika kuzindua makala hayo nchini Marekani, kupata nafasi ya mahojiano na vyombo vikubwa vya habari na kukutana na wadau mbalimbali wa biashara, utalii na uwekezaji ana kwa ana ili kuwavutia kuja nchini kuwekeza.
Nchi nyingine zilizoshiriki kampeni ya Royal Tour ni Jordan, New Zealand, Poland, Mexico, Ecuador, Peru, Israel, Rwanda na sasa Tanzania.
Sababu nyingine ya kutumia Marais walio madarakani kwenye programu hiyo ni kujenga imani kwa watazamaji, yaani watalii na wawekezaji.
Tayari filamu hii imefanikiwa kuitangaza Tanzania kimataifa na itaendelea kufanya hivyo kwa miaka mingi ijayo kwani imewekwa pia inapatikana katika mitandao mikubwa duniani kama Amazon na Apple TV na itaoneshwa katika channeli 350 nchini Marekani zinazowafikia Wamarekani zaidi ya milioni 200.
Katika siku zijazo, Tanzania linatarajia kupokea wawekezaji na watalii wendi katakana na jina la nchi yetu sasa kuwa gumzo duniani kupitia ushiriki wa Rais Samia kenye makala mazlumu ya Royal Tour.
Kama tulivyosema awali, lengo la taarifa yetu hii ni kumpongeza Rais Samia kwa uongozi wake wa kishujaa, kumtia moyo aendelee na jitihada zake na kumhakikishia kawa sisi Watanzania tuko pamoja naye bega kwa bega kukabiliana na changamoto za maendeleo chini.