SoC02 Shule za kata mkombozi wa wengi, changamoto na maboresho yake

Stories of Change - 2022 Competition

Ifakara Brand

New Member
Sep 2, 2022
1
1
Na Amour A. Mawalanga
Ilikua ni mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu ndipo sera ya uanzishwaji wake ilipoanza chini ya mzee wa Msoga Rais wa awamu ya nne Jakaya M. Kikwete huku mtendaji wake mkuu wa serikali akiwa Edward N. Lowasa.

Mwaka 2006 ndipo utekelezaji ukaanza ambapo kila kata ilitakiwa iwe na sekondari yake kulingana na shule ya msingi zilizo katika kata hiyo.Nguvu ya wananchi ilitakiwa ambapo walitakiwa kusimamisha boma halafu serikali iliwajibika kufanya umaliziaji wa majengo hayo na kuleta vitendea kazi pamoja na walimu.

Watu walibeza sana ikiwemo wanasiasa ambao walisema sasa serikali imekuja kuua ubora wa elimu.

Masomo yakaanza,changamoto zikawa nyingi sana,uchache wa walimu,uchache wa vitendea kazi,uchache wa vitabu,miundombinu mibovu kama madarasa na kukosa vyoo,kukosekana kwa alama muhimu za shule kama nembo,sare na wimbo wa shule,mazingira hatarishi ya kusomea kwa shule za vijijini zilizojengwa maporini na kukosekana kwa imani za wananchi juu ya shule hizo

Picha likaendelea kuanzia mwaka 2009 shule za kata zikaanza kutoa mazao yao,hali ikawa mbaya sana sokoni, kati ya wanafunzi 200 zero zilikua kasoro wanafunzi 3.
Waliozipinga wakapata nguvu wakazipa na majina mengi sana, kuna walioziita st. Kayumba,mapenzi day, zero sekondari, shule za kajamba nani, kufeli lazima na majjina mengi yenye kuharibu dhana ya uwepo wake.

Waliozikosoa hawakuja na mikakati mbadala na kushauri nini kifanyike zaidi ya kufurahia tu.

WAKAONA KWA VILE NI ZA MASIKINI WAACHE WAFELI TU.
Loh! masikini,wanafunzi waliokua wameenda kusoma shule za kulipia wengi wao wakajivika ufahari hata wakirudi likizo waliwatenga wenzao.Ikafikia wakati ukiongea nae atakupa msamiati wa kiingereza na kukuongelesha kingereza cha ndani sana kukukomesha.Ikawa uktembea nae watu watamwita yeye tu huku akisifiwa kwamba amekonda na msomi lazima akonde hii ikiwa dongo kwa wewe wa shule za kata kwamba hakuna unachosoma zaidi ya kustarehe tu ndio maan hata mwili haupungui.Hakika matabaka yakawa ya wazi kabisa.

Miaka ikaenda kuna baadhi ya wanafunzi wakafaulu kwa uwezo wa mungu na jitihada zisizo na matumaini ndipo walimu,wazazi na wanafunzi wakaanza kuamka na kusema kumbe kufaulu inawezekana.

Ufaulu ukaongezeka wanafunzi wa shule za kata wakachachamaa wakaanza kufanya vitu, mazingira magumu, changamoto nyingi lakini kwenye matokeo ya kidato cha nne nao wakachomoza na kupata ufaulu wa kwenda elimu ya juu,ualimu,upolisi,jeshini,unesi na fani mbalimbali zenye tija.

Dharau zikazidi kupungua pale ambapo wanafunzi wa shule za kata walipopata maksi za juu kuliko wale wa shule za kulipia ndipo heshima ikazidi sogea.Unajua ili ufanikiwe jambo fulani muda mwingine lazima uone mtu miongoni mwenu alietangulia amefanikiwa,anakupa hamasa na anakua somo zuri kwako na hiki ndicho kilichotokea kwa wanafunzi wa mwanzo kufaulu kutokea shule za kata dhidi ya wenzao.

wanafunzi wa shule za kulipia hawakua na makosa,ilikua si rahisi kuwathamini na kuwaamini watu wanaosoma kwenye mazingira yenye changamoto lukuki.
Leo hii shule za kata zimetoa madaktari, wafamasia, mainjinia, walimu, maafisa boashara, wauguzi, watalamu wa maabara,maaskari,wanajeshi wenye vyeo na viongozi wengi tu wa kisiasa ambao wengi wao walitoka kwenye familia dhaifu.

Angalau sasa kila anaezidharau shule za kata hasemei hadharani tena anaenda chumbani na mke wake na kunong'ona kwamba hizi shule hamna kitu.Kuna baadhi ya wazazi wana uwezo lakini kwasasa imekua kawaida tu kumpeleka mtoto wake shule za kata za serikali huku wakisema elimu ni ileile tu.
HAKIKA MAPINDUZI SIO KITU RAHISI.

Shule za kata zimeleta tija kubwa sana kwa taifa la Tanzania tangu kuanzishwa kwake mpaka leo

-Zimepunguza idadi ya ndoa na mimba za utotoni.

-Zimefuta ujinga kwa vijana wengi wa kitanzania na kujua dunia inaendaje na inataka nini.

-Imesaidia kutokomeza mila na desturi zenye kukandamiza jinsia fulani kama ukeketaji na nyinginezo.

-Zikatengeneza ajira za uhakika kwa walimu.

-Zikawapa nafasi wanafunzi waliopata maksi ndogo kwa sabababu mbalimbali kuendelea na masomo ambao wengine waliamka huko mbeleni.

-Imepunguza vijana wa mitaani ambao wengi wao walipokua wakifeli darasa la saba waliingia kwenye magenge ya uhalifu.

-Elimu ikasaidia vijana wa kitanzania kupima na kutathimini mfumo upi wa siasa unaofaa.

-Elimu ikasaidia vijana kujikinga na magonja ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa
HAKIKA ZIKASAIDIA KUPIGA VITA MAADUI WATATU WA UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI. Unajua ujinga ndio adui mkubwa zaidi, ujinga unaleta umasikini na unaleta maradhi, fikiria mtu anaweza kufanya kazi ngumu ila akipata ela anaenda kununua penzi kwa kahaba na anaweza kufanya ngono isiyo salama. Hapo ujinga umemletea mtu umasikini na pengine maradhi pia.

Pamoja na safari hiyo na mafanikio yake shule za kata zimekua na changamoto nyingi sana

-uchache wa walimu hasa kwa msomo ya hesabu na sayansi.

Serikali ina wajibu wa kuhakikisha inaajiri walimu wa kutosha kukabiliana na changamoto hii, suala la walimu ni suala nyeti, halihitaji siasa.

-Kukosekana kwa mabweni jambo linaloathiri maendeleo ya wanafunzi sio wakike wala wa kiume.

- Kukosekana au upungufu wa maabara zinazokidhi mahitaji.

- Upungufu wa vitabu na maktaba zenye tija.

- Ushirikiano mdogo wa wazazi kwa walimu kuhusu ufatiliaji wa nidham na taaluma za wanafunzi.

- Tatizo la kutowajibika ipasavyo(kukosa wito) kwa baadhi ya walimu ambao wengi wao hufikia hata kusema wanafunzi wafaulu au wafeli wao mshahara unaingia.

- Bodi za shule nyingi ni dhaifu,hukutana mara chache lakini pia zina mikakati ya maneno kuliko vitendo,bodi zingine huteuliwa pasipo kuangalia uwezo wa wateuliwa isipokua hadhi ya mtu katika eneo husika.

- Kukosa ushirikiano wa utatuaji wa kero zao kwa viongozi wa halmashauri zao. Halmashauri nyingi zimekua haziwajibiki ipasavyo.

- Ufinyu wa bajeti kwa uongozi wa shule kumudu gharama za uendeshaji wa shule hizo.
Changamoto karibia zote ni mzgo wa serikali ambao inabidi waubebe. Maendeleo yoyote katika Taifa lolote huanzia kwenye elimu kama alivyosema mgombea urais wa UKAWA mwaka 2015, kipaumbele ni 1. ELIMU 2. ELIMU 3. ELIMU.Na pamoja na yote isisahau kuboresha maslahi ya walimu.

AHSANTE SHULE ZA KATA.
 
Back
Top Bottom