Shule za binafsi kuchangisha pesa ya madawati ni sawa?

Lastname

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
921
296
Shule nyingi za private kama sio zote zinachangisha michango ya majengo na madawati je hili ni sahihi? Maana ile ni shule ya mtu ambaye siku yoyote anaweza kubadilisha matumizi toka shule kuwa kitu kingine chochote sasa anapokuwa anachangisha hiyo michango hamuoni kuwa ni maonezi ?

Kama ni shule za serikali tunajua itaendelea hata matumizi yakibadilika bado ni for public benefits, nijuzeni mnaojua.

Pili, shule nyingi hazijasajiliwa na wanabaki kuhamisha watoto mitihani ikifika kwenda kufanyia shule zingine na sababu zinakuwa hawajatimiza vigezo, hili nalo mnalionaje? Ni sahihi ? kama mtu hajatimiza vigezo si asitoe ile huduma pale mlipomkataza kutoa huduma?

Asante.
 
Hayo yote ni maswali ya msingi mdau.
Tunaomba wanasheria na wadau wa elimu mtusaidie hii kero.
 
shule binafsi ni biashara kama biashara nyingine. na ndiyo maana karo zao ziko juu sana. kuchangisha wazazi kwa ajili ya miundo mbinu ya shule ni wizi kabisa. ni sawa na mwenye duka aje kuwachangisha wateja hela ya kujenga frame, kujaza bidhaa dukani na ya kulipia walinzi, halafu mwisho wa siku wateja mnunue bidhaa kwa bei ya kawaida na faida ni ya mwenye duka. kweli wajinga ndio waliwao.
 
Back
Top Bottom