Je, utaratibu wa Pre-Form one kuwa lazima kwa baadhi ya Shule Binafsi ni sahihi?

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Baadhi ya Wadau wa Elimu wameomba Mamlaka kudhibiti utaratibu huu, huku Wengine wakiona ni Sahihi. Kwa hoja hizi na nyingine nyingi jiunge nasi Twitter Spaces ya JamiiForums muda huu uweze kuwa sehemu ya mjadala huu.

Bonyeza hapa kujiunga > JF SPACES

5DDDFC68-B9E0-40D6-A046-D907F5FDB6CF.jpeg


Mkaka Smart
Mimi nachukulia positive jambo hili kwakuwa humfanya mwanafunzi kuwa active akiwa anasubiria muda wa kwenda shule kuliko mtoto atakaye kaa nyumbani pekee.

Pia siyo mbaya kwa maana ya biashara kama ambavyo shule zenyewe zinakuwa zimedhamiria.

Kuhusu sera ya wanafunzi kupumzika kabla ya kuanza form one, kwa maoni yangu, Serikali ilifanya ili kuruhusu usahihishaji wa mitihani na utoaji wa matokeo.

Ni muhimu watoto kwenda huko, lakini isiwe lazima, hii siyo nzuri. Shule za binafsi zisiwele ulazima huu.

Nashauri regulators wa sekta ya elimu wachukue hatua kwa kuwa swala hili halijawekewa ulazima wa kisheria, shule binafsi zifuate utaratibu. Isiwe lazima, wanaweza kufanya mitihani ya usaili ili kuchuja watoto, lakini pre form one isiwe lazima.

Ziada O. Seukindo
Issue ya pre form one siyo lazima, na sijui ni nani aliianzisha na kiukweli kapata wafuasi. Wengi wanaotetea hili wengi huwa na mawazo ya kuwa watoto wamesoma kiswahili hivyo waende kujifunza kiingereza. Kwangu mimi sioni significance ya hili.

Pia pre form one inatengeneza matabaka kati ya waliosoma na ambao hawakusoma, baadhi ya walimu hukimbiza masomo kwa kudhani wanafunzi wote wamesoma. Pia, siyo fair kwa kuwa wanafunzi wanahitaji kupumzika.

Kama wazazi tumekuwa na tabia ya kutokupenda kukaa na wazazi, kila muda tunawatafutia watoto pa kwenda, hatuna muda wa kuwasoma na kuwafundisha malezi. Kama point ni kuwalinda na maovu, hata huko mashuleni wanakutana tu na vijana wenzao, siyo sawa kutafuta sehemu nyingine ya kumlea mtoto ili akiharibika upate sehemu ya kulaumu.

Chucho
Wakati zinaanziswa zilikuwa na lengo la kuandaa wanafunzi ili wafanye vizuri sekondari kwa kuwa wengi walitoka shule za serikali. Kwa sasa naona kama ni biashara ili kila shule ipate pesa.

Ushauri wangu, iwekwe misingi tangu chini ili watoto wasome kiingereza mapema (tangu shule za msingi) ili waweze ku capture vizuri masomo.

Apostle Lukumay
Imekuja kwa lengo kumfaidisha mwanafunzi, lakini kiukweli haina mchango wowote. Walimu wajenge urafiki na wanafunzi, wasifanye madaraja kwa wanafunzi kati ya wanafunzi wenye uelewa tofauti.

Walimu wawekeze nguvu kwa wanafunzi wote, wataweza kujifunza na kufaulu vizuri mitihani yao.

Kajemi Kefa
Swala hili ni zuri lakini linaleta matabaka. Pia, hawa wanafunzi wadogo wanahitaji kupumzika kama ilivyo kwa binadamu yeyote yule. Kwangu mimi japo inasaidia, siyo muhimu sana.

Mtoto akikaa nyumbani anaweza asipate mambo ya shule, lakini atajifunza mambo mengi ya kimaisha.

Sopa
Haina ulazima sana lakini ni muhimu, inawajengea uzoefu wa kuelewa mapema kwa kuwa kuna utangulizi wa lugha amepata. Lina faida kubwa kwa mwanafunzi kuliko kwenda kupumzika tu nyumbani.

Nchi yetu ina tatizo kubwa la uhaba wa walimu, na ongezeko kubwa la wanafunzi kutokana na sera ya elimu bure. Pre form one inasaidia walau watoto waelewe japo kidogo.

Sisapoti swala hili kuwa lazima, lakini ni jambo lenye umuhimu mkubwa.

Imbonerakure
Kwa mtizamo wangu kama mwalimu ni muhimu kwa shule, mzazi na mwanafunzi lakini siyo lazima.

Elimu ni huduma, ni lazima iwe na namba ya kumvutia mteja, ni kama booking. Shule hizi zinavutia wanafunzi, ukiondoa hiyo shule nyingi hazitapata watoto, ukiondoa zinaweza kukosa kabisa, au zikapata wachache.

Mzazi anaweza kubwa busy (hasa wale wa mjini), program hizi zinafanya watoto wasiwe idle, inawafanya watoto waendelee kuwa kwenye program ya usomaji. Serikali isisitishe huduma hizi ili kuwalinda watoto wasijiingize kwenye makundi mabaya.

Samwel Lemonji
Siyo lazima, na ukifanya analysis hadi sasa utaona kuna wanafunzi wamefika chuo kikuu na hawakwenda pre form one. Kwangu hili ni swala la kibiashara zaidi.

Mkabahati
Ni kumtesa tu mtoto, huwezi kutoa elimu ya mwaka mzima kwa miezi 3. Ni wastage of time.

Kusema pre form one mtoto anaenda kujifunza mambo ya form one siyo kweli. Mtoto apumzike nyumbani, bora aende tuition za mitaani.

Kama lengo ni kuwasaidia waliosoma Shule za Kiswahili kwanini na aliyesoma kwa Kiingereza kuanzia Darasa la kwanza analazimishwa kusoma Pre form one?

Huu utaratibu uwe ni chaguo la Mzazi, Mzazi akiona mwanae anahitaji Huduma hiyo ampeleke na sio kulazimishana

Ni uchoshaji tu, watoto wabaki nyumbani. Kama ni kuangalia uwezo wanaweza kufanya interview. Mimi sisapoti, mtoto akae nyumbani kufanya mambo ya kijamii.

Agnes Madole
Mimi ni mzazi, nina mwanafunzi wangu kapita interview lakini wamesema mtoto ni lazima asome pre form one na asiposoma hawatampokea.

Tume opt kumpeleka shule ambayo siyo lazima kusoma pre form one, maana maisha siyo shule tu. Kuna shule zinalazimisha, hii siyo sawa. Inakuwa kama upigaji, iwepo kwa anayetaka.

Wizara ya elimu iangalie namna ya kuweka muongozo, ushindani usiachwe kuwa huru kiasi hicho.

El Mayo
Hii ni hoja nzito, lengo ni kuinua taaluma kwa shule na wanafunzi wenyewe.

Ugomvi wangu ni kufanya lazima, inakuwa wanaangalia fedha zaidi. Kuna makosa makubwa sana yanayofanyika, ni kama kumpoteza zaidi mtoto, sababu mtoto mdogo ubongo wake una kiwango fulani cha kupokea.

Mtoto apumzike, haina ulazima.

Benedicto Luvanda
Kama mtoto anatakiwa kwenda form one na tunaona kuna gap, basi kuna umuhimu wa kuangalia jambo hili ili lifanyiwe kazi.

Kuna sehemu kielimu hapajakaa sawa.

Nderumaki Frank
Ni kweli, biashara ya shule siyo rahisi. Ni moja ya njia baadhi ya shule zinatumia kujipatia fedha za kujiendeshea.

Elimu yetu imejikita kwenye mitihani, shule nyingi za binafsi zinatumia njia hii kama mkakati wa kuendelea kuwepo kwenye soko.

Goth
Mmoja wa wadau akichangia mjadala wa JF alisema yeye aliawauliza shule kama anaweza kulipia pre form one na mtoto asiende, wakasema YES.

Hii inamaanisha lengo mama siyo kusaidia mwanafunzi zaidi ya kupata pesa.


Marande
Kama mwalimu, naona hakuna umuhimu wa pre form one. Kwangu mimi hoja ya mwanafunzi kufaulu vizuri kwa kuwa kapitia pre form one siyo kweli.

Didy
Pre form one siyo lazima. Sijaona kama inaongeza thamani yoyote, labda kwa shule za seminari ambazo zinatoa elimu zingine mfano dini.
 
Wana kompliketi mambo tu na namna ya kupata pesa na kuuza Tshirts kwa hao Pre form one.
Mbona sisi enzi zetu kulikuwa hakuna hiyo pre form one na watu tulikuwa tunafaulu vizuri tu tulipoanza form one.
 
Mwanafunzi anamaliza darasa la saba, October 5& 6 baada ya kumaliza mtihani wake. October 14 anatakiwa anze masomo ya pre form one, tena Shule ya Bweni. Hapo kanunuliwa Godoro, sale za shule na mahitaji mengine.

Na kuipata hiyo shule ni baada ya kufanya mtihani wa majaribio/interviw mbalimbali kwa gharama isiyo chini ya Sh 20,000 kwa kila interview.

HAYA YOTE YASINGE WEZA KUFANYIKA AWAMU ILIYOPITA. HAYA YANAWEZEKANA SASA.
 
Back
Top Bottom