Shitambala wa Chadema Mbeya ahamia CCM - Chadema kuchukua hatua za kisheria

Nimependa hoja yako Mkuu
Siasa za kurubuni viongozi wa upinzani kuhamia CCM hazitaisaidia CCM, kwa sababu zifuatazo.
  1. Waliishafanya hivyo huko nyumba na kuwapa watu kama kina Tambwe Hiza, Makongoro, Akwilombe, Maghimbi et al. Wananchi wanajua fika kuwa watu hawa wamefuata masilahi binafsi huko CCM na hilo haliwaongezei wala kuwapunguzia matamanio yao ya kuing'oa CCM madarakani kwa kuwa imekuwa ikiwadanganya tokea uchaguzi wa vyama vingi 1995.
  2. Chama hakijengwi na mtu mmoja kwa kuwa jina lake ni Shitambala au hata Dr Slaa, bali ni chama as whole kuonyesha kuwa kipo kwa ajili ya wananchi usiku na mchana na kina watu wenye uwezo wa kufikiria bila woga na kuyatamka mabaya yote yanayosemwa na wananchi chinichini kwa kuhofia kushughulikiwa na vibaraka wa watawala.
  3. Kitendo cha CCM kumrubuni mtu yeyote wa upinzani na kumpatia nafasi ya ulaji wakati CCM kina wanachama walio-committed na wanasota ni kuzidi kuwafanya hawa CCM committed kujiona kuwa ni useless na hivyo kuanzisha minyukano ya hadharani na gizani miongoni mwao, rejea kauli ya Sumaye kuhusu kauli ya Tambwe Hiza.
  4. Kumshikisha mlungula Shitambala ili aiponde CHADEMA ni mchezo wa kitoto sana, only mwendawazimu atadhani kuwa mchezo huu utafanya CDM iporomoke kwenye uso wa wananchi. CCM wanatakiwa kutumia scientific approach kwenye kuiporomosha CDM siyo mbinu za kwenye vijiwe vya kahawa. Kama mimi ningekuwa mshauri wa CCM ningeagiza research ( I mean scientific research siyo kupokea taarifa za kishushu bila kufanyiwa empirical analyis) ifanyike nchi nzima ya kujua mambo yafuatayo 1. Ni kiasi gani wananchi wanaamini taarifa zinazotolewa na serikali au CCM kuwa kweli au si za kweli, 2. Ni kama jibu la (1) ni ndiyo kwa nini au kama siyo kwa nini, 3. Ni wananchi wa rika gani hasa wanakubaliana au kukataa CCM na kwa nini, 3. Kwa nini wanadhani CDM itawakomboa kiuchumi au haitawakomboa, 4. Watanzania wanajisikiaje kujitambulisha kama wana CCM , au wana CDM na kwa nini?, 5. Je wananchi wanaridhika na uongozi wa CCM na serikali yake, na kwa nini?. Nini kikifanyika watakuwa tayari kutoiunga mkono CDM, au CCM na kwa nini?. Je wanadhani CCM ilishinda uchaguzi wa 2010?, kama ndiyo kwa nini na kama siyo kwa nini, Je wanaiona CCM ipo kwa masilahi ya nani hasa? na kwa nini? PLUS MASWALI MENGINE MENGI TU, Baada ya hapo unakaa chini na kufanyia kazi all positive results on the side of CCM hata kama itabidi JK kujiuzulu na kumwachia makamu amalizie ngwe iliyobakia. Baada ya hapo hakikisha kuwa focus kuu ni kuhakikisha vijana wanapata ajira bora na kutomuonea huruma yeyote yule atakaye kwenda kinyume. In general let the Public see that CCM is not there for its members but for poor people.
  5. Chama hakijengwi na mtu bali na watu makini na kwenye hili CDM inaongoza na imepiga bao, sooner or later CCM would be a history if their trend of increasing its popularity is via seducing oposition leaders to defect and using false propaganda. If you are in power the only propaganda people can believe is for you to use an advantage of being party in power by initaing programs and policies which can lift people from poverty anything short of that is lack of thinking and waste of an opportunity. You can't use tricks and force to remain in power forever.
 
nadhani shitambala hakuwa na msimamo thabiti, ila hasira mbaya, huwezi ukawa kiongozi wa chadema ukataka uongoze kama malaika, cdm ni taasisi ya siasa ambayo lazima ujitolee kama huyo aliingia cdm kwa maslahi binafsi, ndio hayo tumeyaona hata alikoenda kuna migogoro mingi tena afadhali hata cdm, sababu bado inakuwa
 
Shitambala hana jipya,amegombea Ubunge three times Mbeya Mjini na awamu zote amaekuwa akiuza nafasi hiyo kwa CCM.Amekuwa akipkea mamilioni kutoka CCM ili kukisalititi CDM.Kwa ujumla hakuna hasara ya kumkosa huyo mamluki hapa Mbeya.Moto umewaka na katu hauzimwi na maluweluwe haya ya CCM.Tutapambana hadi damu ya mwisho.
 
Umeona eeeh! Sijui inakuwaje hii M/kiti wa mkoa
Hizi njaa gani tena haya nani anafuatia Katibu wa Wilaya ya Wabulushi ya Ileje Duh! Haya who is Next? Ngoja 2subiri 2jione ye2 Macho!
 
Anajaribu kuzuia moto kwa kuumwagia petrol bora angetoka kimya kimya kuliko kututhibitishia kuwa amenunuliwa na JK ****** ayazungumze hayo. Nice thought but too late for the implementation Mr. Shitambala
 
wewe unapara miwa

Duh! Ama kweli Anapara miwa! Jiheshimu watu wana maneno machafu humu Wakiaanza itakuwa tunapoteza maana nzima ya Great thinker! Asikutie homa Shitambala, kwani chama si mtu moja. Kashaona hapamfai Chadema mwache asepe zake
 
Sasa Waislamu wanasema CHADEMA ni chama cha Wakristo
Sasa watuwengine wanasema ni Chama kisichopenda Amani

Huyu Mkristo Mwenyekiti wa Zamani wa Chadema Mbeya anasema CHADEMA ni Chama cha Kikabila

It is very fascinating...
 
Sasa Waislamu wanasema CHADEMA ni chama cha Wakristo
Sasa watuwengine wanasema ni Chama kisichopenda Amani

Huyu Mkristo Mwenyekiti wa Zamani wa Chadema Mbeya anasema CHADEMA ni Chama cha Kikabila

It is very fascinating...

Ndio kwanza nasikia
 
vyama vya msimu vina kazi kwelikweli,na bado wengi wataondoka tuu hata Slaa hana raha kwasasa kwa mtu aliyeonana nae na ambaye amesoma psychology anaweza kuthibitisha hilo

psychology ni uwanja mpana kaka, which category of psychology are talking about, bcoz me cjaona kama hana raha.
Alafu hata kama hana raha kwani nani kakudanganya kwamba knowing psychology itafanya ujue kwamba mtu hana furaha kwasababu ya kitu fulani(labda siasa) just kwa kumuona?
 
Si haki kumhusisha Zitto na hili......tumjadili huyu Shitambala kivyake.......kama Zitto nae akihamia CCM basi tutamjadili atakapofanya hivyo.....kwa sasa si haki kufanya hivyo

Aliagiziwa toka kitambo kuimaliza cdm, bt amejaribu akiwa amechelewa. Kakuta wa2 wameishadamka toka kuchwili alfajiri. Ka2mia njia zote za kishushu bt (peni imeisha wino) am out.
 
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM Bw. Sambwee Mwalyego Shitambala aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha CCM baada ya kukihama rasmi CHADEMA katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo mchana.
 

Attachments

  • GO9G5003.JPG
    GO9G5003.JPG
    96.8 KB · Views: 61
  • GO9G5073.JPG
    GO9G5073.JPG
    123.1 KB · Views: 55
That cannot be the news to trouble someone's mind.

Huyu alishakuwa na doa. Wapiga kura wake mwenyewe walikuwa hawamtaki. Naamini Slaa aliposema ana imani naye, ilikuwa tactic tu ya kununua muda ili jamaa adhihirishe upopo wake.
 
Back
Top Bottom