Shitambala wa Chadema Mbeya ahamia CCM - Chadema kuchukua hatua za kisheria

Hakuna msomi asie na uwezo wa kuandika biography yake ila Shitambara.
Hivi kweli huyu anavyojiita wakili, kuna kumbukumbu yoyote ya kesi aliyowahi kushinda?
Hata kama ipo kwa ukilaza wa shitambaa, ni dhahiri itakuwa mteja wake ndie alieyemwongoza katika hiyo case.
Haka kajamaa kana majivuno na kashamba fulani hivi, nilikagundua baada ya kukashuhudia kama mara tatu kwenye campaign kakiwa kanaongea huku kamejishika kiuno.
.
 
Namhurumia huyu jamaa lakini nafikiri bora ameondoka mapema CDM kwani si rizki kwa CDM. Pili ana akili mgando kurudi chama ambacho tayari kimeshaoza cha CCM ambacho kiukweli kinakata roho. Tatu kuondoka kwake CDM hakuna athari yoyote aidha kwa CDM wala aendako hawezi pata chochote bora angeachana na siasa abaki na kazi yake. NNe ana sababisha damage kubwa kwa kazi yake kama wakili kwani ni vigumu kumwamini mtu kigegeu na asiye na subira.
 
Niko hapa Uyole usiku huu huko nje kuna gari linatangaza kuwa kesho kutafanyika mkutano mkubwa wa kumpongeza Shambwe Shitambala kwa kurejea CCM. Wanawahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika mkutano huo

My take: Wanadhani tunadanganyika, wengine kesho kazini kama kawaida tena kesho nitapiga na overtime na Jumamosi asubuhi nipo barabarani kwenye maandamano yatakayoongozwa na Mh.Mbowe.
Hakuna kudanganyika mkuu mpaka kieleweke safari hii. Who is Shitambala to make them proud to that extent? Mbona mimi sijawahi kumsikia kama naye ni mmoja wa wapambanaji wa Chadema. Ni vyema ameondoka mapema CHADEMA maana inaonekana ndiye aliyekuwa anatumiwa kuficha fomu za wagombea wa CHADEMA mpaka wabunge wa CCM wakapita bila kupingwa kwenye majimbo ya Mwakyusa, Mwandosya n.k. Boga tu hilo
 
hiyo prosecution itakuwa ya kijinai au kimadai, kama ni rushwa obviously ni kijinai sasa DPP atakubali kutoa kibali kwa CDM ku prosecute, mi nakubaliana na LAT ni busara kumuacha tu huyu jamaa alijawa na tamaa
 
sisi tunasema kwamba shitambala ana tamaa na uroho wa pesa na madaraka na fisadi mukubwa kanaona akimbilie kwenye bahari ya mafisadi hakika nawaeleza mtu huyu hatofika popote kwani huu ndio mwisho wake kisiasa.
 
Hivi hilo jina la SHITAMBALA halimaanishi "tambala bovu" au kitambaa kilichochakaa? Nahisi kama vile ni tambala bovu na linastahili kwenda CCM ndo kunakomfaa..
 
Mark.mim sikuwaona waliotangazwa kurudi CCM Pamoja na Shitambala,hakuna mwana CDM aliyehama na bwana Shitambala isipokuwa kibaraka mwenzake bwana Kayuni aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la ILEJE.Hao 150 Unaowazungumzia ni hadaa na changa la macho kwa umma na JK. jk anadanganyika,lakini umma wa watanzania haudanganyiki.
 
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya anapokea kadi ya CCM sasa hivi na amemaliza kuongea kuwa Watanzania waiogope sana CHADEMA ni chama cha wahuni na wana uwezo mkubwa wa kufanya fujo na kuzomea! Amesema CHADEMA ni chama cha kikabila na kinaongozwa kwa mtindo wa Kampuni ya Mtu binafsi au kampuni ya kifamilia! Haja mtaja nani mmliki wa CHADEMA ila kasema CHADEMA ina mwneyewe ambaye hasa ndio mwenye kampuni na Dr slaa ni kibarua tu pamoja na wengine! Bado anaendelea kuongea!

Unajua maana ya Shitambala??
Sijawahi kumsikia mazuri ya huyo jamaa kimsingi wanambeya tulikua tunamvumilia tu kwa ajili ya Dr Slaa, but alitakiwa kuondoka siku nyingi saana, SHitambala Shitambala!, mwache aende, si anajua ndo anaiona pepo??, Sasa sijui atagombea wapi!. Mbeya ni wazi kwamba hatoshinda hata kidogo!

Mbeya City Stand Up!
 
Back
Top Bottom