Shitambala awania ujumbe wa NEC

Ataweza minyukano ya RUSHWA? Kwa sababu zile pesa alizokuwa akipewa alipokuwa CDM sasa ni wakati muafaka kuzirejesha pamoja na riba, maana kwa hiyari yake aliamua kutoka kwenye utafutaji uongozi kwa njia ya haki mpaka kwenye utafutaji uongozi kwa njia za kiharamia(yaani rushwa). Je, ataweza?
 
[h=2][/h] Jumamosi, Septemba 01, 2012 06:29 Na Pendo Fundisha, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya, Kapteni Sambwee Shitambala na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amejitokeza na kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wilaya ya Mbeya Mjini.

Shitambala alichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha ofisi za CCM wilayani humo, akiwa ni mwanachama wa 12 kati ya waliochukua fomu za nafasi hiyo kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu hiyo kwa Kaimu Katibu wa CCM wilayani humo, Julius Msaka, Shitambala alisema nia yake ni kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

Alisema nia na dhamira ya kugombea nafasi hiyo ni kuwatumikia wananchi ambao kwa sasa wanahitaji mabadiliko ya kweli katika uchumi na kijamii kwa ujumla.

“Nia na dhamira yangu ni kuwatumikia wananchi na kukiwakilisha chama changu kwa nia moja ya kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi na niwahakikishie kuwa CCM bado ina nafasi kubwa ya kuongoza nchi,’’ alisema Shitambala.

Wanachama wengine wa CCM waliochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Obadia Mbilinyi, Shua Mwasanguti, Aggrey Mwasanguti, Dk. Stephen Mwakajumilo, Burton Mwankunda, Frank Mahemba, Edson Kajigili, Maria Nyagawa, Fatuma Kasenge, Richard Shanghvi na Daniel Fusi.

Kwa upande wake, Msaka alisema wanachama wote wamepewa onyo la kutojinadi wala kuchumbia wapiga kura hadi siku ya uchaguzi na vikao vinavyohusika kupendekeza majina ya wagombea waliokidhi vigezo vya nafasi hiyo.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]

Kama kuna kitu ambacho kinawatafuna ccm ni watu dizaini ya kina shitambala wanapopewa nafasi na kuwaacha watu ambao wamekulia kwenye mfumo wa chama na wamekuwa na mapenzi na chama chao lakini sababu kuna mtu ametoka CDM basi anapewa cheo.mtu ana hata miaka mitatu ndani ya chama anagombea nafasi ya juu!Go Go CCM the grave is yours.
 
Shitambala ni jembe la ukweli,hapa mnamponda kwa sababu ametambua ukweli na kuondoka kwenye chama kinachomilikiwa na watu wachache na sasa yupo kwenye chama cha watu wote
 
Kama kuna kitu ambacho kinawatafuna ccm ni watu dizaini ya kina shitambala wanapopewa nafasi na kuwaacha watu ambao wamekulia kwenye mfumo wa chama na wamekuwa na mapenzi na chama chao lakini sababu kuna mtu ametoka CDM basi anapewa cheo.mtu ana hata miaka mitatu ndani ya chama anagombea nafasi ya juu!Go Go CCM the grave is yours.

nyani haoni kundule.hayo ndio yanayofanyika katika vyama vya upinzani hasa chadema
 
Ataweza minyukano ya RUSHWA? Kwa sababu zile pesa alizokuwa akipewa alipokuwa CDM sasa ni wakati muafaka kuzirejesha pamoja na riba, maana kwa hiyari yake aliamua kutoka kwenye utafutaji uongozi kwa njia ya haki mpaka kwenye utafutaji uongozi kwa njia za kiharamia(yaani rushwa). Je, ataweza?

unakumbuka kwa nini uchaguzi wa bavicha taifa uliahirishwa mara kadhaa?unakumbuka ni kwanini uchaguzi wa wabunge viti maalum chadema uliahirishwa mara kadhaa na pia kugubikwa na minyukano ya hapa na pale?nyani haoni kundule
 
Huenda huo ukawa mwisho wake wa kisiasa kama atashindwa,

Uwezekano wa kushinda ni mdogo sana, hiyo ni kondom iliyotumika hakuna aliyetayari kuitumia tena!!
 
Back
Top Bottom