Ndivyo chama kinavyojengwa hivyo. Rumi haikujengwa kwa siku moja, lazima CDM ikubali kuwa kuna kupanda na kushuka. Shitambala asiweke masharti mengi sana, na mimi sikuona haja ya yeye kujiuzulu kwa sababu ya maneno ya mitaani. Kama ingekuwa maneno tu yanamfanya mtu ajiuzulu basi pasingekuwa na viongozi. Unapojiuzulu ni pale unapoona kwa dhamiri yako kabisa kuwa una hatia katika tuhuma hizo, lakini kama ni maneno tu ya mitaani, no Mr Shitambal alitakiwa kupuuza kwa manufaa ya chama. Mwana mapinduzi huwa hakati tamaa mapema kiasi hicho.
Long live CHADEMA
Kweli kabisa hatukimbii matatizo bali tunayakabili mpaka tupate suluhu