Shibuda sasa amvaa Dk Slaa, adai kuwatumia BAVICHA

Chokochoko hii ya Shibuda si bure! kuna jambo. CDM wanyamaze, akiona kimya atatafuta kingine. Kuna wakati atabogi step tu.
 
Ukisikia habari za uongo na udaku ndio hizi.

Mbunge wa CHADEMA akaingia kwenye kikao cha Nationa Executive Committe ya Chama Cha Mapinduzi umeanza lini utaratibu huo? Na akaongea kama nani??? Magazeti yetu mbona yamekaa kidaku daku hivi???

Hapo kwenye red, Shibuda mwenyewe amethibitisha kuhusu kauli zake hasa nia yake ya kugombea urais 2015, sasa wewe unabisha nini? Udaku uko wapi? Nilitegemea ujue kuwa Shibuda ni mamluki wa CCM ndani ya CDM na ni mkakati wa CCM kupunguza M4C. Shibuda ni mtu tu CDM na anapaswa kupuuzwa kama Dr Slaa alivyofanya!!
 
Of course Shibuda si lolote wala chochote.

lengo la shibuda ni kuivuruga chadema sasa wamemshitukia na busara tu ya chadema kamwe hatafanikiwa atapambana na bavicha tu kwa kuwa wanamisimamo na wanaweza kumthibiti pasipo shaka wala woga, hao ndio chadema, chama cha watu kwa ajili ya umma sio cha wachache.
 
Tumpuuze shibuda,hana madhara na spidi yetu ya kuchukua nchi mwaka 2015. Yupo kwenye msafara wetu kwa bahati mbaya,
 
Chokochoko hii ya Shibuda si bure! kuna jambo. CDM wanyamaze, akiona kimya atatafuta kingine. Kuna wakati atabogi step tu.

naweza kukiamini walichoakiandika RAI leo kuwa Shibuda na Juliana wanatumiwa na CCM kuidhoofisha Chadema
 
[MSUGUANO wa vijana wa Chadema (Bavicha) na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki , John Shibuda, umezidi kuongeza joto la kisiasa ndani ya chama hicho baada ya mbunge huyo kumrushia kombora Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa, akisema ndiye anayewatumia vijana hao kumhujumu.

Tayari Shibuda ameigawa Bavicha baada ya Mwenyekiti wake, John Heche kupingana hadharani na makamu wake, Juliana Shonza kuhusu msimamo wa baraza hilo dhidi ya hatua ya mbunge huyo kutangaza dhamira ya kuwania urais mwaka 2015 ndani ya Nec ya CCM na kumwomba Mwenyekiti wa chama hicho tawala, Rais Jakaya Kikwete awe kampeni meneja wake.

Wakati kauli zake hizo ndani ya Nec ya CCM zikitarajiwa kumweka katika hatari ya kufukuzwa ndani ya Chadema kipindi hiki ambacho amekuwa katika uangalizi maalum, Shibuda jana aliliambia Mwananchi kwamba, yuko tayari kwa lolote na wakati wowote tena kwa asilimia 100.

Shibuda alifafanua kwamba anatuhumiwa kukihujumu chama huku akiwa hajawahi kukiuka maagizo yoyote ya Kamati Kuu ndani ya Chadema , lakini amebaini kuna baadhi ya watu wanatumiwa na viongozi wa juu wa chama hicho akiwamo Dk Slaa kwa lengo la kumfanyia fitina na hujuma.

Alisema kitendo cha Dk Slaa kukalia kimya shutuma zinazoelekezwa kwake na vijana hao wa Chadema kinampa fursa ya kuamini kwamba vigogo wa chama hicho wako nyuma yao na kumtaka sasa Dk Slaa aeleza hadharani uovu wake huo ili Watanzania wafahamu ukweli kuhusu sakata hilo.

"Mimi sina kosa lolote ila ninachofikiria ni kwamba Bavicha wanatumiwa na viongozi wa juu wa Chama ili kutaka kuniharibia lakini cha msingi ni vyema Katibu Mkuu wetu (Dk Slaa), akaweka hadharani maovu yangu ili Watanzania wajue makosa yangu ni yapi," alisema Shibuda na kuongeza:

"Ni wakati wa Chadema kupitia viongozi wake wakuu kueleza ubora wake wa kuwaongoza wananchi uko wapi kwani kama mtu anatangaza nia na kuonekana ameenda kinyume, sidhani kama kuna uongozi thabiti."

Kitisho cha kufukuzwa

Akizungumzia kitisho cha kuweza kufukuzwa Chadema, Shibuda alisema kwa sasa yupo tayari kwa asilimia 100 kupokea jambo lolote litakalotokea dhidi yake ndani ya chama hicho na kwamba kinachotakiwa ni kuonyeshwa makosa yake.

"Kwa asilimia 100, kutoka moyoni nasema nipo tayari kwa lolote litakalotokea kwangu ndani ya Chadema, kwani mimi natambua wazi sina kosa nililolifanya na kama nina makosa basi yaanikwe hadharani ili wananchi nao watambue," alisema.

Akizungumzia kupewa barua ya karipio kali, Shibuda alisema kwamba, hata siku moja hajawahi kupewa barua yoyote ya karipio kali na hafahamu chochote juu ya suala hilo.

"Sikiliza ndugu mwandishi, mimi sijawahi kupewa barua yoyote ya karipio kali na sifahamu chochote juu ya suala hilo labda hao walionipa barua hiyo wangeeleza lini walinipa," alisema.

Kauli ya Dk Slaa

Akizungumzia tuhuma hizo za Shibuda, Dk Slaa alisema asingependa kuingizwa katika mjadala huo kwani hajawahi kumzungumzia Mbunge huyo kuhusu jambo lolote wakati wowote tangu mjadala wake na Bavicha ulipoanza.

Alisema haoni suala la Shibuda kama ni jambo la kuzungumzia kwa sasa kwani halina msingi na kuna mambo mengi ya kujadili ili kuliwezesha taifa kupambana na umasikini.

"Mimi nisingependa kuhusishwa na suala la Shibuda kwani sijawahi kuzungumza chochote kumhusu yeye na kwamba, nina mambo mengi ya kuangalia na sio Shibuda," alisema Dk Slaa na kuongeza:

"Sipendi kuzungumzia kauli za watu hata kidogo kwani tunakazi kubwa ya kupambana na kuwakomboa wananchi kutoka katika umasikini."
]


Safi sana......FOCUS ya katibu iko vzuri kweli zipo ishu nyingi za ku deal nazo sio kupoteza muda na huu ujinga.....Bavicha wenyeviti wa matawi au wana jamii twaweza kuchangia na kurumbana tuache jembe letu lifanye kazi za msingi!
 
Mkuu fuatilia mambo usikimbilie mambo. Shibuda aliingia kwenye NEC ya CCM akiwa kama mjumbe wa APRM iliyokuwa ikiwasilisha mada kwenye kikao hicho.

yan una angaika kumjibu mtu ambaye ajui kinacho endelea
 
Baada ya shibuda kuona hajafanikiwa kumnasa Dr.Slaa ndipo alipoamua kumtaja live ili angalau aseme neno lolote ili apate nguvu ya kuikologa CDM.

Cha kufurahisha ni pale Dr. Slaa kama nabii vile, kampuuza kabla shibuda hajamwomba Slaa aseme neno. Hii ni nzuri sana na hapo ndipo naamini ukimtanguliza Mungu, atakuonesha wabaya wako ili wengine uwapuuze kama Slaa alivomtenda shibuda.

Ushauri wangu Kwa
Dr. S
laa.
  • Please huyu kiumbe (shibuda) anatafuta mtu kwani tangu anatangaza nia mbele ya NEC ya CCM alikuwa tayari kasha poteza uanachama ndani ya CDM kuanzia nia yake, akili na mawazo pia. Napendekeza apewe adhabu ya kisaikolojia ambayo tayari ameshaanza kuitumikia tangu Dr. Slaa na Mbowe waliposema maswala ya shibuda siyo hoja ya kuwafanya wafikilie bali wanafikiria maswala ya msingi. Hiyo tu inampa maumivu kiasi cha kuwaomba wafadhili wa dili lake afenye nini baada ya hapo. Ndipo wanamshauri labda mtaje Dr. slaa ili tu aseme lolote.
  • Achana naye kabisa na ikiwezekana ajadiliwe baadaye sana baada ya M4C kumaliza mikoa yote TZ
 
Kaka bado una muda wa kuleta thread za Shibuda hapa jamvini????? Achana naye bwana, hata kutumia sekunde kadhaa kuchangia hoja juu ya huyu kichaa ni kupoteza muda na nguvu....!!!!!
 
Asante sana kaka,make nasikia kasha kubali. Pambafu yake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1. Pepoooooooooooooz poweeeeeeeeeeeeer!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kukaa kimya ni jibu sahihi kwa mwenye akili kumpuuza mpumbavu.
 
Ukisikia habari za uongo na udaku ndio hizi.

Mbunge wa CHADEMA akaingia kwenye kikao cha Nationa Executive Committe ya Chama Cha Mapinduzi umeanza lini utaratibu huo? Na akaongea kama nani??? Magazeti yetu mbona yamekaa kidaku daku hivi???

uko wapi wewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom