Shibuda achangia bajeti ya waziri mkuu; ataka posho ziongezwe kwa jina jipya

Mkuu, mbona umesoma hii habari na ukakimbilia kuanzisha thread nyingine kumbe hata kuelewa hujaelewa!!!

Mkuu hii ni update ya Thread yangu, tazama muda wa thread ndo ujue tunachokipigia kelele haya ndio marejesho ya viongozi japo tumetahadharisha maamuzi ya kukurupuka hayatakuwa suluhisho.

Tunahitaji kujipanga hapa, kumbuka idadi kule bungeni kujenga upinzani inahusika hasa kwa hiyo kuna umuhimu wa kuchanga mawazo mema ili kuuhadharisha uongozi wetu pia na si malumbano.
 
Anasema ziongezwe zifike laki tano.
Anapingana na wenzake wa kambi ya upinzani

Kashajisahau, Bado yuko CCM! Wakati vyama vinaungana, na hata baadhi ya wabunge wa CCM kuunga upinzani katika kupinga posho yeye anataka iongezwe? Huyu mwenzetu hakuwahi kutoka CCM. Hivi asingejiunga CDM angekuwa anaropoka hapo mjengoni?

Hafai kabisa!
 
Mkuu hii ni update ya Thread yangu, tazama muda wa thread ndo ujue tunachokipigia kelele haya ndio marejesho ya viongozi japo tumetahadharisha maamuzi ya kukurupuka hayatakuwa suluhisho.

Tunahitaji kujipanga hapa, kumbuka idadi kule bungeni kujenga upinzani inahusika hasa kwa hiyo kuna umuhimu wa kuchanga mawazo mema ili kuuhadharisha uongozi wetu pia na si malumbano.

Ninapendekeza CDM wachukue hatua kadiri ya katiba yao. Hakuna haja ya kumbeba mtu yoyote ... waoneshe mfano wa kuchukua stahili inayofaa.

Ni kweli tunahitaji wabunge wapinzani wengi lakini bora wabunge wachache wa ukweli kuliko wabunge wengi makanjanja. Kama Shibuda kakiuka katiba ya CDM achukuliwe hatua za kinidhamu mapema kuepuka kuchipuka makanjanja wengine.

Ninaamini CDM ina viongozi makini na maamuzi yao yatakua ni makini sana. Hali kadhalika yoyote anaetaka kugombea nafasi ya uongozi kwenye CDM lazima ajue hakuna ubabaishaji.
 
YES Maamuzi mazito yanahitajika hapa bila kumuonea mtu aibu
 
Posho kumfukuza Shibuda Chadema Send to a friend

Wednesday, 29 June 2011 22:49
0diggsdigg

MBOWE, ZITTO WASEMA NI MSALITI ASIYEAMINIKA KATIKA CHAMA
Msimamo wake
Lakini Shibuda alilimbia gazeti hili jana atashangaa kama atatuhumiwa kwa maoni yake binafsi aliyoyatoa bungeni juzi juu ya kutaka wabunge waendelee kulipwa posho za vikao vya Bunge.

"Sitarajii Chadema kuna viongozi wanaweza kudidimiza demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, wakati chama kinafanya maandamano kutoa maoni huru kwa Watanzania. Kama mimi sitakiwi kutoa maoni huru basi hakuna maana ya kuandamana kutoa maoni kwa Watanzania".

"Tusitafute hila na visa kwa maslahi binafsi, tutambue kwamba mbunge anapozungumza bungeni anasema kwa maana pana kwa watu wenye mitazamo tofauti kwa lengo la kuleta fikra endelevu".

Alisema kwamba hana habari kama wabunge wote wa Chadema walikutana na kukubaliana kuikataa posho ya vikao vya Bunge.

Shibuda akifafanua zaidi suala hilo la posho japo kwenye Ilani ya Uchaguzi wa 2010 ya chama chake ilitaka kupunguza posho hizo za vikao pamoja na mshahara wa mbunge, alisema, "Ilani ya Uchaguzi ni mpango kazi wa kuendeleza programu ya chama kilichopo madarakani, kwa hiyo hivi sasa hapa bungeni bila kujali itikadi zetu wabunge tunaunganishwa na programu ya kuendeleza nchi, utawala bora na uongozi wa kuongoza fikra za Watanzania".
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Mkuu hapo kwenye red ndio mwanzo wa Bundi ulilolisema. Kama watu hakukubaliana kwenye vikao inakuwaje wakuu waamue tu huku si kuvisha demokrasia ndani ya taasisi? Mimi najua kwamba kuna malalamiko mengi kuhusu maamuzi ya viongozi na kuna wabunge wamediliki kusema kuwa kuna viongozi wanatumiwa na CCM kuidhoofisha CHADEMA.
 
Shibuda si wa Chadema tangu mwanzo,yeye alitaka sehemu ya kupatia ubunge coz mgombea binafsi harusiwi!
Huyu ni wa kumtoa bila kumuangalia usoni otherwise ataendelea kurudisha nyuma mapambano
 
Shibuda lakini anawasaidia CDM kupata Ruzuku kutoka na ubunge wake! CDM kimekuwa chama cha Kisultani marufuku kupinga anachosema Mwenyekiti Mbowe!

Zidumu fikra za MWENYEKITI MBOWE ndio anguko kuu kwa CDM na ni faida kwa chama tawala CCM.Sio siri kama UONGOZI wa juu wa CDM WATAENDELEA NA TABIA YA ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI MUDA SI MREFU CDM ITAKUWA KAMA NCCR AU TLP. JARIBUNI TU KUMTIMUA SHIBUDA NDIO MJUE KUWA HIYO NGUVU YA UMMA MNAYOJIVUNIA UKANDA WA ZIWA IMETOKANA NA NANI?
 
Dr Slaa chomoeni kadi yenu ya CHADEMA kwa huyu mtu. Kwanza hata kadi ya CCM hakuirudisha!
 
Mbunge Shibuda anasema posho ni haki ya mbunge na inaitwa "UJIRA WA MWIHA" na anasema hautoshi na uongezwe hadi laki tano, kuna mbunge kapiga vigelegele kushangilia..
Huyu baba niwakufukuza kabisa, hovyo huyu mtu!
 
Back
Top Bottom