Sheria yetu ya madini na wabunge wasioelewa dhima yao

Mkuu sawa unaruhusiwa ila lazma kule bungeni wabunge wanaulizwa je mnahafiki tuujadili?sasa shida kwa wabunge wafuata upepo a.k.a ndiyo mzee wanaweza kataa. Mfno mdgo hyo mikataba ya madini mingine ilipitiswa bunge la 1995- 2000 wapinzani wanapiga kelele bt wabunge wa ccm wanawazomea na kuupitisha ile leo ndo wanajifnya wala na kibaya zaidi upinzani ndo ulikuwa unaanza kuchipua


Mkuu hapo umenena na hilo ndo tatizo la bunge letu ambalo uchama umejaa mle ndani na wakiwa mle ndani wanaongea sana kuonyesha kuwa wanatetea wananchi ila hakuna kitu ikifika kupitisha miswada ya kuwatetea wananchi wanaufyata
 
Hii haikufanyi ukaacha kutimiza wajibu wako na kuonyesha juhudi ambacho ndio kitu cha muhimu!Unateteaje watu wanaopaswa kuwajibika kwenye mambo muhimu ya nchi kwa hoja dhaifu na historia!
Utakuwa ni upumbavu kufanya jambo lilelile huku ukifahamu matokeo yake ni nini! Yaani unataka wabunge wa upinzani wapeleke mswaada Bungeni, huku ukijua fika hawatofanikiwa?!? Hizo juhudi utakuwa ni upumbavu wa hali ya juu!

Kwanini husiwatake wabunge wa CCM wafanye hivyo? Kwa kuwa wa CCM wakifanya obviously, watafanikiwa. Na kwa umuhimu mkubwa, kwanini husemi Rais awatake wahusika wa sekta wafanye hivyo? Serikali za CCM brought this mess! Kama Magufuli genuinely anataka ku-redress hiyo mess, basi lazima achukue leadership katika hili.
 
Kwa jinsi watu mnavyotoa povu humu ni lazima ujumbe wangu utakuwa umepenya.

Yaani umepenya hadi kunako kabisa.

Naamini hata huyo kasuku wenu naye ujumbe atakuwa kaupata.

Happy weekend
 
Anzieni kwenye dakika ya saba....

Hebu angalieni huyu mtunga sheria anavyosema eti Magufuli abadili sheria.

Eti abadili sheria inayosema 'dhahabu hii ni mali ya wawekezaji'.

Sasa wewe Tundu Lissu kwa nini usi initiate hilo huko bungeni?

Wewe ni mtunga sheria. Na wenzako humo bunge ni watunga sheria.

Umeshindwa kweli kuwashawishi wenzako muibadili hiyo sheria?

 
Mbunge ana uwezo wa kupeleka muswada binafsi bungeni Mkuu!
Kwa kimombo huwa unaitwa Private Member's Bill.

Kwa uhakika zaidi tafuta kitu kinaitwa KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE LA TANZANIA, 2016( Standing Orders of the National Assembly of Tanzania, 2016).

kanuni hizo humpa Mbunge mamlaka ya kuwasilisha muswada binafsi kuhusiana na sheria mpya.

Serikali inapewa mamlaka ya kufanya marekebisho katika sheria zenye makosa baada ya hilo kosa kuthibitishwa au limedhihirishwa mahakamani.

Mtu yeyote anauwezo wa kufanya petisheni( petition) pale ambapo utaona sheria fulani haiko vizuri na inapelekea kuvunja haki zako za msingi wakuu!
Mfano kesi ya REV. MTIKILA V. AG of the United Republic of Tanzania case no. 5, 1993( Kuhusu Private Candidate)
Soma ibara ya 26, 27 na 30( 3) zinatoa muongozo mzuri tu.

I stand to be corrected!
Nipe matokeo ya kesi ya Mtikila.Achana na nadharia angalia uhalisia.
 
Mr. Rock,
Nakupa heko kwa kuokoa hili jahazi maana bandiko lenyewe limekaa kisheria
Halafu mtu anakuja na maneno matupu bila ya kutambua sheria inasemaje!

Kuna ishu zingine huwezi kutumia uzoefu na ujuaji bila kutambua sheria inasemaje.
Ndugai jana kasema,wabunge walete hoja za kuiomba serikali iharakishe mchakato wa kurekebisha sheria ya road licence,mbona hajasema wabunge walete mswada wa kubadirisha sheria?
 
Nipe matokeo ya kesi ya Mtikila.Achana na nadharia angalia uhalisia.
Mtikila alishinda kesi na mahakama iliruhusu kuwepo na wa/mgombea binafsi mkuu.

Mwisho wa siku bunge lilishindwa kutunga au kuweka hilo sharti katika katiba ya jamhuri ya muungano kwa sababu serikali yetu haipo tayari kufanya hivyo kutokana na sababu wanazozijua wao.
 
Ndugai jana kasema,wabunge walete hoja za kuiomba serikali iharakishe mchakato wa kurekebisha sheria ya road licence,mbona hajasema wabunge walete mswada wa kubadirisha sheria?
Mswada wa kubadirisha sheria = Muswada wa kubadilisha sheria.

Tatizo bunge limejaa ukakasi na watu ambao ni closed-minded.

Ingawa mbunge anao uwezo wa kupeleka muswada bungeni kama kanuni za bunge zinavyosema!
 
Bunge gani unaloliongelea? Hili lililojaa maCCM yenye elimu ya kujua kusoma na kuandika?
Bunge ambalo linapitisha bajeti ila Rais anajinunulia tu ndege atakavyo.kujenga tu barabara nje ya bajeti n.k
Bunge hili ambalo wabunge wenu wa Chama Cha Kijani huitwa kikao na Rais na kukaripiwa pindi wakitanguliza maslahi ya wananchi mbele badala ya chama?

Ni kichekesho!!!

Kumbe unapendekeza bunge gani litunge sheria? Unatamani wabunge wote wa CCM wanaojua kusoma na kuandika tu wasiwepo ila lijumuishe Sugu na mtunzi mwenzie Pro.J anayewakilisha Mikumi ndipo tupate sheria nzuri ya madini?
 
Absolutely!

But all they do is just whine, moan and groan.

Last time I checked whining, moaning, and groaning didn't get anything done.

It's actions that get things done.

Hii ndo shida yetu wala MASANGU. Unawalaumu wanafunzi kw kutokununua chaki?
 
Lisu ana akili kuliko watanzania wengi hasa wanaoamini CCM ina nia njema na nchi hii kwa sheria hizo zilipitishwa na upinzani?

Kama upinzani hauna nguvu ya kupitisha ( idadi ndogo) sheria unategemea nn?

Malalamiko ya Lisu ni makubwa zaid kuliko kutoa mswada wa kbadr sheria coz CCM hawatapitisha kwa maana wana masirahi binafsi na mikataba hiyo

Swali je mchanga unadhamani kubwa kuliko madini yenyewe? Kwanini raisi hajaanza na madini kwa ujumla?

Lisu na upinzani wanamuunga mkono RAIS kuliko WanaCCM coz upinzani hausemi RAIS asishuhurikie swala hilo bali linapika kelele kumsaidia RAIS ili anachokifanya kiwe na tija zaidi na asiliingize Taifa kwenye migogoro bali sheria zifanye kazi


Upinzanzi wanataka sheria iseme na si RAIS aseme kwa msemo wa no one above the law
 
Tatizo la Tundu Lissu ni kila wakati kutafuta Rais kakosea nini ili akamtukane kwenye media.
Anayoyaongea yote hakuna jipya na wala hakuna asiyeyajua. Lakini kwa sasa tunataka solutions sio kulaumiana.
CCM walifanya makosa YES, lakini tumepata RAIS ambaye ameonesha yupo tayari kurekebisha makosa. Na kwa bahati nzuri hata wanaCCM wengi wameonesha kumuunga mkono.
Kwa mwanasiasa mwenye akili (au SMART) kama anavyoita Tundu Lissu hii ni best opportunity kulleta hoja bungeni ya kupangua ujinga wote walioufanya akina Lowasa, Mkapa, Kikwete, Chenge, Sumaye na wenzao, ili TAIFA lipate KUPONA.
Kabisa hii ni nafasi ya pekee kwa lisu,ugonvi wa kisiasa aache, kama serikali inadema yeye alete mswada mezani kisha tumuone anaepinga.
 
Sio rahisi Nyani kuyaeleea haya mambo, sheria za madini hazikutungwa leo! Do your homework
 
Sawa, lakini...kama sheria ya madini ni mbaya na hailindi maslahi yetu kwa nini hao wabunge wasiibadilishe?

Kwani ni nani hutunga sheria nchi hii? Rais au bunge?
Mkuu hivi unatarajia mbunge wa upinzani alete mapendekezo yanayoonesha udhaifu wa sheria, halafu wabunge wa ccm waumge mkono?
Si tumeona jinsi serikali inavyowaita wabunge wa ccm na kuweka misimamo?
Serikali inatakiwa kuwasilisha mabadiliko hayo bungeni. Tusisubiri msonobari kudodosha maembe.
 
Sawa, lakini...kama sheria ya madini ni mbaya na hailindi maslahi yetu kwa nini hao wabunge wasiibadilishe?

Kwani ni nani hutunga sheria nchi hii? Rais au bunge?
Unajua kuna sheria ilitungwa na bunge kuhusu makampuni ya madini kujiorodhesha DSE?Tokea imetiwa saini na kikwete mpaka leo hakuna utekelezaji!
Kuweka mikataba wazi nayo inahitaji wabunge?Hawajui chochote kuhusu mikataba hiyo maana ni siri,kwanini inafanywa siri??
 
Back
Top Bottom