Sheria ya Pasu Kwa Pasu ifutwe Kwa Hoja zifuatazo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
SHERIA YA PASU KWA PASU IFUTWE KWA HOJA ZIFUATAZO:

Anaandika, Robert Heriel

Kwa Dunia ya Haki Sawa hiyo sheria haijakaa vizuri Kabisa, Kwa Dunia hii yenye utapeli, dhulma, ubinafsi na Unyonyaji; sheria hiyo ipo haja ya kuipitia vinginevyo kizazi kijacho kitajikuta katika mazingira magumu sana.

Hiyo sheria haitendi HAKI Kwa namna moja ama nyingine, Kwa ufahamu wangu mdogo sheria zinatungwa ili kulinda Haki Fulani. Sheria inayotungwa kutetea HAKI ya MTU mmoja na kusigina Haki ya mtu mwingine sheria hiyo ni kandamizi.

Leo tujadili dhana au sheria ya pasu Kwa pasu katika kugawana Mali hasa Baada ya kuachana.

"Ooooh! Walichuma Mali pamoja" nini maana ya kuchuma Mali pamoja?
Hata mchume Mali pamoja au mfanye Jambo Kwa pamoja lazima kuna mmoja amefanya ziada, hiyo ipo popote pale katika uzalishaji.

Katika Kanuni za uzalishaji na malipo, anayezalisha zaidi ndiye anastahili kulipwa au kupewa zaidi. Hata kama wazalishaji mlikuwa wengi hiyo ni kanuni ya kiuchumi.

Kusema MKE na Mume ATI Kwa vile walizalisha Mali pamoja basi siku wakitengana wagawane Pasu Kwa Pasu ni uonevu na dhulma kubwa Kwa mmojawapo Kati Yao. Hiyo ni sheria kandamizi. Na ambayo inatakiwa ifanyiwe marekebisho yenye tija.

Sheria au dhana ya pasu Kwa pasu IFUTWE Kwa sababu zifuatazo;

1. Ni ukandamizaji, udhulumaji, na Unyonyaji. Pasu Kwa Pasu kiaje? Tuache dhulma na ukandamizaji. Kama MKE alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi, kama mume alikuwa mzalishaji Mkuu apewe zaidi.

Huko ndiko tunakoenda bila Shaka.
Kama Ndoa inatalaka ni vizuri iwekwe sheria mapema yenye HAKI na sio sheria za upendeleo. Kila MTU akinunua Mali yoyote anunue Kwa jina lake na aweke kumbukumbu, vielelezo au ushahidi. Mke umenunua Jiko weka Risiti, umenunua nyumba au kiwanja weka Risiti. Siku mkigawana Mali mtendeane Kwa HAKI.

Sheria ya pasu Kwa pasu imeathiri na itaathiri zaidi kizazi hiki na kijacho kwani ni sheria yenye uonevu mkubwa Kwa moja ya wanandoa. Mwanzoni MTU Kwa upofu WA mapenzi hataona tatizo, lakini kadiri migogoro ikianza kujitokeza ndipo ataona ameingia katika shimo Baya.

Ndoa iwe na mkataba kabisa wa maandishi unaoelezea makubaliano ya wanandoa kuanzia jinsi watakavyoishi, namna watakavyolea Watoto, Makosa ambayo hayatavumilika, namna watavyogawana Mali endapo wakitengana, Watoto wataishi kwa nani na kiwango cha Huduma cha kila mmoja wapo Kwa Watoto hao, majina ya Watoto yatoke upande gani" Hivyo yaani.

Mfano, Haiwezekani mtoto alelewe na Mama mwanzo mwisho alafu ATI maamuzi ya jina la mtoto yatoke Kwa Baba kisa alimzaa, huo ni UHUNI. Udhulumaji, ukandamizaji. Mtoto akilelewa na Mama, majina yatoke kwenye Ukoo wa Mama, mfano. Hiyo ndio HAKI. Kama Baba anataka Haki ya jina lake kuitwa Kwa mtoto basi alee mwanaye.

Uonevu, ukandamizaji, dhulma, Unyonyaji n.k ni mambo yakuangaliwa katika mahusiano ya ndoa.

2. Kuondoa Utegemezi na kuongeza uzalishaji katika Nchi. Kila MTU akiwa mzalishaji katika familia, ni wazi kila MTU atachapa kazi ili kujihami na kujidhatiti kikamilifu. Ndani ya familia kila MTU atataka awe na mchango na achangie Mali kwani hizo ndizo zitagawanywa kama itatokea kuachana.
Mambo

Mambo ya Mario pamoja na kuvizia Mali za mwenza wako au kuachana Kwa Makusudi ili upate Mali zisizozako hayatakuwepo.

Kila mmoja atapambana, na hiyo ndio itaitwa Haki Sawa Kwa wote, Sheria za kusema Mwanaume anaowajibu wa kuhudumia familia IFUTWE na isomeke kuwa Wanandoa, yaani Baba na Mama wanayohaki Sawa kuhudumia Familia katika kiwango Sawa.

Au isomeke kuwa, Wanandoa watatimiza majukumu na wajibu wao kulingana na Mkataba na makubaliano Yao waliosaini na kuandikishana Kabla ya Ndoa.

Pasiwe na mkataba wa Generally kama Ile mikataba ya Wakristo, unatakiwa uwe NI mkataba wa maandishi wenye kurasa za kutosha zitakazolinda Haki na Wajibu Wawili hao

Isomeke hivi;
Huu ni mkataba wa Ndoa baina ya Bw. James Dario na Bi. Alice Ndembo.
Mkataba huo upitiwe na wanasheria, usainiwe na wanasheria, kisha kama MTU atafunga ndoa hiyo Kanisani au msikitini au bomani au Mila kule anaenda kuchukua Cheti tuu.

Na sio ati Watu wasiohusika na ndoa yenu Kwa kile kiitwacho sijui Dini, sijui Serikali, au Mapokeo ya utamaduni ati wao ndio wawe na mchango mkubwa katika mkataba wenu.

Mkataba useme kabisa atakayetaka ndoa kuvunjika(atakayevunja mkataba) atawajibika Kwa kiwango gani?

Mfano atakayevunja ndoa Kwa namna yoyote atalipishwa Nusu ya Mali zake. Alafu mkataba ueleze ni mambo gani yatakayovunja ndoa hiyo.

4. Kupunguza hofu na woga Kwa Watu hasa vijana kuingia kwenye Ndoa.
Kuifuta sheria ya ajabu ambayo ni yauonevu, kuwa pasu Kwa pasu, kutachochea Vijana WA kizazi cha leo kuoa zaidi na kuiheshimu Ndoa.

Vijana wengi WA sasa wanaamini ndoa ni Utapeli, ukandamizaji Kwa wanaume, udhulumaji wa Haki zao. Ninawafahamu baadhi ya Watu ambao hawataki kuoa Kwa sababu ya kuogopa migogoro hasa migogoro ya Mali Baada ya kutengana.

Na upo ushahidi WA kesi nyingi Mahakamani kuhusu migogoro ya kugawana Mali na mirathi. Kama taifa kuna haja ya kuzipitia hizi Sheria upya ili kulijenga taifa hili.

Haiwezekani Pesa ya Mwanamke iwe ya Mwanamke, ahudumie kwao na wewe pia uhudumie kwao, tena uhudumie familia yako, alafu bado mkiachana atake mgawane Mali, huo ni UHUNI, Utapeli, dhulma kubwa, na ukandamizaji. Kijana akifikiria hivyo hawezi kuwa na sababu ya kuoa ikiwa Hana uhakika mzuri wa matokeo/hatma yake.

5. Mali itakayogawanywa pasu Kwa pasu iwe Ile iliyonunuliwa na kuchangiwa na kila mmoja pasu Kwa pasu. Mfano, Mlinunua nyumba Milioni 20, kila mmoja akatoa Milioni 10, basi Mali hiyo ni Hali yenu kugawana Nusu Kwa Nusu.

Masuala ya kusema nilitoa mawazo sijui nilishauri hapo hayapo, kama ushauri ungekuwa na nguvu basi kila familia ingekuwa na nyumba na hayo magari. Kushauri ndio kitu gani bhana!
Kama nyumba imenunuliwa milioni Ishirini, alafu Mume akatoa Milioni 6 alafu MKE akatoa milioni 14 basi kama siku mkiachana Nyumba ikauzwa labda milioni 18. Basi MKE atachukua 74% ya mauzo huku Mume akichukua 26% ya mapato. Hiyo ndio inaitwa Haki.
Hapo hajaonewa yeyote.

Tuelewe kuwa Mapenzi na upendo haviongozwi na sheria Ila ndoa lazima iongozwe na Sheria, Kanuni, na taratibu. Hii ni Kwa sababu ndoa ni taasisi, haiongozwi Kwa hisia Bali Akili, na Akili lazima iwekewe sheria, Kanuni, na utaratibu.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
 
Mkuu, kwenye sheria za ndoa nchini Tanzania hakuna 50/50 ila sheria inamlinda mwanamke apewe gawio la mchango wake kwenye ndoa hata kama hakuwa na kazi. Hii ndiyo falsafa ya sheria ya ndoa.

Kama mwanaume unaamka asubuhi, unakuta nguo na chai mezani vimewekwa na unaacha watoto wadogo unarudi unakuta wako salama huo ni mchango wa mwanamke ambao mahakama ni lazima ziuzingatie kwenye mgawanyo wa mali.
 
ZINAZOTUANGUSHA ni mahakama zetu kwa kupindisha sheria. Sheria hajiasema mgawaanyo uwe pasu kwa pasu.

Quite the contrary.

Sheria imesema mali za wanandoa zenye jina la mmoja ni zake yule aliyenunua, na kama mwenzake alichangia uendelezaji na utunzaji yeye anaingizwa kwenye umiliki wa Tenancy in Common, yani kila mtu na shares zake kulingana na mchango wake. Ila tu ikumbukwe kwamba nyumba yenu ya kuishi haitaguswa wakati wa ndoa bila idhini ya mwingine, haijalishi nani anamiliki au ana mchango gani. Mali ya kugawana pasu kwa pasu ni ile ambayo ina umiliki wa pamoja wa majina mawili, mmeipata wakati mmoja, mkiwa tayari ndani ya ndoa, na imetamkwa Joint Tenancy au Joint Occupancy kwenye nyaraka ya umilikishwaji.

That is the crux of the law.
 
ZINAZOTUANGUSHA ni mahakama zetu kwa kupinsiaha sheria. Sheria hajiasema mgawaanyo uwe pasu kwa pasu.

Quite the contrary.

Sheria imesema mali za wanandoa zenye jina la mmoja ni zake yule aliyenunua, na kama mwenzake alichangia uendelezaji na utunzaji yeye anaingizwa kwenye umiliki wa Tenancy in Common, yani kila mtu na shares zake kulingana na mchango wake. Ila tu mjue nyumba yenu ya kuishi haitaguswa wakati wa ndoa bila idhini ya mwingine bila kujali nani ana mchango gani. Mali ya pasu kwa pasu ni ile ambayo ina umiliki wa pamoja wa majina mawili, mmeipata wakati mmoja, ndani ya ndoa, na imetamkwa Joint Tenancy kwenye karatasi ya umilikishwaji.

That is the crux of the law.

Shukrani Mkuu Kwa ufafanuzi.
Ipo haja ya kuweka Mambo Sawa.
Vinginevyo Ipo agenda ya kuiangusha ndoa Kwa mbinu nyingi ikiwemo hizo sheria na mwishowe jamii itaanguka, hasa jamii Maskini.
 
Nafikiri kuna mkanganyiko sana kwenye sheria za mahakama
Ila kwa upande mwingine dini zinasaidia pia kwa kugawa Mirathi
Ingawa zinatofautiana
 
Kenya wameamua
Screenshot_20230128_150151_Google.jpg
 
Back
Top Bottom