Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

McCarthy,
Umequote post yangu inayohusu ndoa za kimila na sio presumption of marriage. Anyway presumption of marriage ipo kisheria, na si utashi wako, wangu, au utashi wa mahakama. NI SHERIA ! The law is the law, hadi bunge litakapoibadilisha. Na sheria hiyo ipo wazi, 1.) Wawe wameishi PAMOJA (paa moja) kwa muda wa miaka miwili (siku 730) au zaidi.

Unaishije pamoja na mtu aliye marekani wakati wewe upo Sengerema, na katika hizo siku 730 mmeona labda kwa siku moja au mbili tu? Huyo mtu utakuwa umeishi nae kwa siku 730 kama sheria inavyotaka? Kwa kigezo cha simu na teknolojia unafahamu kwamba kuna watu watakuwa na wake 100 hadi 200? Sasa kwa mkristu kuwa na wake 100 au 200 si ni kinyume cha sheria? Sasa sheria inawezaje kujipinga yenyewe, thats illegal!, au kuna sheria mpya mahakama imejitungia? Kwamba mwaka 1971 kulikuwa hakuna barua?

Mtu alikuwa hawezi kumwandikia barua mpenzi wake aliye marekani akaambatanisha na picha, hapakuwa na simu za mezani, toka 1940's watu wanapigiana simu itakuwa 1971?! Hoja dhaifu sana hiyo na haina mashiko, na kama kuna mahakama iliamua hivyo basi kata rufaa na uwashinde kwa hoja, tena ukizingatia ushahidi wa kielektroniki huwa haukubalika mahakamani kirahisi, maana mtu anaweza akatengeneza kwa photoshop screenshoot ya mawasiliano ya watu wawili nanikaonekana yalikuwa ni mawasiliano halisi kabisa..., imagine hata video ya Gwajima aliweza kuikana, itakuwa text messages na voice call?!

2.) Wawe wameishi kama mume na mke. Mahakamani kinachohitajika ni udhibitisho. Hao majirani wanatakiwa wadhibitishe kwamba wahusika wameishi pamoja kwa siku 730 na si 729 au chini ya hapo, that is the law, how? Hiyo ni kazi yao kudhibitisha sio ya mahakama. Pia wadhibitishe kwamba wahusika waliishi kama mume na mke sio kama kaka na dada au mwenye nyumba na house girl wake, how? Hiyo sio kazi ya mahakama, ni kazi ya washuhuda kudhibitisha. Sheria ni sheria hadi bunge itakapoibadilisha.
Soma post yangu na 7 kwa ufafanuzi zaidi.
 
Katika harakat za kuhama nyumba nime poteza vyeti vya ndoa(christian marriage). Utaratib ukoje, kuna namna ya kuvipata tena upya?
 
Mbona imesha rekebishwa muda tuu mkuu mwambie apitie kifungu cha 126 cha sheria ya ndoa imetoa exceptions katika mazingira gan yataangaliwa either kwa mama au baba ku custody mtoto even if yuko chin ya miaka 7 asome pamoja 125 ya sheria tajwa hapo juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisani mnaapa "Hadi kifo kiwatenganishe" maana kanisa likifunga ndoa haliwezi kuwaachanisha ila mahakama inaweza kuwatenganisha sio kuwaachanisha. Ndio maana pamoja na kuachana siku zote mke aliyeachika bado atapewa heshima yake maana kifo bado hakijawatenganisha.
Habarin, ningependa kujua kwa nini ndoa ifanyike kanisani lakin kwenye kutalakiana mnaeenda mahakamani na sio kanisa mlipo funga ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu naombeni kuuliza eti ikiwa hakimu wa mahakama ya mwanzo aliweka saini kwenye wosia kama shahidi anaweza kuja kusikiliza shauri linalohusu wosia huo hapo baadae mtoa wosia akifariki?
 
Samahan kaka mfano mm mke wangu anataka talaka na tunanyumba ambayo nilikopa pesa benki na kuweka dhamana ya mshahara maana mm ni mtumishi je nikiachana nae nyumba inaweza kiuzwa tukagawana au anaweza kuambiwa abaki kwenye nyumba mimi niondoke na mkopo bado haujaisha wananikata mshahara wangu na anawatoto wadogo.
 
Niliachana na mwanamke, ndoa ikavunjwa mahakamani, vyeti bado tunavyo

Mwenzangu anakitumia kwa masuala mbalimbali kazini kwake

Je, kuna tatizo lolote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini wanajamvi!! Niliishi na mwanamke kwa miaka minne bila kufunga ndoa rasmi japo nilimtolea mahari na tuna watoto wawili, baada ya muda ikatokea kutoelewana akarudi kwao baada ya muda akaenda kuishi na mwanaume mwingine na huko ameshazaa watoto watatu na huu ni mwaka wa nne tangu aanze kuishi na huyo mwanaume. Watoto wangu niliwachukua naishi nao mwenyewe.
Swali langu ni:-
1. Je, sheria inasema nini juu ya mali zilizopatikana tukiwa pamoja?
2. Je, ana haki kuja kudai mgao wa mali hizo kisheria?
 
Habarini wanajamvi!! Niliishi na mwanamke kwa miaka minne bila kufunga ndoa rasmi japo nilimtolea mahari na tuna watoto wawili, baada ya muda ikatokea kutoelewana akarudi kwao baada ya muda akaenda kuishi na mwanaume mwingine na huko ameshazaa watoto watatu na huu ni mwaka wa nne tangu aanze kuishi na huyo mwanaume. Watoto wangu niliwachukua naishi nao mwenyewe.
Swali langu ni:-
1. Je, sheria inasema nini juu ya mali zilizopatikana tukiwa pamoja?
2. Je, ana haki kuja kudai mgao wa mali hizo kisheria?
1. Sheria inatambua mali zilizo chumwa na mme na mwanamke kwa kuishi pamoja chini ya dhana ya Ndoa (presumption of marriage) na sheria inawapa watu hao haki ya mgao na haki zingine zote watu wanazoweza pata wale walio oana wafikishana napo Mahakamani ispokua talaka. Hivyo watu wanaoishi pamoja bila kuoana na kuchuma mali kipindi wanaishi pamoja sheria inatambua Mali hizo ni za pamoja na zinastahili mgao kwa mujibu wa sheria. Rejea kifungu Cha 160 cha Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971
2. Anayo haki ya Kudai Mgao kwa Mujibu wa Sheria ya Ndoa Kifungu icho hapo juu.
Kifungu icho kilitungwa kulinda Maslahi na Haki ya watu wanaoishi pamoja na kupata mali angali kua hawajaoana.
 
Samahan kaka mfano mm mke wangu anataka talaka na tunanyumba ambayo nilikopa pesa benki na kuweka dhamana ya mshahara maana mm ni mtumishi je nikiachana nae nyumba inaweza kiuzwa tukagawana au anaweza kuambiwa abaki kwenye nyumba mimi niondoke na mkopo bado haujaisha wananikata mshahara wangu na anawatoto wadogo.
Kwa Kadri ya Uzoefu na Uelewa Wangu:
Mkiachana atapata Mgao kutoka Katika Hiyo Nyumba kwani Mwanamke ambae ni mkeo Mchango wake Katika Upatikanaji wa Mali hiyo Kazi zake Nyumbani (Domestic Works) zinahesabiwa kama Ni mchango wake Kuna Kesi ya Bi Hawa iliamua hili vizuri. Hivyo kwenye namna alivyochangia Hadi wewe ukapata mkopo na Kujenga Nyumba hiyo Mchango wake ni Kazi za nyumbani.
Hauwezi kuambiwa uondoke that iz not Law, ila mtagwana kwa kiwango ambacho kila mmoja alichangia Mfano ikionekana wewe ulichangia 70% kwenye Kupata Nyumba nae 30% basi wewe waweza takiwa umpe fidia ya hiyo 30% ya Thamani ya Nyumba ubakie na nyumba na ukishindwa aweza ambiwa akupe wewe hiyo 70% abaki na Nyumba ikishindikana Nyumba yaweza uzwa na Mgawane kila mtu kwa kadri ya aslimia yake.
 
wakuu naombeni kuuliza eti ikiwa hakimu wa mahakama ya mwanzo aliweka saini kwenye wosia kama shahidi anaweza kuja kusikiliza shauri linalohusu wosia huo hapo baadae mtoa wosia akifariki?
Kwa Mtazamo wangu:
1. Anaweza Kusikiliza endapo patakua hakuna Ubishi juu ya Wosia huo. Hapa ni kusema hakuna ubishani ya nini kilichopo ndani ya Wosia Huo yaani WOSIA unakubaliwa kama ulivyo.

2. Hawezi Kusikiliza. Endapo kuna Ubishi juu ya Wosia huo, yaani watu wanabishana juu ya Kilichomo kwenye wosia basi ni vizuri asisikilize kwani ni Kinnyume cha Maadili ya Kazi yake (Judicial Code of Ethics). Maadili ya Kazi yake yanakataza Kuaamua Kesi yako mwenye, Kusikiliza jambo ulilokua umeshalisikliza hata nusu yake n.k
 
Mwanamke anapomlazimisha mumewe ampe talaka,je mwanamke huyu atakuwa na haki katika kugawana mali?

Iko ivi,walioana na walifanikiwa kujenga, bahati mbaya mume amepata maradhi na anasumbuliwa na kifua.

Ndugu wa mwanaume wakamchukua kwaajili ya matibabu maana ugonjwa anaoumwa unahitaji uangalizi na huduma.

Mke alibaki nyumbani na huko,akaanza kutoka na wanaume kadhaa,baada ya muda anamfata mumewe kwa shari na kumtaka ampe talaka.

Mume bado anampenda mkewe,ila mke anataka talaka bila kuwa na sababu.

Je hamna sheria ya kumlinda mwanaume?

Nawasilisha....
#mchango wenu ni wa muhimu.
 
Pamoja na kumpenda, kwahio ashakubari kumpa talaka na kuachana? Suala uliloleta hapa ni Mgawanyo wa mali tuu si ndio?

Hembu iweke hii ieleweke. Sio watu wanajadili ushauri wa Talaka na Mali.

Yeye anawaza kurumrudisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom