Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Ok mfano nimeenda soth africa na nikaoa huko, nikaja nae tukaishi Tanzania, mali zangu zipo Tanzania na South Africa.

Nimemuoa nikiwa na mali ya tsh milioni kumi.
Namuacha nikiwa na mali ya tsh bilioni kumi.
Alikuwa housewife.

Tukiachana hapi inakuwaje?
Nipatie kamuda hadi kesho au thereafter!
 
The Boss,
The Boss, haijalishi mali hizo ziko nchi gani, ni suala la contribution ya kila mmoja katika mali ya familia (matrimonial property). Pia haijalishi kama alikuwa housewife, rejea Post #04 hapo juu kuhusu Kesi maarufu ya Bi Hawa Mohamed v. Ally Seif.

Na kama mlioana mkiwa South Africa, then mkahamia Tanzania, bila shaka uraia ni wa Tanzania, then Sheria za Tanzania zitatumika. Kama mmehamia Tanzania moja kwa moja ina maana mtakuwa mme-settle suala la mali zenu huko South Africa.

Kwa kifupi, hiyo TSh 10m/- itategemea kwamba yeye mke amechangia kiasi gani na mume amechangia kiasi gani, pia usisahau suala la maintenance (ambalo halijalishi kama kulikuwa na contribution au la), pamoja na utunzaji wa watoto kama wapo, madeni kama yapo, nk! Kila kesi ina merits zake, kulingana na circumstances!
 
Na sheria yetu ya talaka ina semaje kuhusu
pre-nuptial agreements

hili swali halikujibiwa, au? Nimeshtushwa sana leo hii na habari hii ya Uingereza.
Lottery Winner Forced To Pay Ex-Wife £2m

3:46pm UK, Monday November 22, 2010


Jenny Wotherspoon, Sky News Online
A £56m lottery winner has been forced to pay a chunk of his jackpot to his ex-wife who walked out on him 10 years ago for another man.



15621515.jpg
Nigel Page with his second wife Justine



Euromillions winner Nigel Page agreed to give his former partner £2m in an out-of-court settlement, after she tried to sue him for four times as much.
According to The Sun newspaper, Mr Page had an earlier offer of £1m turned down.
The settlement fee awarded to 43-year-old Wendy is thought to be the first time a former partner has recieved a pay-out from a UK lottery winner.
Divorce lawyer Vanessa Lloyd Platt said there are two reasons Mr Page may have been obliged to settle.
"It's likely to be that the couple had a split settlement or that he was paying ongoing maintenance.

What people don't realise is that if you're paying ongoing maintanence and you get a windfall, your ex can always go back and claim some of that money.
 
Mimi sidhani kama mambo ya pre-nup yapo kwenye sheria za ndoa za Tanzania lakini sina hakika sana. Kama kuna wanaojua watuwekee hivyo vipengele hapa.
 
Wadau wa sheria, 'ngoja ngoja huumiza matumbo!'
Kuna kipendele chochote kinachoweza kulinda mali za mume/mke?
Binaadamu hawaaminiki tena.
 
This is a very useful thread. I would like to know what happens in the scenario i will describe shortly:

a friend of mine was married. unfortunately his wife left him for another man leaving him to take care of their 9months old daughter. the wife came demanding for a divorce and the guy refused because he wanted to screw her life too. unfortunately, 3 years later, he met and decided to marry another woman. this time , his ex wife refused to sign the divorce papers. how can he get out of this mess?

I will greatly appreciate your answers.
 
arinaswi,

Dah! Huyo mwanamama alikuwa 'nje ya ndoa' kwa miaka mitatu halafu hataki ku sign divorce papers?
sheria ya kiserikali inasemaje?
 
Salaam wana jamvi...

mimi ni mgeni sana humu ndani, nimevutiwa na mambo mengi sana ambayo kwa kiasi fulani yanaelimisha na yanafunua upeo fulani.

NAomba kuuliza swali ambalo siku zote huwa najiuliza sipati jibu au labda sina ufahamu nalo na wengine huenda wakawa na jibu.

NAuliza hivi?

Tunapofunga Ndoa (mimi ni muislamu) tunafungishwa Ndoa na Sheikh na ili Ndoa iwe sahihi kwa misingi ya dini ya kiislamu, lazima kuwe na walii (yaani mtoa idhini ya kuoza) baba na wengine ambao wameelezewa katika sharia' ya Ndoa , na pasipo walii au muozeshaji , muoa na muolewa basi Ndoa ile ni batili. Wakati Ndoa inapofungwa HAKUNA JAJI , WALA MTU YEYOTE KUTOKA SERIKALINI zaidi ya kitabu ambacho baada ya muda hupelekwa kusajiliwa kwenye daftarila uzazi na vifo. na serikali huikubali Ndoa hiyo kinaga ubaga. swali langu linakuja.

Kama Ndoa hii ilifungwa kwa misingi ya kiislamu, na serikali ikaikubali ni Ndoa, je?

KWANINI MWANAMME WA KIISLAMU ANAPOMUACHA MWANAMKE WA KIISLAMU KUTOKANA NA NDOA HIYO HIYO AMBAYO ILIFUNGWA KWA MISINGI YA KIISLAMU NA SERIKALI IKAKUBALI NDOA ILE PASINA NA MUWAKILISHI YEYOTE KUTOKA SERIKALINI KUTOKUWEPO INAPOFIKIA KUTOA TALAKA SERIKALI INASEMA HAIITAMBUI TALAKA ILE MPAKA UPATE YA MAHAKAMANI????! Au

KWANINI MWANAMKE ANAAPOOMBA TALAKA kwa mwanaume anaambiwa aanze kwanza BAKWATA, na anapokwenda BAKWATA na BAKWATA wakajiridhisha kuwa sababu zote za kuivunja Ndoa ile zipo basi wao hutoa maelekezo kwa MAHAKAMA kuivunja NDOA ILE ! hapa mwanamke kupata shida sana , anapoenda mahakamani ! nenda rudi, ... mwanaume anaruhusiwa kuoa hata kama hajamuacha yule mwanamke lakini mwanamke haruhusiwi kuolewa mpaka apate hiyo talaka ya MAHAKAMA!

Kwa sheria ya Kiislamu, NDOA HAIWEZI KUVUNJWA MPAKA IVUNJWE NA QADHI ! ndio maana BAKWATA kwasabau kuna MUFTI ambae hana cheo cha QADHI hana mamlaka kisharia kuvunja Ndoa ile. !

Sasa mimi naomba niulize ! kwanini SERIKALI IKUBALI NDOA ILE AMBAYO IMEFUNGWA KIISLAMU BILA WAO KUWEPO? NA AT THE SAME TIME IKATAE TALAKA INAYOTOLEWA NA MUME KISHERIA YA KIISLAMU AMBAYO IMERUHUSU KAMA ILIVORUHU KWENYE NDOA ! je hapa hakuna mapungufu kweli.

Na hata kama muem atatoa talaka BAKWATA basi huku nje utaambiwa serikali haitambui!

Jamani sina nia mbaya! nauliza tu napenda kujua, na kama kuna watu wa kurekebisha sheria basi hili na talaka nadhani liwekwe ili kama mtu akipewa talaka serikali ikubali na tusiambiwe kuwa serikali haitambui talaka ya mume mpaka mahakamani!

Mimi sijui sharia naomba nijuzwe..

Salaam

 
Kaka ndoa ni private institution ambayo the state has got interest in it as it is the one which creates family then clan and finally the state. It is the source of the citizens.....being so it is in the interest of the state to regulate it
 
waislam wanawake mnapenda kuachwa? haya endeleeni kukaa kwenye hiyo dini ya uonevu.
 
Yaani kwa kuwa ukimzaa mtoto wako serikali inamtambua basi unataka ukimuua serikali itambue mauaji au?
 
Jamani, baadhi ya wachangiaji hamjamsaidia mleta hoja. Badala yake mmemshambulia. Hilo linanifanya niamini kuwa baadhi ya waliojitokeza kumsaidia mleta hoja si wanasheria, maana wlichokifanya si sehemu ya utamaduni wa wanasheria...anyway, kama alivyochangia msomi mmoja ha juu, ndugu yangu ni muhimu uelewe kwamba serikali ina maslahi makubwa ktk muunganiko wa mtu mme na mtu mke, maana huko hutokea watoto na mali, na masuala mengine yenye manufaa kwa jamii nzima!
 
Jamani, baadhi ya wachangiaji hamjamsaidia mleta hoja. Badala yake mmemshambulia. Hilo linanifanya niamini kuwa baadhi ya waliojitokeza kumsaidia mleta hoja si wanasheria, maana wlichokifanya si sehemu ya utamaduni wa wanasheria...anyway, kama alivyochangia msomi mmoja ha juu, ndugu yangu ni muhimu uelewe kwamba serikali ina maslahi makubwa ktk muunganiko wa mtu mme na mtu mke, maana huko hutokea watoto na mali, na masuala mengine yenye manufaa kwa jamii nzima!

Umenisaidia, unajua ukisoma post nyingi humu jf ni kuwa kuna chuki kubwa juu ya dini! yaani mtu hata kama kile kitu kinamsaidia yeye atapinga mradi tu mtu aloleta mada sio wa dini yake! sijui tunaelelekea wapi! ninachotaka kusaidia kingine nadhani serikali inapaswa kurekebisha sheria zake katika katiba ili hiki kitu kieleweke! wanwake wengine wanateseka kwa mtindo huu.

mwanamke kama hajaachwa na mume HAWEZI KUOLEWA mpaka apate talaka! kidini ! talaka ni ile inayotolewa na mume au Qadhi! na Talaka ya serikali HAIKUBALIWI kidini! umeona hapa!

Hii humfanya mwanamke akae akisubiri apewe talaka ili aweze kuolewa tena au aendelee na maisha yake! huku mwanamme yeye ameruhusiw3a kuoa! mwanaume huoa na mwanamke hukaa akisubiria ! mpaka lini? nilikuwa najaribu kuangalia serikali inamsaidia vipi mwanamke kama huyu? lakini unapewa majibu ya ajabu ajabu! sikui kunyonga kumekuja vipi? acheni chuki
 
Jamani, baadhi ya wachangiaji hamjamsaidia mleta hoja. Badala yake mmemshambulia. Hilo linanifanya niamini kuwa baadhi ya waliojitokeza kumsaidia mleta hoja si wanasheria, maana wlichokifanya si sehemu ya utamaduni wa wanasheria...anyway, kama alivyochangia msomi mmoja ha juu, ndugu yangu ni muhimu uelewe kwamba serikali ina maslahi makubwa ktk muunganiko wa mtu mme na mtu mke, maana huko hutokea watoto na mali, na masuala mengine yenye manufaa kwa jamii nzima!

Reading btn the lines, swali lake linamaana tofauti na mineno miiingi aliyoandika hapa. Kuna kitu analenga. Think hard, utagundua ni nini anataka kutushirikisha.
 
Reading btn the lines, swali lake linamaana tofauti na mineno miiingi aliyoandika hapa. Kuna kitu analenga. Think hard, utagundua ni nini anataka kutushirikisha.

Kweli mkuu,
Hata mimi nimeisoma nikaona anaji-mix sana...she's meaning something behind the curtain...

Ila kama kweli anahitaji msaada basi aweke wazi jamvini tuu.
 
Kabla sijajibu swali lako napenda ufahamu kwanza mambo ya msingi kuhusu talaka km yalivoainishwa ndani ya law of marriage Act,1971.

Napenda kukufahamisha kuwa serikali inatambua talaka za kiislamu isipokuwa ili talaka itolewe hata kama ni kwa misingi ya dini ya kiislamu lazima hatua kadhaa zifuatwe na hii haijalishi hata kama ni kwa wakristo.(ingawaje wakristo wanaamini wao hakuna talaka ni mke mmoja na mume mmoja mpk kifo-kwao marriage is an indisoluble sacrament and what god has joined no man can put asunder..so kanisa haliwezi kutoa talaka ila technically mnaweza achana.

1.Kwa mfano,talaka haitolewi mpaka mahakama ijiridhishe kuwa ndoa imevunjika beyond repair yani hairekebishiki..irreparably broken.

2.ili kujiridhisha kuwa ndoa imevunjika beynd repair sheria inataka kabla hamjaenda mahakamani mpitie kwanza marriage reconciliatory boards-yani mabaraza ya usuluhisi...hapa ndipo unakuta bakwata,makanisa,na ustawi wa jamii na seyrikali za mitaa wanahusika..kwa hiyo siyo kweli kuwa ni nyinyi tu lazima mpitie bakwata hata wakristo lazma wapitie mabaraza.wao wanawasuluhisha na wakishindwa ndio wanawapa hati ya maandishi ambayo itaonesha wameshindwa kuwasuluhisha.

3.mkitoka hapo mnaenda mahakamani na huko mahakama itaangalia sababu za kutaka talaka kwa mujibu wa sheria section 107(2)mfano zinaa,ukatili nk na pia lazima ijiridhishe pamoja nakuwepo kwa hayo mambo ndoa yenu imeharibika beyond repair.

4.sasa suala lako la talaka kwa mujibu wa kiislam mahakama inatambua kwa mfano mi si muislamu ila najua kuna talaka ila,khului,nk isipokuwa ili ziwe valid pia bado hizo hatua zinatakiwa zifuatwe.

Interestingly,hiyo talaka khului mwanamke wa kiislam anaweza kujiredeem yani kurudisha mahari na kujinasua kutoka kwny ndoa (talaka) yeye mwenyewe,(mnaita kujikhului)na kuna kesi ninaifahamu mahakama imetambua talaka hiyo.

So sio kweli serikali haitambui talaka za kiislamu la hasha bali mnatakiwa kufuata procedure zilizowekwa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971,ambayo ni sura ya 29 ya sheria zetu!
Ni hayo tu kwa sasa
 
Mimi nilikuwa na mwanamke naishi naye nimeishi naye kwa zaidi ya miaka minne sikuwahi kufunga naye ndoa wala sikumtolea mahali,nimezaa naye watoto wawili sasa tumehitilafiana naye akabeba kila kitu ndani mwangu akaondoka navyo pamja na watoto na kuhamia kwa mwanamme mwingine.vitu wanavyotumia nivya kwangu je?nina haki ya kwenda kumyangaya vile vitu?naomba msaada wa kisheria kifungu kwa kifungu
 
Nenda WLAC au NOLA hapo utapata msaada mzuri wa kisheria japo sijajua uko mkoani au wilayani. Wanasheria watakufafanulia ufanyeje kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971
 
Mi niko dar.lakini kuna mtu aliniambia mwanamke ukiishi naye kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mkeo na anahaki ya mali uliyonayo sasa je?nayeye anahaki ya kuchukua mali yangu na kwenda kuitumia na mwanamke mwingine ok ntakwenda huko uliko nielekeza kaka
 
Back
Top Bottom