Sheria ya Mafao miaka 55, wafanyakazi wamehusishwa?

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Serikali imepitisha sheria rasmi kuwa hakuna mtumishi yeyote anaeweza kuchukua mafao yake katika mfuko wowote wa pensheni mpaka tu afikie umri wa kustaafu miaka 55 kwa hiari au 60 kwa lazima.

Uamuzi huu unazua maswali yafuatayo:-

1. Je, mdau wa kwanza katika hili ambaye ni mfanyakazi amehusishwa katika maamuzi haya?
2. Je, Mifuko hii ya Pensheni itaongeza riba katika michango? maana ikumbukwe kuwa thamani ya milioni moja ya leo si sawa na milioni moja baada ya miaka 10 ijayo.
3. Iwapo mtumishi hahitaji tena kuajiriwa na kuchangia katika mfuko, kwanini pesa hii asipewe afanyie kazi anazozijua mwenyewe za kimaendeleo?
4. Kwanini serikali inawakumbuka wananchi pale tu inapohitaji jasho la wananchi?
5. Kwanini serikali impangie mtu binafsi mahitaji yake?
6. Uwezo wa kutumia mafao haya kujipatia mkopo wa nyumba ni kweli au changa la macho?

Majibu mengi yanahitajika katika hili kuweza kuwasaidia wafanyakazi kujua nini faida na hasara za kusubiri hadi umri wa kustaafu ndipo mfanyakazi aweze kuchukua mafao yake.
 
Serikali imepitisha sheria rasmi kuwa hakuna mtumishi yeyote anaeweza kuchukua mafao yake katika mfuko wowote wa pensheni mpaka tu afikie umri wa kustaafu miaka 55 kwa hiari au 60 kwa lazima.

3. Iwapo mtumishi hahitaji tena kuajiriwa na kuchangia katika mfuko, kwanini pesa hii asipewe afanyie kazi anazozijua mwenyewe za kimaendeleo?

Majibu mengi yanahitajika katika hili kuweza kuwasaidia wafanyakazi kujua nini faida na hasara za kusubiri hadi umri wa kustaafu ndipo mfanyakazi aweze kuchukua mafao yake.

Nitaishangaa sana serekali kama kweli mtu akiachishwa/akiacha kazi hatoruhusiwa kuchukua kilicho chake...
 
Kwa nini wanakiuka mikataba ya awali? Au fedha ndiyo zimeliwa na wanataka wafanyakazi wawe wanapokea kidogokidogo kama pensheni kuliko mkupuo.
 
Haya ni ya miaka mitatu tu ijayo...Waziri mtarajiwa nitalifuta hili , pale mwaka 2015 tukiingia madarakani. Wafanyakazi jipeni moyo mkombozi naingia Mjengoni 2015. safu mpya ikiongozwa na waziri mkuu......(wadau mtajeniiiiiiiiiiiiiiii)
 
Kinachonishangaza SHERIA huwa haitungwi RETROSEPECTIVELY. Lakini serikali hii inacheza double standards.

Mikataba ya wali ni kwamba ukiacha kazi basi unalipwa chako unaondoka. Lakini sheria hii sasa inakataza kwamba mpaka ufikishe miaka 55 au 60 kinyume na mikataba ya awali.

Sasa uone kwanini serikali inacheza double standards, katika sheria hii wafanyakazi WAPYA wameruhusiwa kuchagua mifuko wanayotaka eg NSSF, PPF, LAPF, PSPF etc. Lakini wafanyakazi wa zamani tumekatazwa kuchagua mifuko kwasababu ya mikataba yetu ya awali.

Hii ndiyo DOUBLE STANDARD. Kwenye mafao sheria haizingatii mikataba ya awali. Lakini kwenye kuhama mifuko SHERIA inasema tuzingatie mikataba ya awali.

Haya ndiyo matatizo ya kuwa na AG dizaini ya akina Werema wanaodhani KICHWA NI KWAAJILI YA KUOTESHA NYWELE NA WALA SIO KUFIKIRI.
 
Mkataba wa NSSF niliyosaini hausemi nilipwe fedha baada ya miaka 55. Mkataba unasema nilipwe fedha wakati wowote kama nikiacha kazi. Kubadili sheria ili mkataba huu ufe ni aina fulani ya uwenda wazimu. Kwanza fedha ninayoweka riba yake ni ndogo sana. Sasa kama mimi naweka fedha kwa ajili ya kuongeza mtaji hii ina maana kwamba matarajio yangu yote yatakuwa yamekufa.
Na kwa nini tusishirikishwe? Kwa nini waamue wenyewe tu? Hivi wamelewa madaraka siyo? Sikubaliani wabadili sheria.
 
Mlangaja Ukidai kwanini hatukushirikishwi? ni utetezi DHAIFU. UKWELI ni kwamba wafanyakazi tulishirikishwa kwanza kupitia TUCTA na pili wafanyakazi tulishirikishwa kupitia wawakilishi wetu ambao ni WABUNGE wa JMT.
 
Hivi unategemea Mwigulu angekusaidia?. Hatujashirikishwa.
 
hivi umri wa mtanzania kuishi ni miaka mingapi???? huenda wamecheza na hii kitu!
 
Pesa zetu zinaandaliwa kugharimia uchaguzi mkuu mwaka 2015. Haiingii akilini hata siku moja serikali kutumia kigezo cha kufikisha umri wa kustaafu wakati waTZ tunakufa hata kabla haujafikia umri huo kutokana na maisha duni ya kila siku!
 
Hapa ndipo nafikaga mahali najiuliza hivi hii nchi inaongozwa na binadamu? au mashetani yaliyojificha
kwenye miili ya binadamu?hivi kweli watu wenye mioyo ya ubinadamu wanaweza kukaa na kupitisha
kitu kama hiki bila kuwaza maumivu watakayoyapata watanzania kwa maamuzi yao ya kishetani kiasi
hiki!!!huu ni wizi wa mchana kweupe,wanaendelea kukopeshana pesa za mifuko hii,hivyo wanaona
ili ziwe nyingi wazuie tusichukue,hivi leo hii mtu ameacha au kuachiswa kazi na hataki kuendelea
kuajiriwa anataka kujiajiri unamwambia asubiri afikishe miaka 55,kweli inaingia akilini? "Mungu ikumbuke
hii nchi tuhurumie watanzania tupe ujasiri wa kukataa udhalimu huu tunaofanyiwa"
 
-Serikali imejikopesha mabilioni kutoka mifuko hii hawajarejesha na inaelekea hawana mpango wa kufanya hivyo...
-Mifuko hii imejiingiza kwenye miradi mingi ya kifisadi kwa mabilioni na kuishia kula hasara...

Sasa hali imekuwa mbaya Serikali inatafuta pa kutokea kwa kudhibiti wafanyakazi wasichukue pesa zao pale wanapotaka!!

Hii kitu inaweza kuleta mtafaruku mkubwa sana serikali isipokuwa makini...
 
Jamani, kwani hii tayari imeshapitishwa kuwa sheria. Mbona hatujasikia hata ikijadiliwa bungeni au kuna baadhi ya sheria hazipiti bungeni????????
 
Tunahitaji technolojia ya Wapalestina. Zile rocket.
Jamani hatuna Serikali!! Bahati mbaya kabisa, Wabunge wa CCM nao wamekuwa ni viongozi wa serikali. Ni kupiga makofi, makofi kwa mawaziri.
 
Serikali imepitisha sheria rasmi kuwa hakuna mtumishi yeyote anaeweza kuchukua mafao yake katika mfuko wowote wa pensheni mpaka tu afikie umri wa kustaafu miaka 55 kwa hiari au 60 kwa lazima.

Mtumishi ni nani. Maana hii term ni Civil Servant. Wakati kama uko private sector huitwi Civil Servant bali unaitwa employee. Tafakari.
 
Mlangaja Ukidai kwanini hatukushirikishwi? ni utetezi DHAIFU. UKWELI ni kwamba wafanyakazi tulishirikishwa kwanza kupitia TUCTA na pili wafanyakazi tulishirikishwa kupitia wawakilishi wetu ambao ni WABUNGE wa JMT.
Hivi unategemea Mwigulu angekusaidia?. Hatujashirikishwa.
hapo ndio matatizo yetu yalipojikita na wengi wetu hatujui kuwa udhaifu wa serikali ni matokeo ya udhaifu wetu.

Life expectancy ya Mtz now ni kati ya miaka 45-50 sasa unaposema miaka 55 sijui unafikiria Waingereza!

Tunawaona hawa wakuu wa taasisi na wawakilishi wengine kama watu 'waliojaliwa' kupata ulaji huo, liti tungelijua kuwa maamuzi na porojo zao ndio umasikini wetu ndio tungelijua kuwa kati ya Tundu Lissu na Mh. Werema ni nani mwenye "kichwa chake ni nyenzo ya kufikiri au mahala pa kuoteshea nywele"!

Na bado tutaona zaidi ya haya.

How about wabunge, je watachukua pension baada ya bunge kuvunjwa (miaka mitano), au watasubiri umri huo pia?
 
Ilitakiwa baada ya makubaliano, tuvunje mikataba na hii mifuko ya kijamii, tulipwe fedha zetu halafu ndio tukubaliane kusaini mikataba mipya inayosema miaka 55 nk.....
 
Back
Top Bottom