Sheria ya Mafao miaka 55, wafanyakazi wamehusishwa?

katika hili nimebakwa......!!!! tena mchana kweupeeee.....!!!!!!

serikali inasisitiza watu tujiajiri huku haitaki kutupa mafao yetu! ok! nimegundua serikali inataka tufanye biashara au tujiajiri tukiwa wazee kama Kingunge ngombale mwiru!
 
Hili ni changa la macho, hebu jiulize wewe utakuwa na mafao kiasi gani mpaka ukopeshwe nyumba??? ndugu zangu kila siku mnaabiwa serikali haina pesa, na uchaguzi unakaribia watapata wapi pesa ya uchaguzi 2015??? na safari za nje, posho za vikao????? Watanzania tuamke, wanasema watawapa mikopo ya nyumba, kwani kila mtu tatizo lake ni nyumba????
 
Wakuu naomba Mwongozo,

Mimi nataka kuongea na mwajiri wangu a sipeleke tena Makatao yangu huko NSSF, Hawa jamaa DAWA YAO NI NDOGO SANA WAKIMWAGA MBOGA SISI TUBOMOE KABISA JIKO LA KUPIKIA,

 
Mlangaja Ukidai kwanini hatukushirikishwi? ni utetezi DHAIFU. UKWELI ni kwamba wafanyakazi tulishirikishwa kwanza kupitia TUCTA na pili wafanyakazi tulishirikishwa kupitia wawakilishi wetu ambao ni WABUNGE wa JMT.
Acha hizo wewe wabunge wa magamba a.k.a wagonga meza wanaweza kumshirikisha mtu katika maslahi yao kweli??Think twice!!
 
Hivi kikwete alitoka wapi jamani??? Mbona ni kansa inayotumaliza taratibu??? Uwiiiiii hili shetani litaondoka lini madarakani???
 
Mambo ya nchi hii utata mtupu!

SSRA Wizi mtupu, mafao hadi ufikishe miaka 55 au 60

UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA
MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya
Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili,
2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza
kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini
mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits)
yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa
pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko
atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55)
au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya
nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye
Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza
lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa
mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu
maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.
Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi
pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya
hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia
wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu
tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu
kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena
muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na
Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama
sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha
kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea
haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa
kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama,
kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri
ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa,
mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa
kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la
ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na
fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo
kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda
kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama
yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.
Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la
kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.
 
Mie nimeshafika viwanja vya mnazi mmoja naandamana kupinga, wanapinga njooni tuungane.
 
lazima tuilipuee najua hii ilikuwa ni Agenda iliyofichwa ndo maana wabunge hawakuijadili siri tunazo na lazima mahakamani tuende nipeni siku
 
Hivi kikwete alitoka wapi jamani??? Mbona ni kansa inayotumaliza taratibu??? Uwiiiiii hili shetani litaondoka lini madarakani???

Na hili nalo mnataka kumlaumu mjomba?

Hayo mambo ya SSRA Madame sio JK
 
Hivi kikwete alitoka wapi jamani??? Mbona ni kansa inayotumaliza taratibu??? Uwiiiiii hili shetani litaondoka lini madarakani???

Cacico, JK akiondoka madarakani sheria zinabaki pale pale. Dawa ni kufanya shinikizo kulazimisha sheria hiyo ipitiwe upya, na inawezekana. Si wakumbuka sheria ya mabadiliko ya Katiba, jinsi CDM walivyoikomalia JK akakubali hoja zao hadi Serikali ikabidi iandae muswada mpya? Unakumbuka wabunge wa CCM walivyonuna?
 
Ilijadiliwa na kupitishwa kwenywe BUNGE la APRIL 13, 2012. JK akasign chapuchapu na imeanza kutumika tangua JULY 1, 2012.
Wakati sheria hii inaandaliwa na kujadiliwa, kilichokuwa kikisemwa kuwa ni dhamira ya sheriahiyo ni kuungnisha mifuko ya hifadhio ya jamii ili kuiweka chini ya chombo kimoja - SSRA. hili la kukatisha kuchukua sent zetu wala halikusemwa.
 
daaaah,very touching thread,kabla sijaanza kuchangia,uzoefu kutoka nchi nyingine kuhusu suala hili ukoje wadau
 
na nina uhakika hata ka lingezungumziwa bungeni wabunge wa chadema wasingekubali upuuzi huu
 
Yani hili linchi,hata halitamaniki.Hii mifuko serikali imeishaifirisi.serikali kila siku inakopa kwenye hii mifuko,sasa wameona hawana ela za kuwalipa wateja wao on the spot wanapohitaji ela zao,wanakuja na sababu zisizoeleweka.utanipangiaje utaratibu wa kuchukua ela yangu,niliyoipata kwa jasho langu?
 
Back
Top Bottom