Ukoo Flani
Senior Member
- Sep 1, 2011
- 156
- 41
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.
Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.
"Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda.
Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Chanzo: Nipashe
Huyu Sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya Waislamu TZ ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote? Halafu baada ya Sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje Taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi Tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?