Sheikh Ponda amezitoa wapi hizi takwimu?

Hivi idadi kubwa ya waumini wa dini bila kuwa na uwezo kiakili inasaidia nini katika Dunia hii? Hivi idadi kubwa ya wapalestina imesaidiaje kuwaondoa katika makucha kandamizi na utwala wa waisraeli? Hivi bado hatuwaoni wamasai na wasukuma mtu mmoja avyoswaga kundi la makumi ya ng'ombe?
Ndugu zangu tuache ujinga wakujitambulisha na kutengana kwa kufuata dini za wakandamizaji na wanyanyasaji. Kila siku najiuliza itakuaje babu zetu wale walio hasiwa kwenye bandari za bara Arab wakiamka na kuwakuta wakina sheikh Ponda na misimamo Yao ya KUWATENGA ndugu zao waafrika weusi na kuwakumbatia waarabu na dini yao?
Mfano wako wa Israel na Palestina sio sahihi, Israeli wangeachwa peke yao wangeshatandikwa siku nyingi na Wapiganaji wa Kipalestina, ila kwa vile Israel inasimamishwa na mataifa ya Magharibi, USA, UK nk
 
Mimi sioni tatizo kujua idadi ya dini na waumini wake hapa nchini mbona nchi zingine takwimu kama hizi zipo wazi kuna nini Tanzania?
 
Tumefikia hapa kutokana na watawala wetu kutumia dini kama mbinu ya kujiweka madarakani. Sasa wanaposhinda, baadhi ya hawa viongozi wa dini wanafikiri ushindi huo umepatikana na waumini wa dini waliyoipigia kampenni. Mfano mdogo huko Igunga, tumeshuhudia madhehebu ya dini yakifanya kampeni za wazi na kuwahasa waumini wao kuwa ni lazima wachague chama fulani. Sasa hizi ni athari chache tu, mengi na magumu zaidi yatakuja chini ya mwamvuli huu huu.
 
Hivi shetani ana akili kuliko mungu? Haujui shatani atakundanganya ili utekeleze maovu anayotaka?Jini hawezi kuwa above god hata siku moja! Ni mawazo finyu.
 
Hivi shetani ana akili kuliko mungu? Haujui shatani atakundanganya ili utekeleze maovu anayotaka?Jini hawezi kuwa above god hata siku moja! Ni mawazo finyu.
Ukitaka kupima akili na nguvu za Shetani, hebu angalia idadi ya waumini walioko kwenye nyumba za ibada (Makanisa, Misikiti nk) na muda wanaoutumia humo, kisha ulinganishe na idadi ya watu kwenye Mabaa, Madanguro nk na muda wanaoutumia humo! ("Wanaoitwa ni Wengi lakini Wateule ni Wachache!")
 
wakitaka wajue wako wangapi wahesabu watakaojitokeza kwenye maandamao yao ya amani halafu plus watakaoshiriki sensa..its very easy kwani majina ya kiislamu si yanajulikana na sensa huwa tunarekodi majina yote bwana
 
Wacheni masuala yasiyo kichwa wala miguu

unataka kujua shekhe ponda kazitoa wapi hizo takwimu, mimi pia ningependa.

Ushauri

mwenye namba ya shekhe ponda au email yake aiweke hapa na wanajukwaa wamtafute atuambie

wakatabahu

jumuiya na taasisi za kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na sheikh mkuu wa baraza la waislamu (bakwata), mufti issa shaban simba, kwamba waislamu wamekubali kuhesabiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam jana, katibu mkuu wa jumuiya hizo, sheikh ponda issa ponda, alisema kauli ya mufti simba, inaashiria kwamba bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.

Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.

"waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya watanzania hawatahesabiwa," alisema shekh ponda.

Hivi karibuni mufti simba, alitoa msimamo wa bakwata, akiwataka waislamu wote nchini kushiriki sensa ya watu na makazi itakayofanyika agosti 26, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

huyu sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya waislamu tz ni zaidi ya nusu ya watanzania wote? Halafu baada ya sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?
 
Hivi cheo cha usheikh amepewa na nani? Sheikh ponda ameishia darasa la ngapi?

Hivi huyu ni sheikh au muuni?

SHEIKH ni mtu tajiri na maarufu katika mji fulani, Hakuna cheo cha kidini ktk uislam katika hili TZ bado tunajikongoja. Hawa wanzetu elimu ya kizungu hawaitaki wanapenda kubabaisha kwa rejea za hdithi zisizo za kitaalamu wa ubinadamu!!!
 
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.

Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.

"Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda.

Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

Huyu Sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya Waislamu TZ ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote? Halafu baada ya Sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje Taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi Tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?

Nafikiri kiswahili kidogo kimekuchanganya hapo.

Mimi nilivyomwelewa ni kuwa zaidi ya 80% ya waislam hawatamsikiliza maagizo ya Mufti wa BAKWATA. na amesema kuwa Waiskam ni zaidi ya 50% ya population ya waTz.

Hivyo ndivo nilivyomwelewa mimi ambaye kiswahili ni lugha ya kigeni kwangu.

Lugha yangu ya asli ni ile inayoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto.

mi napendekeza waweke huo udini wao, ili tufuatilie nyendo zao. nimechoka na kelele zao. kuna mmoja alitoa ufafanuzi kuwa, eneo la kiseke mwanza, maeneo ya huduma za jamii, wakati wakristo wametengewa zaidi ya hekata 1,000 kufanya shughuli za kijamii kujenga makanisa na mambo memngine yanayowahusu, waislamu wametengewa hekata 100 tu. sina hakika na takwimu hizi, lakini akasisitiza, kilichosababisha utofauti wa ukubwa wa maeneo, ni kwa kuwa serikali ina takwimu za idadi ya watu kwa kuzingatia dini zao kitu ambacho hakijawahi kufanyiwa kazi tanzania.

mimi nilimjibu nikamweleza kuwa, waislamu kuna madhehebu makubwa manne, wakati wakristo utahesabu madhehebu hadi utachoka. kiukweli sijui idadi ya madhehebu kwani yaliyopo si chini ya 50 kwa yale ninayoyafahamu. kwa hiyo iwapo kila dhehebu litaomba kiwanja huko kiseke, hata hizo hekata 1,000/ hazitatosha, lakini waislam kwa idadi ya madhehebu yao, wana uhakika wa kupata kila dhehebu hekta 25, ambalo ni eneo kubwa mno.

sasa kama wanahisi wananyanyaswa katika kugawa rasilimali za taifa, tuhesabiwe kwa dini zetu ili tuone mwishoni itakuwaje
Ntamaholo habari za siku mkuu,MWZ vipi?hakika ulimjibu vema huyo mtu kuhusu mgawanyo wa hekari za ardhi.
ila mi napendekeza wendelee kugoma hivyo hivyo,maana nao wameanza kuamka,na wamechoka kudanganywa hovyo na magamba,kwangu mimi naona waislamu wameamua ku-revenge baada ya kudanganywa juu ya mahakama ya kadhi,so hii ni kutaka kulipiza kisasi.

Otherwise kufanya sensa kwa kigezo cha dini hakina mantiki hata kidogo,na hata hivyo wanaweza wakatammbuana wenyewe kupitia structure ya dini yao,kama ilivyo kwa wakatoliki mfumo wao wanatambuana kuanzia kwenye Jumuia,kigango,parokia na kisha Jimbo.kama vipi wakajifunze kwa wakatoliki sio dhambi.

Ndio maana mm naona ni kulipa kisasi kwa serikali iliyowadanganya kama watoto kuhusu mahakama ya Kadhi.
 
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu imepanga kwenda mahakamani kuzuia zoezi la sensa na kupinga kauli iliyotolewa na Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu (Bakwata), Mufti Issa Shaban Simba, kwamba Waislamu wamekubali kuhesabiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa jumuiya hizo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema kauli ya Mufti Simba, inaashiria kwamba Bakwata limekiuka makubaliano yaliyofikiwa mjini Dodoma na jumuiya zote za waumini wa dini hiyo.

Alisema kauli hiyo haitakuwa na athari kubwa kwa msimamo wa Waislamu wengi ambao hawatashiriki zoezi la sensa.

"Waislamu tumepanga tarehe hiyo ya sensa kufanya maandamano ya amani nchi nzima kwani sensa inayokusudiwa haitakuwa na matokeo sahihi kwakuwa asilimia 80 ya Waislamu ambao ni zaidi ya nusu ya Watanzania hawatahesabiwa," alisema Shekh Ponda.

Hivi karibuni Mufti Simba, alitoa msimamo wa Bakwata, akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

Huyu Sheikh amezipata wapi hizo takwimu kwamba 80% ya Waislamu TZ ni zaidi ya nusu ya Watanzania wote? Halafu baada ya Sensa ya dini ikajulikana waumini wa dini fulani ndio majority italisaidiaje Taifa? Ninaamini kuwa wapo waislamu wengi Tanzania wasioyumbishwa na kauli na misimamo ya viongozi wao, lakini viongozi wa aina hii wana mchango gani kwenye ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla?
Akiendelea na upuuzi wake msitu wa pande utamhusu. Nashauri akae kimya au arudi Burundi la sivyo Tanzania ni ya muhimu mara 1,000,0000,000 kuliko yeye.
 
Sasa Sheikh Ponda kama anajua waislam ni 80% ya watanzania wote, hivi kuna sababu gani ya kutaka kipengere cha dini kiwepo kwenye hizo karatasi za sensa?

Mi binafsi ningependa Waislam wote wogemee hiyo sensa then serikali iendelee na utalatibu wake after that tutajua tu waislam wako wangapi even though hatutajua wakristo pia wako wangapi kwasababu nchi hii ina dini nyingi including wapagani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom