Sheikh Ponda ajeruhiwa vibaya baada ya kupigwa Risasi mjini Morogoro

Status
Not open for further replies.
Mda kama dakika 20 zilizopita mjini Morogoro shehe Ponda amepigwa risasi na polisi .

Dhahama hiyo imempata baada ya kushuka kwenye tax ambako kulikuwa leo akiendesha mhadhala baada ya mhadhala huo kukawa kama kuna maandamano kueleke barabarani, gafla polisi walitokea na kuanzanza kutawanya wakati huo yeye alikuwa hayupo.

Ndipo mda mdogo akawasili akashuka na ndipo akapigwa risasi.


------------------------------------

UPDATE:

Haijulikani hali yake. RPC, Faustine Shilogile, anasema hali ni shwari ila Ponda hajui hali yake Maana polisi walizuia gari la Ponda wamkamate, lakini wananchi wakaanza kushambulia polisi ndipo wakarusha risasi hewani kutawanya watu, lakini wananchi wakamtorosha. Anasema taarifa ni nyingi za uongo, hakuna watu polisi wala hospitali waliozingira na anaomba anayejua alipo atoe taarifa.

polisi kweli wanafiki mbna kila siku inasisitizwa kutojichukulia sheria mkononi lakini wao wanajichukulia sheria mikononi,,, sio case ya Ponda tu wangapi wameuawa mikononi mwa polisi tena wengine vituoni kabisa? KWA NINI NILIZALIWA TANZANIA MIMI? PTUUU
 
Kama ni habari za kweli basi Tunataka Waziri Mkuu afute kauli yake na aachie ngazi ili hatua zaidi za kisheria zifuate.
 
Niko hapa natizama Habari ya saa2 usimu kwenye local chanel lakin hakuna Habari yoyote ile iliyotangazwa kutokana na tukio la Ponda sasa sijui wanasubiri mpaka dola ichakachue na kuhariri hiyo Habari ndo waitangaze? labda nijaribu kisikiliza redio Kama naweza kuisikia hiyo Habari lakini hakuna cha Tv yoyote ile iliyotangaza! Labda tusubiri magazeti kesho asubui!

kwa usalama wa nchi Bora wasiiripoti kabisa, wafuasi wake wanamsimamo mkali sana tunaweza kuzua mengine.!
 
Nilipoona wanaoshambuliwa ni Wayahudi, nilikaa kimya kwani mimi sikua Myahudi, walipowashambulia Chadema, sikuhangaika kwani mimi sikuwa Chadema, wwalipowashambulia jirani zangu sikuhangaika, ila waliopo kuja kunishambulia hapakuwa na mtu wa kunitetea.
Pole sana Ponda, nilikuona magereza Segerea, imeniumiza na kunihuzunisha sana, Mungu au lined uhai wako ili uje uwe shahidi mwema kwa Taifa lako.
Wewe Ni GT wa Ukweli! Cc ZeMacpolo,Kataviyetu,etc,.
 
Kwa kauli yako hii inamaanisha matukio haya yaliyofanywa na polisi yalikufurahisha/Yanakufuruhisha
1. Kuuliwa wafuasi watano wa CDM kule Arusha
2. Kuuliwa kwa Ally Dona pale Morogoro
3. Polisi kumuua mwandishi wa habari Mwangosi kule Nyororo Iringa
4. Polisi kulipua Bomu na kupiga risasi Mkutano wa CDM kule Soweto Arusha na kuua watu wanne
5. Polisi anaowaongoza kujiingiza katika biashara ya nyara za serikali pamoja na madawa ya Kulevya
6. Polisi kusimamia kupigwa kwa wabunge wa CDM kule mwanza na Green Guard wa CCM

Hautakiwi kuwa mbaguzi kiasi hiki kwani wote waliodhuriwa na hao polisi ni Watanzania bila kujali dini au Itikadi zao za kisiasa.

Mkuu kwani humfahamu kaka Rejao..!?? kagundua kuwa chama chake hakina urafiki hadi na watu wa imani yake ndo anang'aka..!!!
 
Last edited by a moderator:
Nikwel maandamano yalikuwepo lakn shehe ponda hajapigwa risasi yoyote ila hajulikan aliko baada ya wafuas wake kumtorosha.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom