Sheikh Ponda aanza tena kuchafua hali ya hewa

Status
Not open for further replies.

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,670
Zanzibar. Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimeitaka Serikali kumtiambaroni na kumchukulia hatua za kisheria Sheikh Ponda Issa Ponda kwa madai ya kukichafua chama hicho na kuhatarisha amani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Idara ya Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwaambia waandishi wa habari jana mjini hapa kuwa Ponda anapita misikitini mjini Zanzibar akieneza chuki na kuwachochea wananchi ili wafanye vurugu. Katika siku za hivi karibuni tukiwa katika Mfungo wa Ramadhan, mtu anayejiita Sheikh Ponda Issa Ponda kutoka Tanzania Bara ameamua kuweka kambi Zanzibar, akijaribu tena kuasisi ghasia, vurugu na kueneza hasama na chuki miongoni mwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla,alidai Waride.

Waride alisema Ponda amekuwa akiwakashifu viongozi wakuu wa Serikali, kutaka CCM isichaguliwe nakuwataka wananchi waandamane kama wanavyofanya wenzao wa Misri.

Ponda anapitapita kwenye baadhi ya Misikiti Zanzibar, akitoa mihadhara na mada zenye taswira ya uchochezi kwa lugha laini ya dini na kufanya siasa, anaishambulia Serikali, chama tawala CCM na kutukana vingozi wa Serikali akilenga kuamsha vurugu na kushawishi maandamano haramu, alisema Katibu huyo.

Alidai kuwa amepita maeneo ya Nungwi, Kwarara na Muyuni ambako inasemekana wamewataka waumini wafanye uasi, vya kulipiza visasi na kutangaza Jihad ambayo ni vita vya kidini. Alitaka vyombo vya Serikali vimkamate na kumchukulia hatua Ponda kwa madai kuwa anahatarisha amani ya Zanzibar wakati akiwa katika kifungo cha nje alichopewa na mahakama hivi karibuni katika kesi ya kuvamia eneo huko Changombe , Dar es Salaam.

Chanzo: MCL
 
Ponda anasema ukweli nani asiyejua kuwa ndani ya Chama na Serikali ya Chama Tawala kumejaa wahuni watupu?It's about time now Ponda beats you at your own game,almost same way you did to sabotage CHADEMA votes in 2010 General election as well as Igunga's by-election.
 
Source Habari Leo na Uhuru

Sheikh Ponda Issa Ponda anasakwa na jeahi la Polisi kwa kile kinachodaiwa kuendesha mikutano na mihadhara ya uchochezi ya kidini na kutaka Waislamu kufanya uasi na kufanya maandamano kama Misri na kudai maslai ya Waislam na kama inawezekana wapewe yote wanayoyataka.
 
Hii nchi ukianza kutaja uozo wa CCM basi wewe ni mchochezi, hivi CCM mnayofanya kuna asiyo yajua kweli?
au mnadhani mtatawala daima?
CUF chukua nchi hii utoe haki sawa kwa woteeeeeeeeeeeeeee
 
Huyu ndiyo wale wenzao na chadema. Cdm muungeni mkono kwa vitendo ili muwajue watz vizuri.
 
Kumbe kusema ukweli juu ya uovu wa serikali ya CCM ni uchochezi,P.U.M.B.A.V.U,Tuache mambo ya ajabu.Na nachukua nafasi hii adimu kama raia mwema wa Tanzania kumpongeza Mheshimiwa Ponda Issa Ponda kwa kuwaeleza watunzania wa zanzibar kuhusu uovu wa CCM ktk uendeshaji wa serikali.GOOOOO! GOOO SHEIKH PONDA tupo pamoja Magamba yasichaguliwe tena Tanganyika na Zanzibar.
 
Well done Ponda! Polisi na CCM ni sawa Kopo na Mfuniko.!! Ingekuwa ni Shekhe mkuu wa Bakwata Tanzania (taasisiya Ccm) ndio amezungumza kukosoa CUF au CDM,tusingesikia ikisemekana akamatwe kwa kuchochoea uasi. Lakini kwa kuwa Shekhe Ponda anawananga CCM chama ambacho ndio Adui mkubwa wa Watanzania basi lazima ataitwa mchochezi.

Mwigulu Nchemba ni mara mangapi amezungumza maneno ya Uchochozi na hakuchukuliwa hatua zozote? Kunya anye kuku,akinya Bata ni Kuhara!!
Binafsi namuunga Ponda mkono kuendelea kuwatangazia Watanzania ubaya wa CCM.

Waliposimama viongozi wa Dini na kumtaja kiongozi wa mmoja sasa wa CCM kuwa ni Chaguo la Mungu,mbona hatukusikia CCM wakipinga,ila leo akisimama kiongozi wa Dini km yule mwingine na kuikosoa CCM ndio tunaambiwa ni mchochezi au anataka watu Waasi!? Ama kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huwezi!! Shame on CCM!
 
Tatizo ni kuwaambia waislamu wasiichague ccm hiyo ya maandamano wamejuaje ni haramu ilihali hayajapangwa ni lini?
Mbona Maaskofu waliposema Upinzani usichaguliwe maana Kikwete ni chaguo la Mungu mlitulia kimya?
 
Huyu sheikh huwa si mwamini wala kumwelewa

Huwezi kumuelewa kwa kuwa wewe sio muelewa! Na tena Ponda sio Shekhe wa BAKWATA ni Shekhe wa Waislamu wanaojitambua......Nyie CCM mmewazoe wale Mashekhe Wanafiki wa BAKWATA(taasisi ya CCM!) Utamwaminije huku wewe mwenyewe hujiamini?

Ccm ndio Adui wa Waislamu na Watanzania kwa ujumla.Anachofanya Ponda sio dhambi wala uasi km mnavyodai bali anachofanya ni haki yake Kikatiba kuwaelimisha watu na kuwaonyesha ubaya wa CCM!....Hongera Shekhe Ponda!

Anachofanya Shekhe Ponda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom