kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,222
- 1,670
Zanzibar. Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimeitaka Serikali kumtiambaroni na kumchukulia hatua za kisheria Sheikh Ponda Issa Ponda kwa madai ya kukichafua chama hicho na kuhatarisha amani.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Idara ya Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwaambia waandishi wa habari jana mjini hapa kuwa Ponda anapita misikitini mjini Zanzibar akieneza chuki na kuwachochea wananchi ili wafanye vurugu. Katika siku za hivi karibuni tukiwa katika Mfungo wa Ramadhan, mtu anayejiita Sheikh Ponda Issa Ponda kutoka Tanzania Bara ameamua kuweka kambi Zanzibar, akijaribu tena kuasisi ghasia, vurugu na kueneza hasama na chuki miongoni mwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla,alidai Waride.
Waride alisema Ponda amekuwa akiwakashifu viongozi wakuu wa Serikali, kutaka CCM isichaguliwe nakuwataka wananchi waandamane kama wanavyofanya wenzao wa Misri.
Ponda anapitapita kwenye baadhi ya Misikiti Zanzibar, akitoa mihadhara na mada zenye taswira ya uchochezi kwa lugha laini ya dini na kufanya siasa, anaishambulia Serikali, chama tawala CCM na kutukana vingozi wa Serikali akilenga kuamsha vurugu na kushawishi maandamano haramu, alisema Katibu huyo.
Alidai kuwa amepita maeneo ya Nungwi, Kwarara na Muyuni ambako inasemekana wamewataka waumini wafanye uasi, vya kulipiza visasi na kutangaza Jihad ambayo ni vita vya kidini. Alitaka vyombo vya Serikali vimkamate na kumchukulia hatua Ponda kwa madai kuwa anahatarisha amani ya Zanzibar wakati akiwa katika kifungo cha nje alichopewa na mahakama hivi karibuni katika kesi ya kuvamia eneo huko Changombe , Dar es Salaam.
Chanzo: MCL