Tunataka kusikia deni la taifa litalipwaje (22 trillion), tunataka kusikia hela za EPA zimerudi zote na watuhumia wako mahakamani, tunataka kusikia majina wa waliohusika na biashara ya kusafirisha wanyama hai, tunataka kusikia majina ya polisi waliohusika na mauaji ya raia wasio na hati huko Arusha, Nyamongo na Songea na hatua zilizochukuliwa.