Sijui kama yuko sawa.... alishawahi kukesha akifanya ibada ya ufufuo kwa marehemu mke wa Mwenyekiti wa CCM Arusha akaishia patupu... hawa ndiyo CHADEMA wanaotaka kuongoza nchi na sera za ubaguzi wa kidini...
Wewe, ushahidi na vielelezo vyote vinavyokusudiwa kutolewa huorodheshwa kabla ya kesi kuanza, sasa wewe utapelekaje kitepu chako kama hakikuorodheshwa? wacha ujinga!
CCM-Magamba ndio mnaudini,na hayo maneno usimlishe Mh Lema hayo maneno yalisemwa na Juma Ikangaa na sasa mahaka inatafuta kuthibisha madai hayo,ila kwa sasa tulie nauhakika kuwa nani kasema ni Ikangaa ndio watu wamemsikia mahakamani,na hata hivyo udini huu muasisi ni JK kipindi cha uchaguzi na hii ni kutokana na kuelemewa hivyo akaamua kuwagawa watu kwa udini akaupigia upatu sana,lakini leo hii wana CCM hao hao ambao ndio magamba wenyewe wanabanana makanisani na kwenye maulid hapo mnazi mmoja,kila mtu ni shahidi jinsi hawa wana magamba-CCM wanavyobanana kwenye nyumba za ibada huku wakijaribu kutafuta support ya kwenda Ikulu,leo mnavyosema udini ni sera ya CDM ni ya kweli hayo?
Na kwakuwa mna hamu sana na jimbo la Arusha najua mnajaribu sana kupindisha sheria na tayari kuna tetesi kuwa EL anasimamia jimbo hilo lirudi ili mmweze kujenga ngome kwa ajili ya 2015.yetu macho na juhudi zetu hazitokoma,pamoja tutashinda CDM
Nikupe pole bwana GWALISHENZI manake kama unatmia miwani basi leo utakuwa umesahau kuvaa na kama hutumii basi nina shaka na uwezo wako wa kusoma na kupambanua sentensi na siku zijazo read btn the lines ndo ujaribu kujibu na uwe na uwelewa mzuri wa NYAKATI; wakati uliopo, ujao, uliopita n.k! Cant blaim you anyway.........
Alkaeda wote ni waislam lakini waislam wote si Alkaeda, bado sijaona mtu mwenye kunieleza how this should be an issue, naona ni mwendelezo tu wa vijembe badala ya kujibu hoja kwa hoja.
Mkuu umenena. UDINI ni sumu mbaya sana inayopandikizwa na CCM kama silaha ya kisiasa dhidi ya wengine. Yaani hii ni hatari sana kwa taifa letu. Huwezi kunishawishi Lema na CHADEMA kwa ujumla ni wendawazimu kiasi hicho hadi watamke ****** kama huo. CCM mnakera na mnatupeleka siko kwa siasa zenu za maji taka. Naamini kabisa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinaandaa mikakati madhubuti ya kukabiliana na ujinga huu wa CCM.
Si muda mrefu mambo yataiva na tutawataarifu rasmi hapa mjengoni, lakini kwanza tunafanya kazi ya kutambulishana! Lakini fahamu hadi Askari wa kimarekani na ambao wameshawahi kushiriki vita kule Iraq, Afaghanistan na kwengineko sasa wanasilimu na kujiunga na haya makundi; jee wewe bado kwanza!
Ushahidi huu hauna nguvu ya kumtia hatiani Lema, unless kama atakiri mwenyewe kuwa alitenda kosa tajwa
Mkuu siasa uchwara tu hizo. Wanasiasa walioishiwa hoja hukimbilia DINI. Hivi mahakama ikithibitisha kwamba Lema hakutamka hayo maneno inakuwaje hapo? Just wait and see soon itathibitishwa sio Lema bali washindani wake (Batilda, et al) ndio wadini kwa kujaribu kupeleka ushahidi wa uongo wenye mwelekeo wa kidini mahakamani.