Komeo
JF-Expert Member
- May 3, 2011
- 2,498
- 1,171
Hapo kwenye red. Ni nani anayetoa vibali vya kufanya mikutano ya vyama vya siasa vilivyosajiliwa na Tendwa? Hilo kosa liko kinyume na kifungu kipi cha Katiba au sheria ipi? Ninavyofahamu mimi ni kuwa vyama vya siasa vinaweza lakini havilazimishwi kuitaarifu polisi kwa ajili ya taarifa tu juu ya uwepo wao eneo fulani, na sio kuomba hicho "kibali".MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, wamekamatwa na kusafirishwa hadi wilayani Chunya kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kutoa maneno ya uchochezi. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa walikamatwa juzi katika eneo la Inyara, wakiwa ndani ya basi kuelekea Dodoma.