MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako na Katibu Mwenezi wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini, Lucas Mwampiki, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, wamekamatwa na kusafirishwa hadi wilayani Chunya kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kutoa maneno ya uchochezi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kusema kuwa walikamatwa juzi katika eneo la Inyara, wakiwa ndani ya basi kuelekea Dodoma.
Alisema kuwa viongozi hao walisafirishwa hadi Chunya ambako waliunganishwa na wenzao wawili kabla ya kupelekwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Kamanda Diwani aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Katibu wa CHADEMA Kata ya Makongorosi, Erick Luvanda na Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Dominick Chaula.
Alisema baada ya kusomewa mashtaka yao mahakamani, watuhumiwa walipewa dhamana na kutakiwa kurudi tena mahakamani hapo Agosti 16, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kwa kesi hiyo.
Hivi karibuni viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Chunya walifanya mikutano mbalimbali kwa siku 10 wilayani humo ikiwa ni sehemu ya operesheni iliyopewa jina la ‘CHADEMA Twanga Kotekote' yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi na kukijenga chama hicho.
Source:Tanzania Daima