Serikali yashauriwa kuongeza bajeti kwenye tume ya taifa ya matumizi bora ya ardhi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,977
958

MHE. JAFARI WAMBURA AISHAURI SERIKALI KUTENGA FEDHA ZA KUTOSHA KWAAJILI YA TUME YA TAIFA YA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI

Mbunge wa Jimbo la Rorya Mhe. Jafari Chege Wambura tarehe 22 Juni 2023 amechangia hotuba ya Bajeti ya Serikali Kuu kwa mwaka 2023-2024 bungeni jijini Dodoma

"Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya hasa kwenye Jimbo la Rorya. Wiki hii tumepokea zaidi Shilingi Milioni 570 kwaajili ya ujenzi wa Sekondari mpya na mwaka uliopita nilipewa Shilingi Milioni 470 kwaajili ya Sekondari mpya " - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Naendelea kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi anavyotushika mkono wananchi wa Rorya. Kwa muda mrefu tumekuwa na changamoto ya Maji lakini sasa katika Miradi ya miji 28 tumepewa zaidi ya Shilingi Bilioni 132 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya Maji. Na sasa linajengwa Tanki la Lita za Ujazo Milioni 6 kwa ajili ya kuhakikisha linasambaza Maji kwenye Wilaya ya Rorya." - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutupa fedha kwaajili ya ujenzi wa VETA. Na kuridhia kuingiza barabara ya Mika - Utegi - Shilati - Kilongwe kwa ujenzi wa kiwango cha lami kwa kilomita 56 ambayo inakwenda kufungua uchumi wa Rorya, nchi jirani na mkoa mzima wa Mara" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Namshukuru Waziri wa Fedha na Mipango kwa kumshauri Mheshimiwa Rais kuridhia na kufuta ada kwa wanafunzi wanaosoma Vyuo vya Ufundi na kuridhia kwenye Vyuo vya Kati kutoa mikopo kwa wanafunzi waliochaguliwa kwenda maeneo hayo" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Nashauri, Waziri wa Fedha na Mipango, wanafunzi wote wanaokwenda kwenye Vyuo vya Kati wapewe mikopo haijalishi anakwenda kusomea fani gani. Ambaye hakusomea masomo ya Sayansi ukirudi nyuma utagundua si sababu yake, hakuwa yeye ndiyo chanzo cha kutokusomea Sayansi maana Shule zetu nyingi zina changamoto nyingi sana za Walimu wa Sayansi" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Nakushukuru Waziri wa Fedha na Mipango kwa kumshauri Mheshimiwa Rais kwa kuridhia kuondoa VAT kwenye nyumba zinazojengwa za kibiashara zenye gharama chini ya Shilingi Milioni 50. National Housing, TBA na Mifuko ya Hifadhi inayofanya maendeleo ya ujenzi wa Nyumba walitumia hii kama fursa ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ili nyumba za bei nafuu zijengwe maeneo yote ya nchi nzima" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Natamani nione NSSF, TBA, National Housing wanakuja Rorya wanajenga nyumba Milioni 25 kwaajili ya kuwasaidia watumishi, waende Halmashauri zingine wajenge nyumba Milioni 30 na Milioni 45 maana walikuwa wanalia na kigezo cha gharama za nyumba na wananchi wengi walikuwa wanashindwa kulipia hizi nyumba kwa sababu ya ongezeko la VAT" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi wamepewa Mamlaka makubwa ya kupanga na kuainisha Matumizi bora ya Ardhi. Leo kwenye mpango wa tatu wa Taifa 2022 - 2026, anayekwenda kutafsiri asilimia 50 ya kuainisha Mpango Bora wa Matumizi ya Ardhi, Anayetafsiri Ilani ya CCM 2020-2025 ifikapo 2025 Vijiji viwe vimepangwa Matumizi zaidi ya 4131 na anayekwenda kutafsiri hotuba za viongozi ni hii tume" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi bora ya Ardhi wamefanya kazi kubwa sana Msomera, Loliondo, Bunda, Tarime. Kwanini Tume hii hatuipi meno na hatuitengei fedha nyingi ili iweze kuendana na Ilani ya CCM 2020-2025, Maelekezo ya Mheshimiwa Rais na Iendane na Mpango wa tatu wa Taifa. Kama tunataka kuondokana na migogoro ya Ardhi nchini ni lazima tume hii tuitengee fedha" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Mheshimiwa Waziri kwa sababu kuna fedha ya mkopo ili Shilingi Bilioni 345 mmege zaidi ya Bilioni 20 au Bilioni 30 muwape Tume ya Taifa ya Matumizi bora ya Ardhi ili waende wakapange Matumizi bora ya Ardhi nchini ili waweze kutimiza na kuendana na malengo ya Mheshimiwa Rais" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya
 

Attachments

  • mfanoqwe.jpg
    mfanoqwe.jpg
    51.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom