Serikali yaomba madaktari nje ya nchi, BILIONI 200 ZATENGWA KUWALIPA

au India?
Hii serikali ya kihindi kiongozi!Maana wanakunyima shilingi 2000 alafu gharama ya kesi ni 20000000000.Alafu pia hii ni njia ya kupiga hela za walipa kodi kwa ufisadi yaani wanatengeneza matatizo ili waibe pesa kwa kujifanya wanatatua matatizo!Dhaifu anashauriwa na liwalo na liwalo akisaidiw na mr.usingizi wasura chini ya mwamvuli wa wapuuzi ccccm unategemea niini kiitokee?
 
Ooooooooh! Bilion 200? si walisema serikali haina hela? Watawalipa milele hao marafiki au mpaka uchaguzi mkuu 2015 serikali mpya itakapochukuwa nafasi??
 
Naiunga mkono serikali kwa Immediate response maana kuzidi kuvimbishiana kifua na madaktari wakati watu tunazidi kuumia na suluhu haipatikani basi ni sawa tu wafanye chochote kuzinusuru afya za raia wake.After all serikali ikiendelea kusikiliza kila madai yao likiwemo hilo la mshahara wa mil3.5 nchi haitatawalika maana kila kada ya watumishi wa umma ita-react kutaka kuongezewa mishahara mwisho wa siku bajeti ya nchi inakuwa inaishia kwenye matumizi ya serikali bila miradi ya maendeleo.Serikali lazima ionyeshe msimamo wake kama muhimili mkuu wa nchi.

Kwasasa tuangalie namna ya kutatua tatizo la kuwahudumia wagonjwa mahospitalini wakati wao bado wapo kwenye malumbano yao yasiyo na kikomo.
Ni kweli cha msingi ni kuokoa maisha ya wananchi kwanza.Wananchi wengi wameathirika kutokana na mfululizo wa migomo ,tumefiwa na ndugu na jamaa zetu.Serikali lazima ichukue hatua kulinda maisha ya watu wake wakati jitahada zingine zinaendelea za kutafutia ufumbuzi mgomo huu.
 
Its all bulshit..madai ya walimu ni kama bilioni 40 hivi wanasubiri wagome watafte mbadala kwa bilioni 100...kweli hii nchi ya MFALME JUHA....
 
Wamekwisha kabisa, tuwaombee fahamu zao zirudi. Kuliko kuboresha hali ya mazingira ya afya hapa, unachukua fedha na kuzitupa kwa madaktari ambao hawataweza hata kuwasiliana na wananchi wako. Bado siamini kama wamefiki kiwango kidogo hivyo cha kufikiri. Siuamini huu uzi.

Chanzo hujakiona?
 
wakitekelezewa madaktari madai yao, watumishi wengine wataanza manung'uniko. Madaktari waache ubinafsi.mbona serikali inawaruhusu kuwa na hospitali binafsi majumbani, mishahara yao ni karibu mara 2 ya watumishi wengine. Hilo halipo kwa watumishi wengine wa serikali. Madaktari waache mgomo wa kiburi, hakuna serikali itakayokubali kupiga magoti kwa stahili hii.
we una matatizo ya kisaikolojia kama si gamba..by the way una uhuru wa kubwabwaja.....mdomo wako....kifo ni kitu cha kawaida hakuna binaadam aliyeletwa kuurithi ulimwengu..tunachotaka ni usawa na haki haijalishi kias gan cha damu kitamwagika kwan hakuna nchi iliyoendelea duniani bila kumwaga damu kama ipo nitajie....
 
Wajinga ndio waliwao. We acha tu, yatawashinda.

Kwa nini tupoteze pesa kwa jambo ambalo linawezekana juu ya meza? Au ndo njia ya kuwanyima vijana ajira
Iwe vipi watoto wa jirani waletwe home na kupewa huduma nzuri na wa kwetu wenyewe tusiwasikilize?
Au ndo 10%?
 
hii serikali ya kihindi kiongozi!maana wanakunyima shilingi 2000 alafu gharama ya kesi ni 20000000000.alafu pia hii ni njia ya kupiga hela za walipa kodi kwa ufisadi yaani wanatengeneza matatizo ili waibe pesa kwa kujifanya wanatatua matatizo!dhaifu anashauriwa na liwalo na liwalo akisaidiw na mr.usingizi wasura chini ya mwamvuli wa wapuuzi ccccm unategemea niini kiitokee?
create a problem....provide a solution......hapa ndo utaona kwamba how genius our tyrants are...
 
Serikali, kweli hata mpatanishi wa kimataifa Rais mstaafu Mkapa kashindwa kupewa mgogoro huu?
Ondoeni kesi yenu mahakamani anzeni usuluhishi. Pia wale waliowafukuza madkt waambieni wamekwenda
nje ya utaratibu. Kesi bado haijasikilizwa. Suluhu hapa ni hekima ya kujishusha tu. si wageni kuja kutibu
wagonjwa. Mnapoleta wageni, zile huduma mnazowapa, madokt wanaziona na kuzilinganisha na
za kwao kisha wanakuwa wachungu zaidi.

Nani anajua nani atakuwa rais wa kesho? Watawapeleka jela ktk uzee wenu ndipo mtakuwa kama Marais
wa misri na irak.
 
hahahaha! ccm oyeeeeeeeeeeeee! This is the cardinal sign of failure. yan wamekaa mawazir wake had mwakyembe na makamba wakiwemo na kuadhimia hv!!!!!!!!!!!!!! vry fantastic, anyway yetu macho baana.
 
Sasa hiyo Bil 200 itatoka kwenye mfuko gani na itajadiliwa vipi wakati Mama Spika hataki mjadala wa Madr bungeni???
 
kumbe pesa za kutekeleza madai ya madaktar zipo,kumbe sarikali ndio inayotengeneza migogoro.je hizo pesa zilifichwa wapina kwa malengo yapi?jamani tuzinduke tunaibiwa tuzinduke!!!!!!!!!!!!!!!!!!! na tuwahoji tusikubali kupelekwapelekwakm coloni la ccm.
 
Mwisho wa siku Tatizo liko palepale....na Bil 200 zimekwenda!!!! sina imeni sana na hii hoja...ila kama ndivyo, kweli hii ITAKUWA NI SERIKALI SIVIKU!!!!!!


Walimu wametangaza kuanza mgomo jumatatu. Je kama kweli watatekeleza nia yao hiyo ya kugoma serikali itakodi walimu toka nje ya nchi tena?
 
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika
zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri
kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa RaisKikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote
zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo,kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili yakuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote
warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

Habari zimedai kuwa
madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki zikiwemo India, China, Cubana Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao
wamegoma.

Inaelezwa kuwa mara baadaa ya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa
nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa
kazini kwa masharti makali.

Hata hivyo, uamuzi wa
serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni,lakini walikwama baada ya
Spika Anna Makinda kuzuiamjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.

Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali nikiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai
kuwa kuna kesi mahakamani.
“Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani,sasa imewezaje kuwafukuza
madaktari wakati jambo lipo mahakamani?”
alihoji Dk. Kigwang’ala.

Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadilianokwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.

Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuruwa mahakama.

Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko
katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

Hospitali zingine ambako
madaktari wamefukuzwa
kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.

Jeshi lachukua nafasi za
madaktari, Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu
kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini.

Juzi Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma
ya matibabu kwa wagonjwa.

Msemaji wa JWTZ Kanali
Kapambala Mgawe katika
mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya
Jeshi Lugalo Kikosi ya 521,
Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila
vikwazo.

“Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo
hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu
labda kwa asilimia 90.

Mgawe alisema madaktari
wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake,hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua
kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.

Chanzo:TANZANIA DAIMA
UZURI WA HAYA MAMBO HUA YANAKUJA KUONYESHA NI JINSI GANI SERIKALI YETU INATHAMINI WATU WAKE! YAANI KAMA WEWE NI MBONGO TU, BASI MBELE YA SERIKALI MAISHA YAKO HAYANA THAMANI! VIONGOZI WETU WAKO TAYARI KUTUMIA MABILIONI YA MAPESA KUWALIPA WATU WA NJE, ILA KUKUBALI KUWA WATAALAM WETU NA MAZINGIRA YAO YA KAZI YAPO MAINTAINED VIBAYA HAWATAKI! HALAFU WANATUAMBIA HELA HAZIPO! iLA MIMI NADHANI WANA MAANA KWAMBA PESA ZA KUMPA MTANZANIA MWENZAO NDIO HAZIPO!
VILE VILE WASITUDANGANYE HAPA! KWANI HIZO NCHI WANAZOTAKA KUTOA MADAKTARI NDIO ZIMEJITOSHELEZA NA MADAKTARI? WATAPATA MADAKTARI WANGAPI?( MANAKE MADAKTARI WALIOGOMA HUKU NI ZAIDI YA 1000) NDIO WATATULETEA WALE MADAKTARI AMBAO KULE KWAO NI BOGUS WAJE WAFANYIE MAZOEZI KWENYE MIILI YA WATANZANIA WETU WAGONJWA, HALAFU ON TOP OF THAT WALIPWE MABILIONI YETU!
 
Sijawahi kusikia ,nasikitika kuwa na viongozi wenye vichwa vinavyotembelewa na nyenyele kichwani billioni 200 kwa kiwango kikubwa kingepunguza matatizo makubwa kwa sekta ya afya
serikali ya awamu ya nne wamevimbiwa ,kumbe wanatafuta utukufu ndio maana kuna mjinga kama charles changoji anasema atawakamata madaktari na kuwafunga ha ha
 
Back
Top Bottom