Serikali yaomba madaktari nje ya nchi, BILIONI 200 ZATENGWA KUWALIPA

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,930
1,165
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika
zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri
kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa RaisKikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote
zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo,kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili yakuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote
warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

Habari zimedai kuwa
madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki zikiwemo India, China, Cubana Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao
wamegoma.

Inaelezwa kuwa mara baadaa ya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa
nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa
kazini kwa masharti makali.

Hata hivyo, uamuzi wa
serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni,lakini walikwama baada ya
Spika Anna Makinda kuzuiamjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.

Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali nikiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai
kuwa kuna kesi mahakamani.
“Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani,sasa imewezaje kuwafukuza
madaktari wakati jambo lipo mahakamani?”
alihoji Dk. Kigwang’ala.

Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadilianokwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.

Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuruwa mahakama.

Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko
katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

Hospitali zingine ambako
madaktari wamefukuzwa
kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.

Jeshi lachukua nafasi za
madaktari, Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu
kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini.

Juzi Waziri Mkuu Mizengo
Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma
ya matibabu kwa wagonjwa.

Msemaji wa JWTZ Kanali
Kapambala Mgawe katika
mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya
Jeshi Lugalo Kikosi ya 521,
Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila
vikwazo.

“Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo
hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu
labda kwa asilimia 90.

Mgawe alisema madaktari
wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake,hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua
kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.

Chanzo:TANZANIA DAIMA
 
Wamekwisha kabisa, tuwaombee fahamu zao zirudi. Kuliko kuboresha hali ya mazingira ya afya hapa, unachukua fedha na kuzitupa kwa madaktari ambao hawataweza hata kuwasiliana na wananchi wako. Bado siamini kama wamefiki kiwango kidogo hivyo cha kufikiri. Siuamini huu uzi.
 
Wamekwisha kabisa, tuwaombee fahamu zao zirudi. Kuliko kuboresha hali ya mazingira ya afya hapa, unachukua fedha na kuzitupa kwa madaktari ambao hawataweza hata kuwasiliana na wananchi wako. Bado siamini kama wamefiki kiwango kidogo hivyo cha kufikiri. Siuamini huu uzi.

Chanzo hujakiona?
 
Natamani hao madaktari wakishakuja manesi na wauguzi wengine wagome ili serikali ituletee manesi wa cuba, india na nchi rafiki! Haahaha serikali dhaifu, Cabinet dhaifu, rais dhaifu na maamuzi yao dhaifu! Utashangaa hao madokta wa kutoka nje watalipwa kwa dollar what a shame.
 
Huu ni muujiza unapendekezwa! Madaktari wa kigeni wengi ya kutosha kuziba pengo la wanaogoma!

Ki hali halisi ni kwamba wagonjwa wetu wataendelea kuumia/kufa hadi suluhisho la kweli na madaktari wetu wenyewe litakapopatikana.
 
Huyu dhaifu kweli hana akili kabisa yaani atawawa kikatili hadi atajuta na ataenda kutupwa motoni kwa jinsi anavyowatesa watz, jamani tufunge na kuomba Mungu hayuko mbali nasi time will tell soon
 
Na walimu wanagoma watakodishwa wa kuziba pengo?hapa ni kuwa serekali sikivu ya dhaifu jk inahairisha matatizo badala ya kutatua,is so sad.kuliko kukodi bora wangewapa na urai.
 
Unategemea nini baraza la mawaziri likiongozwa na Mr Liwalo na liwe likimshauri Mr Dhaifu? Ndio matokeo yake haya.Alafu baadaye ooh nilishauliwa vibaya Mpango ukikwama.nawasubiri kwa Hamu kuona dr wa kichina, na indians akimuhoji mswahili vizuri na kumtibu malaria katika mazingira haya ya vifaa duni.
 
Back
Top Bottom