Serikali yaomba madaktari nje ya nchi, BILIONI 200 ZATENGWA KUWALIPA

Kama hii habari ni ya kweli basi vyama vya upinzani, wanaharakati na sisi wananchi tunapaswa kuandamana mapema iwezekanavyo kuelekea magogoni kumwambia huyo DHAIFU kuwa hayo sio matumizi sahihi ya kodi zetu na ni usaliti kwetu kwani hayo sio maisha bora aliyotuahidi!!!
Hakika watakuwa wamefikia mwisho wao wa kufikiri - Hivi huyo Mchina/Cuba/Hindi ataongea lugha gani na hawa wagonjwa wetu???
 
Hivi kumbe "Dhambi ya Uchakachuaji" ni mbaya kiasi hicho? Fikiria 2010 wananchi walimkataa JK na Tume ya Uchaguzi ikachakachua matokeo sasa kila mtu anamwita DHAIFU! Kuchagua Spika CCM nao wakamchakachua SS na kumbeba AN na matokeo yake tumekuwa na Bunge DHAIFU! Na matokeo ya uchakachuaje huu yanatutesa wote - waliokuwemo na wasiokuwemo!!!
Watanzania tuamke usingizini na kusema kwa dhati "Hapana, sasa imetosha"!!!
 
Yaani hapo ni lazima pawe na wakalimani 200 X 2 = 400 nauli toka kwao nyumba nzuri kwa vile ni wageni usafiri.
wawe na moyo wa kuwahudumia wagonjwa wachafu waliotoka kwenye nyumba inayopikwa kwa kuni nguo chafu hakuna maji ya uhakika ...mgonjwa anapiga mswaki kwa miti ane kunya porini hajatawaza
wakija wakikaa week tu wao wenyewe watakimbia
 
serikali imeamua kuagiza
madaktari kutoka nchi za nje
watakaochukua nafasi ya
wale wa hapa nchini ambao
wamegoma kuanzia
mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka katika moja ya
vyanzo vya kuaminika
zimesema kuwa uamuzi huo
wa serikali ulipitishwa katika
kikao cha baraza la mawaziri
kilichokutana mjini dodoma juzi chini ya uenyekiti wa rais jakaya kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao
hicho zilidai kuwa rais
kikwete alikerwa na tabia ya
madaktari kupingana na
serikali licha ya juhudi zote
zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo,
kiasi cha sh bilioni 200
kimetengwa kwa ajili ya
kuwaleta na kuwagharimia
madaktari hao wa nje na pia
baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za
jeshi kama lugalo na zingine
ndogo kubeba jukumu hilo
kwa sasa pamoja kuagiza
madaktari wastaafu wote
warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

Habari zimedai kuwa
madaktari hao wanasadikiwa
watatoka katika nchi rafiki,
zikiwemo india, china, cuba
na afrika kusini, na kwamba
wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao
wamegoma.

Inaelezwa kuwa mara baada
a ya kukamilika na kuanza
rasmi kwa huduma za
matibabu, madaktari wa hapa
nchini waliomo katika mgomo
na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na
serikali kimyakimya,
watalazimika kurejeshwa
kazini kwa masharti makali.

Hata hivyo, uamuzi wa
serikali kuwatimua madaktari
wakati suala lao liko
mahakamani, umewagawa
wabunge.

Baadhi ya wabunge walijaribu
kuhoji suala hilo bungeni,
lakini walikwama baada ya
spika anna makinda kuzui a
mjadala huo kwa madai kuwa
suala hilo liko mahakamani. Mbunge wa nzega, dk. Hamis
kigwangala, alisema kuwa
kilichofanywa na serikali ni
kiini macho kwani juzi waziri
mkuu mizengo pinda alisema
serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai
kuwa kuna kesi mahakamani.
"juzi serikali imesema kuwa
haiwezi kutoa kauli kwa vile
jambo hilo lipo mahakamani,
sasa imewezaje kuwafukuza
madaktari wakati jambo lipo
mahakamani?"
alihoji dk. Kigwang'ala.

Aliitaka serikali kuondoa kesi
hiyo ili kurejesha majadiliano
kwani ndio njia pekee ya
kukabiliana na mgogoro huo. Mbunge wa ubungo, john
mnyika, alimshangaa spika
anna makinda kuzuia mjadala
huo kwani ungeweza
kujadiliwa bila kuingilia uhuru
wa mahakama.

Juzi uongozi wa hospitali ya
taifa muhimbili, uliwafukuza
kazi madaktari 229 walioko
katika mafunzo kwa njia ya
vitendo kutokana na mgomo
unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi
mmoja.

Hospitali zingine ambako
madaktari wamefukuzwa
kutokana na mgomo huo ni
pamoja na mbeya na dodoma. Jeshi lachukua nafasi za
madaktari wakati huo huo jeshi la
wananchi wa tanzania (jwtz),
limeanza kutekeleza kwa
vitendo agizo la serikali la
kutoa huduma za kitabibu
kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini. Juzi waziri mkuu mizengo
pinda akiwa bungeni alisema
serikali imeamua kuwatumia
madaktari waliopo wizara ya
afya na ustawi wa jamii,
wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma
ya matibabu kwa wagonjwa. Msemaji wa jwtz kanali
kapambala mgawe katika
mahojiano maalum na gazeti
hili, alisema juzi baada ya
waziri mkuu pinda kutoa agizo
hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la dar
es salaam, hospitali kuu ya
jeshi lugalo kikosi ya 521,
mgulani na ile ya kikosi cha
navy-kigamboni na hospitali
zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila
vikwazo. "kwanza naomba umma
uelewe hivi hospitali za jwtz
hapa nchini kwa asilimia 70
zimekuwa zikiwatibu raia bila
vikwazo vyovyote hivyo agizo
hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa
kutibiwa katika hospitali zetu
labda kwa asilimia 90.

Mgawe alisema madaktari
wanajeshi wapo kwa ajili ya
kulinda taifa na watu wake,
hivyo akawahakikishia
wananchi wanaougua
kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa
akidai kuwa hawaoni mantiki
ya daktari kugoma.

Chanzo:tanzania daima
hivi wananchi wanakaa dar tu au na mikoani ,je huko mikoani walipogoma madaktari watatuma madaktari au jamani tanzania sio dar tu maana nimesikia kwa masikio yangu eti wamekodi madaktari wa hindu mandar,agakhani,ibrahim haji.hosp za kihindi kama 4 hivi ,sasa billion hizo siwangeboresha huduma au jamani mbona wanakuwa hivihawa,
 
Kwa hasira na maguvu viongozi wanapata hasara ya kuamua na kutekeleza mambo bila kutumia busara.
Utetezi pekee wanaobaki nao ni kwamba watawaliwa hawana uwezo wa kutambua upuuzi wao.
Tutaona mengi katika serikali hii.
 
Mwisho wa siku Tatizo liko palepale....na Bil 200 zimekwenda!!!! sina imeni sana na hii hoja...ila kama ndivyo, kweli hii ITAKUWA NI SERIKALI SIVIKU!!!!!!
 
dah! Wanaagizia kama magar vile!..wajiandae kuagizia na walimu,manes,...na hata majesh siku wananchi tukichachamaa
 
Hii ndio ile PM alisema na liwalo liwe...hata kama uamuzi huo utakuwa si wa busara kama ulivyo na liwalo liwe...hata kama kuwagharamikia hao wageni/rafiki itakuwa mara kumi kuliko kusiliza kilio cha madaktari na liwalo liwe....etc

Honestly this TZ is a very sad story... Kuna President sijui ana priside nini....kuna PM sijui ana prime mini...kuna ministers sijui wanaminister kitu gani...kuna Parliment hili ndio hopeless... with over 100+ special seats when in actual fact we only need less than 10 seats to represent specific interest groups

Believe you me the latest decision imekuwa motivated na ukweli kwamba kuna kikundi kidogo cha watu kitakachotakiwa kuratibu the whole exercise ambacho kinatarajia kunufaika a hundred times ukilinganisha na huduma itakayotolewa na utaratibu huo. TZ you aint seen nothing yet, the worst is yet to come. SHAME
 
Nakumbuka wakati mmoja bosi wangu alipata ajali akiwa hapa nchni na akalazimka kuwa evacuated kwenda South Afica, hivyo ilikuja Air Ambulance toaka huko. Hospitalia ya Agakahan ilijitahidi sana kutoa Ground Ambulance iliyo bora kuliko zote walizo nazo lakini cha kushangaza daktari incharge wa Air Ambulance hakuruhusu hata strecher za Aga khan kuingia ndani ya Air Ambulance yake. Ilibidi hata mgonjwa afanyiwe Stelalization akiwa chini na kubadilishwa mavazi ndipo akingizwa katika hiyo Air Ambulance.

Hivyo nashukuru sana kwa uamuzi huu wa kuwaleta madakatarui kutoka nje ya nchi, hii ndio itathibitisha ni kwa kiais gani madakatari wetu walikuwa na uzalendo kwa kukubali kuendelea kutoa huduma katika mazingira duni ya tiba yalivyo sasa.

TRC ilipobinafisishwa RITES wakaleta vichwa vya trni vyao pamoja na madetreva wa viche hivyo walistajabua kukuta vichwa vyetu vikiendelea kutoa huduma ilihali havina breki, ni vibovu n.k Ni vyema sasa wakaja watu kutoka nje ili tuweze kutambua kuwa ni kwa kiwango gani uzalendo wetu umesababisha kuua utaalamu
 
Yaani hii inaonyesha pesa ya kuwalipa Madaktari ipo ila ni kiburi tu cha serikali. Hivi mfano walimu nawo wakigoma ina maana wataletwa walimu toka nje? Lakini kama hiyo ni kweli, mjue kati ya hizo fedha kuna ulaji wa hawo wakubwa- lazima uchakachuaji upo.
 
Naiunga mkono serikali kwa Immediate response maana kuzidi kuvimbishiana kifua na madaktari wakati watu tunazidi kuumia na suluhu haipatikani basi ni sawa tu wafanye chochote kuzinusuru afya za raia wake.After all serikali ikiendelea kusikiliza kila madai yao likiwemo hilo la mshahara wa mil3.5 nchi haitatawalika maana kila kada ya watumishi wa umma ita-react kutaka kuongezewa mishahara mwisho wa siku bajeti ya nchi inakuwa inaishia kwenye matumizi ya serikali bila miradi ya maendeleo.Serikali lazima ionyeshe msimamo wake kama muhimili mkuu wa nchi.

Kwasasa tuangalie namna ya kutatua tatizo la kuwahudumia wagonjwa mahospitalini wakati wao bado wapo kwenye malumbano yao yasiyo na kikomo.
 
Yaani hii inaonyesha pesa ya kuwalipa Madaktari ipo ila ni kiburi tu cha serikali. Hivi mfano walimu nawo wakigoma ina maana wataletwa walimu toka nje? Lakini kama hiyo ni kweli, mjue kati ya hizo fedha kuna ulaji wa hawo wakubwa- lazima uchakachuaji upo.

Wakitekelezewa madaktari madai yao, watumishi wengine wataanza manung'uniko. Madaktari waache ubinafsi.Mbona serikali inawaruhusu kuwa na hospitali binafsi majumbani, Mishahara yao ni karibu mara 2 ya watumishi wengine. hilo halipo kwa watumishi wengine wa serikali. Madaktari waache mgomo wa kiburi, hakuna serikali itakayokubali kupiga magoti kwa stahili hii.
 
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao.

Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.

Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.

Inaelezwa kuwa mara baada ya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa kazini kwa masharti makali.

Hata hivyo, uamuzi wa serikali kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.

Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada ya Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani. Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema serikali haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani.

"Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo mahakamani?" alihoji Dk. Kigwang'ala.

Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo. Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.

Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza kulipwa posho zao za mwezi mmoja.

Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma. Jeshi lachukua nafasi za madaktari Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini. Juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa.

Msemaji wa JWTZ Kanali Kapambala Mgawe katika mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Kikosi ya 521, Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila vikwazo.

"Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu labda kwa asilimia 90. Mgawe alisema madaktari wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake, hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.
 
Sure z anothr SILLY SEASON! Tukifk uchaguz ujao kwa aman cjui coz serkal imekua ikifanya ad hoc decisiöns whch ar like addenda in our country! Haingii akilin kuwaagiza madaktar toka nje ya nchi whl ikijulkana kua garama ni kubwa ya kumhudumia dr toka india ukilingansha na dr wa tz! "SERIKAL DHAIFU HUFANYA MAAMUZI DHAIFU SIKU ZOTE" tusubr tuingie mtaan kuiondoa serkal Dhaifu
 
Back
Top Bottom