Serikali ya mseto mbioni kama wengine tulivyotabiri. Je, CHADEMA watakubali kushiriki katika Serikali ya aina hiyo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,140
144,641
Nchi hii ukiona media au watu maarufu (wanasiasa, wasomi, wanazuoni, n.k) wanaongelea jambo fulani kwa uhuru, jambo ambalo mwanzoni walikuwa hawezi kuliongelea au kuliuunga mkono, ujue teyari jambo husika lina baraka za watawala na liko mbioni kutumia au kutokea.

Kwa misingi huo, naiona serikali ya mseto kwa upande wa Tanzania Bara ikienda kuundwa siku za mbeleni ambapo mabadiliko ya katiba au katiba mpya itaruhusu kuundwa kwa serikali ya aina hiyo nchini kwetu.

Swali ni je, CHADEMA watakubali kushiriki katika serikali hiyo?

NB: Mbowe anaweza kuwa teyari kuridhia kuundwa kwa Serikali ya aina hii huku yeye akiweza kupewa hata uwaziri mkuu, ila namshauri awe makini na asitumie vibaya nafasi yake kama mwenyekiti kutaka kufanikisha jambo hili(in case ana dhamira hiyo) kwani anaweza kukigawa na kukivuruga vibaya chama.

Kwasababu naamini Mbowe hahitaji kuhongwa cheo na wala hana njaa, ila atataka tu kufanikisha hilo kwa masilahi ya Taifa , namshauri asikubali nafasi hiyo ya uwaziri mkuu(in case atapewa) bali aongoze wenzake kumpendekeza kiongozi mwingine apewe hiyo nafasi iwapo CHADEMA wataridhia kuundwa serikali ya mseto huko mbeleni.

Mbowe akikubali nafasi hiyo itakuwa ni mwanzo wa propaganda chafu dhidi yake na chama chake kwa ujumla na hivyo chama watakidhoofisha.

Wengine tulishatabiri kuundwa kwa serikali ya aina hii katika zama hizi:


Pia soma hapa:
 

Attachments

  • Screenshot_20220626-132739_Twitter.jpg
    Screenshot_20220626-132739_Twitter.jpg
    64.4 KB · Views: 4
Mleta mada ni kwamba siyo kwamba serikali ya mseyo inaundwa leo ama kesho. Hapana.

Isipokuwa ni mapendekezo kwamba serikali ya mseyo iwekwe kwenye katiba inayopiganiwa sasa ili uchaguzi ujao mseto ndiyo utengenezwe
 
Mleta mada ni kwamba siyo kwamba serikali ya mseyo inaundwa leo ama kesho. Hapana.

Isipokuwa ni mapendekezo kwamba serikali ya mseyo iwekwe kwenye katiba inayopiganiwa sasa ili uchaguzi ujao mseto ndiyo utengenezwe
Hata mimi nafahamu hayo ni mapendekezo lakini tambua hilo teyari ni jambo limeshawekea mikakati na watawala. Kinachoendelea sasa ni formalities tu.
 
Serikali ya mseto haiji kwa hisani huwa inatokea pale ambapi hakuna chama chenye uwezo wa kuunda serikali baada ya uchaguzi.
 
Je Waziri Mkuu atakubali kuachia ngazi?
Siyo term hii, hiyo ni mipango ya next election, bila kuliandaa Taifa patachimbika.

Takwimu ziko wazi, watoto waliozaliwa mwaka 2005 uchaguzi unaokuja wanapiga kura, pata picha hawa wengi wao hawataki hata kuisikia ccm.
 
Serikali ya Mseto binafsi naiona haina maana hasa nikitazama mfano wa Zanzibar, wale wanaokaribishwa huko hugeuka mabubu, au waimba mapambio wa serikali.

Siasa zetu zimejaa wanasiasa maslahi sana.
 
Back
Top Bottom