Serikali ya CCM ni janga la taifa

Ndugu zangu watanzania nimekuwa nikijuuliza maswali mengi kuhusu huyu Mtu au Mfu anayetiwa[/COLOR] Kikwete, ingawa wengine wanamuiita Fisadi, Vasco Da Gama, christopher columbus, Mtalii na majina mengi ambayo wengi wenu mmekuwa mkimuita. Tangu achukuwe nchi 2005 na kupora nchi 2010 kumekuwa na malalamiko mengi tu kuhusu huyu bwana Kikwete kuwa ameiingiza nchi yetu kwenye matatizo mengi kama vile kashfa za Rushwa ambazo hata yeye anahusika na wizi wa kodi za Watanzani, Mikataba feki ya madini ambayo yanawanufaisha Wageni kuliko Wazawa na Taifa, Richimond & Dowans, EPA, KAGODA na majanga mengine yanayo iandama Nchi Yetu Nimekuwa nikijiuliza kuwa huyu KIKWETE NI JANGA LA TAIFA na kutuletea haya Matatizo yote halafu ni Jeuri anakebehi na kauli za kukejeli kwa wananchi, Speech zake zipo Hopeless kama yeye Mwenye alivyo. Kwa nini hajiuzulu? Nisaidieni wana JF:A S 13:

Please rekebisha hilo neno la blue. ni baya!!
 
as much as i would like to see JK go, i'd not support abusive words kama hilo neno jamaa ameli-highlight kwa blue color
 
kama unaangalia orijino komedi na unaelewa kwa nini mkwere humuelewi?
 
Ndugu zangu watanzania nimekuwa nikijuuliza maswali mengi kuhusu huyu Mtu au Mfu anayetiwa Kikwete, ingawa wengine wanamuiita Fisadi, Vasco Da Gama, christopher columbus, Mtalii na majina mengi ambayo wengi wenu mmekuwa mkimuita. Tangu achukuwe nchi 2005 na kupora nchi 2010 kumekuwa na malalamiko mengi tu kuhusu huyu bwana Kikwete kuwa ameiingiza nchi yetu kwenye matatizo mengi kama vile kashfa za Rushwa ambazo hata yeye anahusika na wizi wa kodi za Watanzani, Mikataba feki ya madini ambayo yanawanufaisha Wageni kuliko Wazawa na Taifa, Richimond & Dowans, EPA, KAGODA na majanga mengine yanayo iandama Nchi Yetu Nimekuwa nikijiuliza kuwa huyu KIKWETE NI JANGA LA TAIFA na kutuletea haya Matatizo yote halafu ni Jeuri anakebehi na kauli za kukejeli kwa wananchi, Speech zake zipo Hopeless kama yeye Mwenye alivyo. Kwa nini hajiuzulu? Nisaidieni wana JF:A S 13:

Wewe mwanaitelejensi edit hilo neno MFU haraka. Huku ni kukosa ustaarabu kwa binadamu mwenzako sembuse rais wa nchi. Kama ni hoja toa hoja yako kwa ustaarabu sio kwa maneno machafu.
 
Ndugu watanzania wenzangu,tukiwa tunakaribia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu,Miongoni mwa mambo yanayosababisha tushindwe kuendelea na serikali ya CCM na rais wetu ndugu JK aka mzee wa kuomba,mie nakuja na kauli mbiu kuwa JK NA CCM NI JANGA LA KITAIFA kama yalivyo majanga mengine kama vile mgao wa umeme,maradhi,ujinga na umaskini.Nchi yetu haiwezi kuendelea mpaka janga hili kuu la kitaifa tulipige vita.
 
Ndugu watanzania wenzangu,tukiwa tunakaribia kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu,Miongoni mwa mambo yanayosababisha tushindwe kuendelea na serikali ya CCM na rais wetu ndugu JK aka mzee wa kuomba,mie nakuja na kauli mbiu kuwa JK NA CCM NI JANGA LA KITAIFA kama yalivyo majanga mengine kama vile mgao wa umeme,maradhi,ujinga na umaskini.Nchi yetu haiwezi kuendelea mpaka janga hili kuu la kitaifa tulipige vita.
Hakuna Janga la utaifa hapo, sisiem na jk wake wanabakia kuwa janga la wanachama kwa wenzake wa chama chao. Ni wasaliti wa waasisi wa chama chao!
 
Decemba 9, 2011 Kama taifa tutakuwa tuna sheherekea miaka 50 ya uhuru, hii ni nusu Karne. Kuna nchi zimepata uhuru miaka ya karibuni zaidi kuliko sisi lakini ukiweka kwenye mizani na Tanzania sisi tuko nyuma kimaendeleo. Zaidi ya 40% ya watanzania wanapata mlo mmoja kwa siku, zaidi ya watanzania 60% hawa wanatumia kiwango cha chini ya USD 1 kwa siku. Vifo na maradhi kwa wakina mama wajawazito na watoto vinazidi kuongezeka kila siku, Malengo ya Millenium Development Goal (MDG) Kamwe hatutafikia labda kama juhudi za kuchakachua takwimu zitafanyika.

Umeme bado ni tatizo, hivi serikali inategemea itakuza uchumi kwa minajili hii ya gizani? Uzalishaji wa viwanja na sekata zote za uchumi zinadumaa. Kama kawaida tunapewa ahadi nyepesi na uwongo tunaridhika. Nimeangalia bunge ni usanii tu. Ni watanzania wenzetu wachache sana wanaweza kufikiri na kujua kwanini wako bungeni. Badala ya kuipa changamoto serikali imekuwa ni sehemu ya kupongezana na kutongozana kisiasa. Kiwango cha elimu kina shuka siku hadi siku. Wenye uwezo watoto wao wanasoma private school na baadaye wanasoma private universities nje ili warudi na elimu bora kuendeleaa kututawala.

Binafsi naona CCM ni janga la taifa hili, ili tuendelee basi ifike wakati basi wakubali wameturudisha nyuma sana. Nenda Kigali, Bunjumbura migao ya umeme ni historia, barabara kiwango cha lami. Miji haina foleni sababu miji hiyo imepangwa. Dar es Salaam ni aibu. Kuna siku Mch nimetoka Mlimani City kufika Millenium Tower imenichukua Masaa 3..ningeweza kwenda Morogoro na Kurudi sababu kubwa siku hiyo Mh alikuwa anakwenda fungua bara bara Mwenge ya kwenda Bagamoyo.


Kila siku ni ahadi, uwongo na uzembe unalelewa na hawa waliomadarakani, wamelewa kabisa na wako usingizini...majibu mepesi Tanzania inaendelea sana linganisha na wakati wa uhuru. Huu ni uchuro, wizi na ufisadi wa keki ya taifa uanatudumaza. Mgao wa umeme na foleni si wa CHADEMA, CCM, TLP, CUF, Waislam, Wakristu, mabohora na Pagan sote twaathirika. Jamani imetosha sasa Mzee Jakaya huwezi fanya maamuzi magumu pumzika tuanze upya kama taifa.Tumekuwa kama tumelogwa hatuwezi jadiliana kwa tija, ushabiki na ujinga. Soma michango ya wanaJF wengine ni aibu mtu anayejua tumia computer lakini hana fikira za kuchangia maendeleo ya nchi. Slogan za Tanzania ni nchi ya amani lakini maskini zimetuchosha.


CCM ni janga la taifa

Mch Masa K
 
Decemba 9, 2011 Kama taifa tutakuwa tuna sheherekea miaka 50 ya uhuru, hii ni nusu Karne. Kuna nchi zimepata uhuru miaka ya karibuni zaidikuliko sisi lakini ukiweka kwenye mizani na Tanzania sisi tuko nyuma kimaendeleo. Zaidi ya 40% ya watanzania wanapata mlo mmoja kwa siku, zaidi ya watanzania 60% hawa wanatumia kiwango cha chini ya USD 1 kwa siku. Vifo na maradhi kwa wakina mama wajawazito na watoto vinazidi kuongezeka kila siku, Malengo ya Millenium Development Goal (MDG) Kamwe hatutafikia labda kama juhudi za kuchakachua zitafanyika.

Umeme bado ni tatizo, hivi serikali inategemea itakuza uchumi kwa minajili hii ya gizani? Uzalishaji wa viwanja na sekata zote za uchumi zinadumaa. Kama kawaida tunapewa ahadi nyepesi na uwongo tunaridhika. Nimeangalia bunge ni usanii tu. Ni watanzania wenzetu wachache sana wanaweza kufikiri na kujua kwanini wako bungeni. Badala ya kuipa changamoto serikali imekuwa ni sehemu ya kupongezana na kutongozana kisiasa.

Binafsi naona CCM ni janga la taifa hili, ili tuendelee basi ifike wakati basi wakubali wameturudisha nyuma sana. Nenda Kigali, Bunjumbura migao ya umeme ni historia, barabara kiwango cha lami. Miji haina foleni sababu miji hiyo imepangwa. Dar es Salaam ni aibu. Kuna siku Mch nimetoka Mlimani City kufika Millenium Tower imenichukua Masaa 3..ningeweza kwenda Morogoro na Kurudi sababu kubwa siku hiyo Mh alikuwa anakwenda fungua bara bara Mwenge ya kwenda Bagamoyo.


Kila siku ni ahadi, uwongo na uzembe unalelewa na hawa waliomadarakani, wamelewa kabisa na wako usingizini...majibu mepesi Tanzania inaendelea sana linganisha na wakati wa uhuru. Huu ni uchuro, wizi na ufisadi wa keki ya taifa uanatudumaza. Mgao wa umeme na foleni si wa CHADEMA, CCM, TLP, CUF, Waislam, Wakristu, waislam, Pagan sote twaathirika. Jamani imetosha sasa Mzee Jakaya huwezi fanya maamuzi magumu pumzika tuanze upya kama taifa.Tumekuwa kama tumelogwa hatuwezi jadiliana kwa tija, ushabiki na ujinga. Soma michango ya wanaJF wengine ni aibu mtu anayejua tumia computer lakini hana fikira za kuchangia maendeleo ya nchi. Slogan za Tanzania ni nchi ya amani lakini maskini zimetuchosha.


CCM ni janga la taifa

Mch Masa K
Mchungaji umesomeka sana. Naomba unisaidie tofauti kwenye bold, naamini hujaandika kwa bahati mbaya. Otherwise "CCM ni janga kwa Taifa na bila kuiondoa madarakani hayo maisha bora na mafanikio ya miaka 50 ni pipe dream. Labda ni mafanikio kwa watu binafsi hasa mafisadi
 
Mchungaji umesomeka sana. Naomba unisaidie tofauti kwenye bold, naamini hujaandika kwa bahati mbaya. Otherwise "CCM ni janga kwa Taifa na bila kuiondoa madarakani hayo maisha bora na mafanikio ya miaka 50 ni pipe dream. Labda ni mafanikio kwa watu binafsi hasa mafisadi

Typing error

Maana yangu matatizo ya kijamii haya angalii itikadi wala dini. Kama taifa tusidanganywe na Khanga, kofia na chumvi. we need more than that. Ujinga na kutothubutu kwetu kuna tugharimu sana.
 
Masa,

Majanga makubwa ni uwajibikaji..........

Kwa mtu binafsi nakubaliana nalo! Ila serikali inafanya nini kuwezesha wananchi wake? Fatilia kwa karibu Issue ya BAE utaona uozo wa serikali kwenye kufikiria, Membe anatumia tumbo lake kufanya maamuzi. Angalia issue ya Umeme...nachoka kabisa Mzee wa Porojo alisema Mgao wa umeme utakuwa Historia, February mwaka huu Dodom akaropoka tena oooohhh mvua haikunyesha...hawajibiki huyu!
 
Typing error

Maana yangu matatizo ya kijamii haya angalii itikadi wala dini. Kama taifa tusidanganywe na Khanga, kofia na chumvi. we need more than that. Ujinga na kutothubutu kwetu kuna tugharimu sana.
Nimekupata Rev.
 
Hivi ina maana hakuna hata mmoja wa kuhamasisha mapinduzi ya kiraia? Jamani mimi msema hovyo nipo tayari kupiga domo nchi nzima kuwaambia watanzania tuipindue hii serikali ya wakoloni weusi.
 
Hii kero ya umeme nazidi mchukia Ngereja na CCM
Fellow, huna sababu ya kumchukia Ngeleja mkuu. Ngeleja ni kondoo wa kafara tu. Hana lolote analoweza kufanya kuokoa issue. Hapa tatizo kubwa ni Kikwete. Jamaa kila siku yupo kwenye ndege anazunguka kama pia lakini harudi na ufumbuzi wa matatizo ya watanzania.
Ila katika yote nawashangaa sana watanzania wanaoishabikia CCM napata hasira ya ajabu sana juu ya hawa watu. Maana inaonyesha kwamba hawa wenyetu hawaoni kabisa hizi shida tunazozipata.
 
Mchungaji vipi kikibadilishwa jina kutoka CCM kikaitwa jina lingine sema PDP bado litakuwa janga la Taifa?

Na vipi wanachama wengi wa CCM na watanzania wengi wakijiunga na Chadema kwa sasa unadhani bado itakuwa imara na bora kama tunavyoiona hivi sasa? Sema wabunge kama 50 wa CCM waame gafla na waikane CCM wajiunge na CDM na baada ya chaguzi ndogo CDM ichukue viti hivyo kupitia wabunge hao hao waliokimbia CCM!


Kama umesomea Tanzania, ebu vuta hisia wakati wa Migomo mkiwa wanafunzi ni asilimia ngapi walikuwa mende! wale vibaraka ambao wanaogopa kudai haki zao walikuwa wengi kuliko au wachache zaidi?


Ebu angalia hypothesisi zote tatu kama zinaweza ku-prove kuwa Watanzania wenyewe bado ni janga na hatima ya matatizo yanayowapata; kama hypothesis ita-prove hilo basi tumia kesi ya RA kushinda kwa kishindo Ubunge kama ushahidi na EL na hata ushindi wa Chenge.


Nasubiri analysis yako Rev; ukiona ni mada pana basi waweza kutoa kitabu labda!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom