Serikali ya CCM ni janga la taifa

Kwanini Bwawa la Mteraa..??
Kwani hilo bwawa ndio chanzo tu hapa TZ?
Kwanini wasiaangalie na Ziwa Victoria?
Na kwanini wasiangalie vyanzo vingine vya
Kuanzisha umeme kama Upepo..??
Hivi hawa viongozi wetu ni wameshindwa
kabisa kufikiria jinsi ya kukabiliana na hili
Tatizo la umeme au ndio vipi tena??

Kama hawataki kufikiria jinsi ya kutatua tatizo
La umeme kwanini wasiuzee sehemu ya TANESCO kwa
Watu au mashirika binafsi ???

Likija swali la umeme nina maswali kuliko majibu..
 
Kwanini Bwawa la Mteraa..??
Kwani hilo bwawa ndio chanzo tu hapa TZ?
Kwanini wasiaangalie na Ziwa Victoria?
Na kwanini wasiangalie vyanzo vingine vya
Kuanzisha umeme kama Upepo..??
Hivi hawa viongozi wetu ni wameshindwa
kabisa kufikiria jinsi ya kukabiliana na hili
Tatizo la umeme au ndio vipi tena??

Kama hawataki kufikiria jinsi ya kutatua tatizo
La umeme kwanini wasiuzee sehemu ya TANESCO kwa
Watu au mashirika binafsi ???

Likija swali la umeme nina maswali kuliko majibu..
kina ngereja ndio wanamiliki vituo vya mafuta na biashara ya majenereta.wat next u think?
 
Fellow, huna sababu ya kumchukia Ngeleja mkuu. Ngeleja ni kondoo wa kafara tu. Hana lolote analoweza kufanya kuokoa issue. Hapa tatizo kubwa ni Kikwete. Jamaa kila siku yupo kwenye ndege anazunguka kama pia lakini harudi na ufumbuzi wa matatizo ya watanzania.
Ila katika yote nawashangaa sana watanzania wanaoishabikia CCM napata hasira ya ajabu sana juu ya hawa watu. Maana inaonyesha kwamba hawa wenyetu hawaoni kabisa hizi shida tunazozipata.

hata hao wanaoshabikia CCM wanajua moyoni kwamba chama kishapoteza mwelekeo ila wanaganga njaa, chezea njaa wewe!!!!!
 
Kwa mtu binafsi nakubaliana nalo! Ila serikali inafanya nini kuwezesha wananchi wake? Fatilia kwa karibu Issue ya BAE utaona uozo wa serikali kwenye kufikiria, Membe anatumia tumbo lake kufanya maamuzi. Angalia issue ya Umeme...nachoka kabisa Mzee wa Porojo alisema Mgao wa umeme utakuwa Historia, February mwaka huu Dodom akaropoka tena oooohhh mvua haikunyesha...hawajibiki huyu!
kweli mkuu
Ngeleja anatumia utumbo mpana kufanya maamuzi
 
Bila watanzania kuamka usingizini tutazidi kulaumu hasi Yesu arudi.
 
Decemba 9, 2011 Kama taifa tutakuwa tuna sheherekea miaka 50 ya uhuru, hii ni nusu Karne. Kuna nchi zimepata uhuru miaka ya karibuni zaidi kuliko sisi lakini ukiweka kwenye mizani na Tanzania sisi tuko nyuma kimaendeleo. Zaidi ya 40% ya watanzania wanapata mlo mmoja kwa siku, zaidi ya watanzania 60% hawa wanatumia kiwango cha chini ya USD 1 kwa siku. Vifo na maradhi kwa wakina mama wajawazito na watoto vinazidi kuongezeka kila siku, Malengo ya Millenium Development Goal (MDG) Kamwe hatutafikia labda kama juhudi za kuchakachua takwimu zitafanyika.

Umeme bado ni tatizo, hivi serikali inategemea itakuza uchumi kwa minajili hii ya gizani? Uzalishaji wa viwanja na sekata zote za uchumi zinadumaa. Kama kawaida tunapewa ahadi nyepesi na uwongo tunaridhika. Nimeangalia bunge ni usanii tu. Ni watanzania wenzetu wachache sana wanaweza kufikiri na kujua kwanini wako bungeni. Badala ya kuipa changamoto serikali imekuwa ni sehemu ya kupongezana na kutongozana kisiasa. Kiwango cha elimu kina shuka siku hadi siku. Wenye uwezo watoto wao wanasoma private school na baadaye wanasoma private universities nje ili warudi na elimu bora kuendeleaa kututawala.

Binafsi naona CCM ni janga la taifa hili, ili tuendelee basi ifike wakati basi wakubali wameturudisha nyuma sana. Nenda Kigali, Bunjumbura migao ya umeme ni historia, barabara kiwango cha lami. Miji haina foleni sababu miji hiyo imepangwa. Dar es Salaam ni aibu. Kuna siku Mch nimetoka Mlimani City kufika Millenium Tower imenichukua Masaa 3..ningeweza kwenda Morogoro na Kurudi sababu kubwa siku hiyo Mh alikuwa anakwenda fungua bara bara Mwenge ya kwenda Bagamoyo.


Kila siku ni ahadi, uwongo na uzembe unalelewa na hawa waliomadarakani, wamelewa kabisa na wako usingizini...majibu mepesi Tanzania inaendelea sana linganisha na wakati wa uhuru. Huu ni uchuro, wizi na ufisadi wa keki ya taifa uanatudumaza. Mgao wa umeme na foleni si wa CHADEMA, CCM, TLP, CUF, Waislam, Wakristu, mabohora na Pagan sote twaathirika. Jamani imetosha sasa Mzee Jakaya huwezi fanya maamuzi magumu pumzika tuanze upya kama taifa.Tumekuwa kama tumelogwa hatuwezi jadiliana kwa tija, ushabiki na ujinga. Soma michango ya wanaJF wengine ni aibu mtu anayejua tumia computer lakini hana fikira za kuchangia maendeleo ya nchi. Slogan za Tanzania ni nchi ya amani lakini maskini zimetuchosha.


CCM ni janga la taifa

Mch Masa K

Hiyo kwenye nyekundu, sikubaliani na wewe, takwimu zinaonesha vifo vya kinamama na watoto chini ya miaka mitano vimepunguwa toka Kikwete aiingie madarakani.
 
Kero ya umeme na maisha magumu, halafu na kujisahau kwa wanasiasa na wabunge wa CCM kunanifanya nianze kuamini hawa jamaa wameamua kijifikisha mwisho wa kuongoza....they want to rest now and leave others to lead
 
Soma michango ya wanaJF wengine ni aibu mtu anayejua tumia computer lakini hana fikira za kuchangia maendeleo ya nchi. Slogan za Tanzania ni nchi ya amani lakini maskini zimetuchosha.


CCM ni janga la taifa

Mch Masa K

Hoja yako imenigusa sana Mch, lakini hapo penye bold, almanusura chozi linidondoke.

Yana mwisho mkuu
 
Kwa mtu binafsi nakubaliana nalo! Ila serikali inafanya nini kuwezesha wananchi wake? Fatilia kwa karibu Issue ya BAE utaona uozo wa serikali kwenye kufikiria, Membe anatumia tumbo lake kufanya maamuzi. Angalia issue ya Umeme...nachoka kabisa Mzee wa Porojo alisema Mgao wa umeme utakuwa Historia, February mwaka huu Dodom akaropoka tena oooohhh mvua haikunyesha...hawajibiki huyu!

Na jana wakati anafungua chuo cha mafunzo cha TANESCO, Membe kasema by August watakuwa wametatua tatizo....we are waiting
 
labda tuseme tu kuwa huenda taifa letu lina ulemavu, maana hata mtoto akifikisha miaka 2 au 3 hatembei au kutambaa, hiyo moja kwa moja ni kuwa mtoto huyo ni mlemavu, kwa hiyo huenda taifa letu lina ulemavu wa viongozi au wa maendeleo. mmmh! 50 years?????????????????
 
Kero ya umeme na maisha magumu, halafu na kujisahau kwa wanasiasa na wabunge wa CCM kunanifanya nianze kuamini hawa jamaa wameamua kijifikisha mwisho wa kuongoza....they want to rest now and leave others to lead

Unadhani wamejisahau mkuu au wanatekeleza 'majukumu' yao ipasavyo? Hebu jivike joho la kijani, uitwe mbunge pale mjengoni, alafu utuambie ungechangia kwa tofauti gani na wao...
 
Hiyo kwenye nyekundu, sikubaliani na wewe, takwimu zinaonesha vifo vya kinamama na watoto chini ya miaka mitano vimepunguwa toka Kikwete aiingie madarakani.

dada au siui mama au sijui ni bibi, achana na hizo habari za takwimu, ni za kisiasa, viongozi wa siku hizi wanategemea takwimu kuwalinda, nyerere pekee ndie alikuwa anataja wazi wazi majanga ya kitaifa, kwa mfano alikuwa anatambua janga la njaa na kulitatua, asaivi 50 years bado kuna watu wanakufa njaa na serikali inaficha, aibu hii.
 
Hiyo kwenye nyekundu, sikubaliani na wewe, takwimu zinaonesha vifo vya kinamama na watoto chini ya miaka mitano vimepunguwa toka Kikwete aiingie madarakani.

Kwa nijuavyo iliyopungua ni ratio (x/100,000 cases), lakini jumla ya wanaokufa imeongezeka. Kama una takwimu naziomba...
 
Unadhani wamejisahau mkuu au wanatekeleza 'majukumu' yao ipasavyo? Hebu jivike joho la kijani, uitwe mbunge pale mjengoni, alafu utuambie ungechangia kwa tofauti gani na wao...

yaap! nafikiri tatizo kubwa ni lile joho, joho lina laana lile, ama limeshakuwa kuukuu, tunahitaji kubadilisha joho jipya.
 
Kuna mambo ukiyatafakari waweza kujichukia mwenyewe. Ili twende hatua nyingine ni lazima sisi wenyewe tuamke na kufanya maamuzi japo magumu. Tukisubiri wanasiasa.........litatuchwea. Tumekuwa wapole sana na wepesi wa kulaumu........hizo nguvu tunazotumia kulaumu tukizihamishia kwenye vitendo tungekuwa mbali sana.
 
Mchungaji vipi kikibadilishwa jina kutoka CCM kikaitwa jina lingine sema PDP bado litakuwa janga la Taifa?

Na vipi wanachama wengi wa CCM na watanzania wengi wakijiunga na Chadema kwa sasa unadhani bado itakuwa imara na bora kama tunavyoiona hivi sasa? Sema wabunge kama 50 wa CCM waame gafla na waikane CCM wajiunge na CDM na baada ya chaguzi ndogo CDM ichukue viti hivyo kupitia wabunge hao hao waliokimbia CCM!


Kama umesomea Tanzania, ebu vuta hisia wakati wa Migomo mkiwa wanafunzi ni asilimia ngapi walikuwa mende! wale vibaraka ambao wanaogopa kudai haki zao walikuwa wengi kuliko au wachache zaidi?


Ebu angalia hypothesisi zote tatu kama zinaweza ku-prove kuwa Watanzania wenyewe bado ni janga na hatima ya matatizo yanayowapata; kama hypothesis ita-prove hilo basi tumia kesi ya RA kushinda kwa kishindo Ubunge kama ushahidi na EL na hata ushindi wa Chenge.


Nasubiri analysis yako Rev; ukiona ni mada pana basi waweza kutoa kitabu labda!.


Mkuu wa PLO

Suala ni si kuwa CHADEMA tu! Ninachokilalamika hapa ni hili la CCM kutufanya sisi Watanzania ujinga wetu uwe mtaji wao wa kuendesha mambo hovyo hovyo. Wabunge aina ya Shibuda wanastahili kubakia CCM ifike wakati tuvuke kutoka kwenye utani twende kwenye mambo ya msingi. Nimesomea Tanzania kwa ngazi zote, migomo ya chuo kikuu wale walikuwa na uwezo mdogo I mean wachechemeaji mara nyingi ndiyo walikuwa traitors, wakitishiwa watafukuzwa mara nyingi walikuwa wakiasi migomo. Vitisho vya kufukuzwa ilikuwa ni ngao kwa uongozi wa chuo. Lakini wale walikuwa wanajiamini walijua hata nikifukuzwa hapa nitaenda SUA ama MZumbe option zinakuwa nyingi. Watu hao hao kuja kwenye maisha ya kawaida ni waoga wanakuwa oppressed na wanaogopa poteza kazi zao na wananufaika na mfumo huu mbovu. Angalia hata wanaCCM wengi hapa JF hawawezi jenga hoja ni wababaishaji kwenye ufahamu wao.

Elimu ya uraia ni suluhisho kubwa, wengi sasa wanajiunga na mageuzi wakiwa na moyo wa kubadilisha na kuiondoa nchi mikononi mwa walafi wa CCM na vibaraka wao

Masa K
 
Back
Top Bottom