Serikali ya CCM kwa mara ya kwanza inaweza kukaribisha machafuko nchini

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Nimepita kwa watu kadhaa hasa sehemu za viwanda kwa walalahoi wengi, kuwadadisi juu ya swala la sheriha ya kutokutoa mafao mpaka umri wa kustafu kufika ya mifuko ya ifadhi ya Jamii, NSSF na kadhalika.

Watu wamekuwa na hasira sana na serikali. Wengi wakisema, liwalo na liwe.

Namuomba Rais, Wabunge na mamlaka zote zibadilishe sheria hii ili mifuko ya ifadhi ya jamii iwape elimu kwanza wafanyakazi ndio iwe sheria.
 
Elimu ya nini?Watatudanganya tu.Wao ndiyo wana uhakika wa kuishi hiyo miaka 55-60 kwa sababu wanamaisha mazuri.Asilimia kubwa kufikia miaka hiyo ni ndoto.Watupatie tu pesa zetu,mi sihitaji elimu kabisa hapo,nahisi naibiwa tu!
 
Sheria imepitishwa kimya kimya ili mifuko ya Jamii iendelee kubaki na pesa na kutumika kifisadi !!!
 
Kinacho niuma sana, kwa nini nilimpigia kura Rais Jakaya Kikwete. Bora ningelala tu nyumbani
 
Ukweli nikuwa wanaua huduma za afya kupunguza lifespan za wananchi ili malipo yao yayeyuke mifukoni mwao, its too bad!1 serikali huwezi ukasikia inasemea haya mambo ya lifespan za watu wake. Ni full usanii kwenda mbele, sijui ni nani huyo asiyewatakia wananchi wake afya njema ili waweze kudhalisha? Asiyejua kuwa wananchi wengi afya zao ni mgogoro? Ni nani asiyejua mfumko wa bei unawafanya watu waishi kwa kufanyia kazi matumbo yao bila kujiendeleza kipato?
 
Sheria imepitishwa kimya kimya ili mifuko ya Jamii iendelee kubaki na pesa na kutumika kifisadi !!!
Na ndiyo zitatumika kuwavalisha watu makofia, khanga na bendera za kijani!! Nchi hii imejaa vilaza kila kona, 60 years hapo hapo wenyewe wanakopeshana kwa masharti nafuu hata asipolipa sawa tu!!
 
Hii sheria ni kandamizi na haimtendei haki mtumishi, nashangaa walioipitisha walikuwa wanawaza nini.
 
kinacho niuma sana, kwa nini nilimpigia kura rais jakaya kikwete. Bora ningelala tu nyumbani

aaaah wenzio tulikosea mala ya kwanza wewe ukarudia tena aaaahh mkuu katubu na usirudie tena 2015
 
Huu ni wizi wa dhahiri na kuwanyima wananchi fursa za kujipatia maendeleo yao kutokana na jasho lao naomba serikali sikivu ya CCM iliangalie upya suala hili ili tupewe haki zetu mara tu ajira zetu zinapo koma

  • A%20S%20465.gif
    • A%20S%20465.gif
      A%20S%20465.gif

      • A%20S%20465.gif





 
Angalau umegundua kosa ulilofanya. Hopefully next time utajirekebisha!

Sitokipigia kura chama chochote, kwa sababu chadema ambao kidogo na waamini yaelekea wamenunulika kwahili. Wapo kimyaaaa!

 
Sitokipigia kura chama chochote, kwa sababu chadema ambao kidogo na waamini yaelekea wamenunulika kwahili. Wapo kimyaaaa!


Hata wakipiga kelele ni bure, kelele pekee haziwezi kuibadili sheria hii mbovu. Sheria hii itabadilishwa na serikali makini inayojua cha kufanya kwa maslahi ya wananchi. Kutopiga kura ni sawa na kutaka serikali dhaifu iendelee which means sheria hii tusiyoitaka iendelee pia. And that is the best case scenario, unajuaje kuwa serikali hii ya ccm haitatunga even worse law?
 
kwa hili ni muhimu kuandamana bila kuomba kibali cha polisi ccm, ili kuonesha hawawezi kutupelekesha wanavyo taka, wanataka pesa hii waitumie katika hongo wakati wa kampeni '15. maana wanajua siyo siri tene watu wakisikia jina CCM wanatamani kutapuika
 
Matokeo ya mashirika kukosa fedha, baada yakutumia fedha za michango ya wafanyakazi kwenye ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma, na matumizi mengine kama chaguzi kuwanufaisha CCM. Fursa pekee iliyopo ni kuiona CCM na serikali yake ilivyo uchi na dhulmati kwa kila mtu bila kujali.

LAKINI NDIVYO TULIVYOIWEKA MADARAKANI LICHA YA KUSHAURIWA SANA NA WANASIASA MAKINI
 
Back
Top Bottom