Dhamana iliyowekwa na mifuko ya hifadhi ya Jamii PSSSF/ NSSF kwenye Mikopo

DOMINGO THOMAS

JF-Expert Member
Feb 16, 2023
237
218
Hapa watumishi wengi watajua/wanajua wanachukua pesa walizo wekeza kwenye mfuko ( michango yao ya kwenye mfuko ) kitu ambacho sio sahihi.

Mifuko ilicho kifanya (Sheria mpya inavyo sema) michango yako iliyopo NSSF/PSSSF inatumika/itatumika kama dhamana ya mkopo, yani ukishindwa kulipa uo mkopo unao chukua bank mafao yako (michango yako) ndio itakuwa dhamana ya kulipa hilo deni (Mkopo). Na sio mfuko kutoa Mikopo kwa wanachama wake.

Kwa maana hiyo rejesho la lile deni (mkopo) ambao mtumishi ameuchukua bank, ambao dhamana yake ni michango yake iliyo kuwepo NSSF/PSSSF, haita katwa kwenye michango yake ambayo ipo kwenye mfuko NSSF/PSSSF bali itakatwa kwenye mshaara wake. Michango yake ipo kama dhamana tu, hii ni sawa kuwekea nyumba, gari au kiwanja dhamana ambapo ukishindwa kulipa deni dhamana yako ndio itachukuliwa.

Watumishi wakumbuke, Kazi ya mifuko ya hifadhi ya jamii sio kutoa mikopo. Lengo mama la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutuoa mafao. Mikopo ni kazi ya Financial institutions kama Mabank etc.

Naomba kuwasilisha.
 
Hii ni fursa ilonyimwa, yaani pesa yako mwenyewe iwe dhamana ya mkopo? Nguvu ya kukopa huyo mwajiriwa ataitoa wapi kama si kutegemea nguvu ya mshahara alonao mhusika? Kwa mishahara gani ama hii tayari inakatwa benki kwa mikopo!

Hii haina tofauti na kujitekenya kisha ucheke usiku wa manane. Kikubwa wapunguze umri wa kuweza kuchukua lile fao la 10% ambalo hutolewa ukifikisha miaka 56 tofauti na hapo ni kuwakebehi watumishi na kuwageuza mtaji wa siasa nyepesi
 
Hilo Fao la 10% lipo kwenye mfuko gani..!? ( Hakuna fao kama hilo kwasasa ).
 
Aisee kuna ticha jirani angu hapa alishaenda nmb kuulizia
Hajui kwamba hamna tofauti yyte na atalipa kila mwezi kupitia mshahara wake kama vile amekopa benki! Hiyo ni dhamana tu, kwahiyo kwa MTU mwenye ajira ambae tangu awali alikua anaweza kukopa benki hamna tofauti yoyote.
 
Hapa watumishi wengi watajua/wanajua wanachukua pesa walizo wekeza kwenye mfuko ( michango yao ya kwenye mfuko ) kitu ambacho sio sahihi.

Mifuko ilicho kifanya (Sheria mpya inavyo sema) michango yako iliyopo NSSF/PSSSF inatumika/itatumika kama dhamana ya mkopo, yani ukishindwa kulipa uo mkopo unao chukua bank mafao yako (michango yako) ndio itakuwa dhamana ya kulipa hilo deni (Mkopo). Na sio mfuko kutoa Mikopo kwa wanachama wake.

Kwa maana hiyo rejesho la lile deni (mkopo) ambao mtumishi ameuchukua bank, ambao dhamana yake ni michango yake iliyo kuwepo NSSF/PSSSF, haita katwa kwenye michango yake ambayo ipo kwenye mfuko NSSF/PSSSF bali itakatwa kwenye mshaara wake. Michango yake ipo kama dhamana tu, hii ni sawa kuwekea nyumba, gari au kiwanja dhamana ambapo ukishindwa kulipa deni dhamana yako ndio itachukuliwa.

Watumishi wakumbuke, Kazi ya mifuko ya hifadhi ya jamii sio kutoa mikopo. Lengo mama la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kutuoa mafao. Mikopo ni kazi ya Financial institutions kama Mabank etc.

Naomba kuwasilisha.
Kwa mantiki hiyo mtumishi ambaye amefikia kiwango cha mwisho ktk makato yake benkihataweza bado kukopa kwa dhamana hii?
 
Back
Top Bottom