Serikali sasa ijifunze toka Tigo kwa wanaovujisha siri zake nje

Huyu jamaa sijaelewa kama ni mzima wa akili au mgonjwa. Hivi ukiwa support tigo kufukuza wafanyakazi wake kwa kutoa siri una maana ipi?. Inaonyesha hajui hata upelelezi unafanyika vipi. TUMHURUMIE.
 
Ina maana Tigo pia wameshiriki kumvamia Ben Nyumbani kwake na kumtendea kinyume na maadili mke wake na si Serikali!
 
Harafu wewe usiwe ***** unaonekana sana kushabikia chama cha magamba subirini 2015 kitaeleweka.sapor
KUFUNGIWA kwa gazeti la MwanaHalisi, Jumatatu ya wiki iliyopita kumekwenda sambamba na kuwatambua na kufukuzwa kazi kwa maofisa 31 wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Tanzania jijini Dar es Salaam.

Katika toleo lake la mwisho wiki mbili zilizopita, gazeti hilo linatuhumiwa kuandika habari ya uchochezi dhidi ya serikali kwa kuichafua Idara ya Usalama wa Taifa, uchonganishi na ugombanishi kwa watu huku pia likihatarisha maisha kati yao kwa kuwatuhumu kuhusika na utekaji nyara, utesaji wa kikatili na jaribio la kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka Juni 26, mwaka huu.

Sitaki kurejea habari hiyo wala kukumbushia machungu ya unyama aliofanyiwa daktari huyo hasa kwa vile suala hilo lenyewe linashughulikiwa na vyombo vya dola, halafu kuna kesi inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya mmoja kati ya watu wanaodaiwa kufanya ukatili huo kutiwa mbaroni mwezi uliopita.

Ninachotaka kuzungumzia hapa ni hatua iliyochukuliwa na kampuni ya Tigo ya kuwatimua kazi mara moja baadhi ya maofisa wake, wale ambao wanadaiwa kutoa nje siri za wateja wa mwajiri huyo kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

Wanatuhumiwa kuvujisha siri za mawasiliano yaliyofanywa na baadhi ya wateja wake na Ulimboka kwa gazeti hilo ikiwemo kutoa namba za simu zao, muda waliowasiliana naye kwa namna moja ama nyingine na majina yao, kisha wakahusishwa na madai ya kumteka, kumtesa, kujaribu kumuua na kumtelekeza katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Tumesikia kelele nyingi zilizopigwa kijinga na baadhi ya watu wakiishutumu serikali kwa kulifungia gazeti hilo. Tumeona baadhi yao wanavyokwenda mbali zaidi kwa kutaka ilifungulie, wengine wakisema ifanye hivyo “mara moja na bila masharti yoyote” kwa madai kuwa adhabu hiyo ni ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari nchini.

Wanazungumza kipuuzi kwa kauli za kijinga dhidi ya mamlaka halali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanajifanya eti hawafahamu kuwa vyombo vyote vya habari vinaendesha majukumu yake siyo kwa ridhaa zake vyenyewe isipokuwa kwa matakwa ya kisheria bila ya kujali kama ni mbovu kama wanavyodai na hata vinginevyo.

Magazeti yote nchini yanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, ileile inayopigiwa kelele nyingi ikisemwa imeshapitwa na wakati na kandamizi, lakini ileile na vilevile inapotumika kusajilia magazeti hakuna anayedai au kusema kuwa ni kandamizi ama kwamba inatakiwa ibadilishwe.

Udikteta wa sheria hiyo na maneno mengine ya shutuma dhidi yake unakuja tu wakati gazeti linapochukuliwa hatua zote halali za kisheria na serikali ikiwemo kuonywa, kufungiwa au kufutwa kabisa kutoka kwenye orodha ya magazeti pindi linapokwenda kinyume cha weledi pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

Hapo ndipo kelele zinapoanza kutoka midomoni mwa baadhi ya watu wakiongozwa zaidi na wanasiasa na wanaharakati nchini, wote wakifanya hivyo siyo kwa nia njema isipokuwa kwa ujinga wa kutumiwa na magenge yanayoitwa wahisani na wafadhili kutoka nje ya nchi.

Wanafanya hivyo kwa kutaka kuivuruga serikali ili ishindwe kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kile ambacho katika ujumla wao wanapenda kiondoshwe madarakani mwaka 2015 huku chaguo lao hivi sasa likiwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachotaka kuleta ushoga nchini!

Nikirudi katika maudhui hasa ya makala yangu hii, napenda kuipongeza kampuni ya Tigo Tanzania ilivyochukua hatua za haraka kuwawajibisha watumishi wake kwa kuvujisha nje siri za wateja wake, jambo linaloweza kusababisha watu wengi waikimbie na kujiunga na mitandao mingine ya simu maana ipo mingi na tayari ushindani miongoni mwa makampuni hayo ni mkubwa kupindukia.

Tayari kuna kampuni mbalimbali zikiwemo kubwa za Vodacom, Airtel na Zantel huku nyingine zikianzishwa na kuingia sokoni, jambo ambalo litaongeza ushindani ambao ni pamoja na uaminifu, uadilifu, unyenyekevu; nafuu ya gharama za kupiga, kupokea ama kutumia ujumbe mfupi wa maneno na ubora wa mawasiliano kwa wateja wake.

Haiwezekani mwajiri aendelee kuwakumbatia watumishi waliokosa uaminifu na kufikia mpaka hatua ya kutoa nje siri za wateja wake ambao kimsingi uwepo wao ndio maisha yao ya kila siku, familia zao na ndugu zao wenyewe, lakini wanakuwa na ujinga wa kutumiwa na waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati kutenda kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

Sifahamu endapo kampuni hiyo ina utaratibu wa kuapisha watumishi wake iwe kwa mdomo au maandishi na kumbukumbu hizo kuhifadhiwa, lakini hata iweje ni ujinga na kinyume cha utumishi mahali popote duniani kwa mfanyakazi awe wa ndani au shambani kutangaza kitu chochote kinachofanywa na mwajiri mahali popote bila idhini yake mwenyewe.

Kama jambo hilo lingekuwa halina tatizo hakika wafanyakazi wenye mchezo huo wa ovyo wangekuwa wanavujisha kwanza siri zao wenyewe na wake zao nyumbani, waume zao au wapenzi wao, vinginevyo wangekuwa wanaeleza wanavyokiuka sheria na kanuni za ajira zao kwa hujuma zote wanazofanya.

Kila wakivujisha nyaraka zisizotakiwa kutoka nje ya ofisi au kwa watu wasiotakiwa siku zote wangekuwa wanatangaza walichofanya, lakini hawafanyi hivyo kwa vile wanaelewa kuwa hairuhusiwi katika hali zote na hilo ni kosa la jinai kwa sheria zote za kazi.

Ndiyo maana naipongeza kampuni hiyo kwa kuwachukulia hatua za haraka kuwang’oa na kuachana nao mara moja. Naishukuru kwa sababu imetimiza wajibu wake halali unaopaswa kufanywa na waajiri wote duniani kuanzia sekta binafsi hadi za umma ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mchezo wa kuvujisha siri za ofisi sehemu za kazi umegeuzwa kuwa mchezo wa kawaida kuanzia wizarani hadi bungeni, taasisi za fedha na idara takribani zote za serikali.

Leo utasikia “nyaraka tulizonazo” au “habari za ndani zilizopatikana kutoka” wizara hiyo, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na kadhalika.

Huko ndiko zinakotoka siri nyingi za serikali na kuangukia mikononi mwa wanaharakati wa masuala ya kijamii ingawa ukweli ni wanaharakati wa kisiasa, viongozi wa vyama vya siasa na makundi mengine yakiwemo haramu.

Ndiyo maana kwa mfano haishangazi kusikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa au Mwenyekiti wake, Freeman Aikaeli Mbowe wakitamba kukamata nyaraka za serikali na kuongeza uongo na uzushi juu yake.

Wanadai nyaraka hizo ni maelekezo maalum ya serikali kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa, Miji na Wilaya ya kuwashughulikia wapinzani huku wakijua ni uongo ila wanafanya hivyo kwa malengo ya kisiasa na kupotosha ukweli.

Wanatumia nyaraka hizo kufanya uchochezi kwa nia ovu, uchonganishi na ugombanishi ili wananchi waichukie serikali yao na CCM kwa kuwapandikizia majungu, uzushi na fitina zote wanazoweza kuzifanya wakati wowote na mahali popote.

Bila kujifunza kutoka kampuni ya Tigo na kuanza kuwafuatilia watumishi wote wa serikali na taasisi zake wanaovujisha nje siri za ndani ikiwemo kudurufu nyaraka, kuwakabidhi wanasiasa au watu wengine kinyume cha sheria na kanuni za ajira, kisha kuwatimua kazi na tena kwa haraka na kupoteza haki zao zote kamwe hawawezi kukoma.

Hiyo ndiyo kazi inayopaswa ianze sasa na kusimamiwa moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
 
Registration ya namba za simu si ndio matumizi yake haya, sasa kwa nini wafukuzwe? Hawakujua kama ku-register simu ingekula na kwao?!

Hapana!! Si kwa ajili ya kutoa habari za wateja kwa mtu yo yote. Sijui sheria za Tanzania, lakini nchi kama Marekani kunakodaiwa kuwa na demokrasia na uhuru,ili kupata taarifa toka kwenye kampuni za simu au kiintelegisia lazima kupitia vyombo vya kisheria. Kufukuzwa kwa watumishi hawa haitoshi, lazima Tume ya Mawasiliano nayo ichukuliwe hatua kwa kampuni ya simu husika, nashangaa kwa hili imekaa kimya.

Halafu mtumaji wa taarifa hii amechanganya mambo kiasi cha kufanya uchangiaje uelekezwe kwingine au amefanya kufukuzwa kwa wafanyakazi kuwe entry point ya mambo mengine aliyoelezea na kutoa dukuduku lake.
 
Pengine ungekuwa neutral ungesimama ktk point uliyolenga, maskini umetumia muda mwingi kuandika lihabari lireefu tahamaki! Ukajikuta umepoteza mantiki kwa wivu na chuki za kisiasa ulizo nazo! Labda ungeishauri serikali kurudisha mfumo wa chama kimoja chini ya sera za zidumu fikra za mwenyekiti huenda hayo yangefanikiwa! Ila kwa dunia ya leo hizo ni ndoto za alinacha! Labda nikuulize kidogo, bila wapinzani kufichua ufisadi wa epa, richmond na nanii na nanii, ulitarajia kuyajua hayo kupitia nini?
 
Huyu jamaa sijaelewa kama ni mzima wa akili au mgonjwa. Hivi ukiwa support tigo kufukuza wafanyakazi wake kwa kutoa siri una maana ipi?. Inaonyesha hajui hata upelelezi unafanyika vipi. TUMHURUMIE.

Wewe binafsi unapenda kupelelezwa? Siri zako zikitolewa hadharani utamkumbatia aliyetoa siri zako? Angalia pande zote mbili. Wao ni wafanya biashara wasingependa siri za wateja wao zitoke nje kwa namna yo yote hiyo kwani inaathiri biashara. Na mimi Tigo kwa sasa bye bye!!!!
 
KUFUNGIWA kwa gazeti la MwanaHalisi, Jumatatu ya wiki iliyopita kumekwenda sambamba na kuwatambua na kufukuzwa kazi kwa maofisa 31 wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Tanzania jijini Dar es Salaam.

Katika toleo lake la mwisho wiki mbili zilizopita, gazeti hilo linatuhumiwa kuandika habari ya uchochezi dhidi ya serikali kwa kuichafua Idara ya Usalama wa Taifa, uchonganishi na ugombanishi kwa watu huku pia likihatarisha maisha kati yao kwa kuwatuhumu kuhusika na utekaji nyara, utesaji wa kikatili na jaribio la kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka Juni 26, mwaka huu.

Sitaki kurejea habari hiyo wala kukumbushia machungu ya unyama aliofanyiwa daktari huyo hasa kwa vile suala hilo lenyewe linashughulikiwa na vyombo vya dola, halafu kuna kesi inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya mmoja kati ya watu wanaodaiwa kufanya ukatili huo kutiwa mbaroni mwezi uliopita.

Ninachotaka kuzungumzia hapa ni hatua iliyochukuliwa na kampuni ya Tigo ya kuwatimua kazi mara moja baadhi ya maofisa wake, wale ambao wanadaiwa kutoa nje siri za wateja wa mwajiri huyo kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

Wanatuhumiwa kuvujisha siri za mawasiliano yaliyofanywa na baadhi ya wateja wake na Ulimboka kwa gazeti hilo ikiwemo kutoa namba za simu zao, muda waliowasiliana naye kwa namna moja ama nyingine na majina yao, kisha wakahusishwa na madai ya kumteka, kumtesa, kujaribu kumuua na kumtelekeza katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Tumesikia kelele nyingi zilizopigwa kijinga na baadhi ya watu wakiishutumu serikali kwa kulifungia gazeti hilo. Tumeona baadhi yao wanavyokwenda mbali zaidi kwa kutaka ilifungulie, wengine wakisema ifanye hivyo “mara moja na bila masharti yoyote” kwa madai kuwa adhabu hiyo ni ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari nchini.

Wanazungumza kipuuzi kwa kauli za kijinga dhidi ya mamlaka halali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanajifanya eti hawafahamu kuwa vyombo vyote vya habari vinaendesha majukumu yake siyo kwa ridhaa zake vyenyewe isipokuwa kwa matakwa ya kisheria bila ya kujali kama ni mbovu kama wanavyodai na hata vinginevyo.

Magazeti yote nchini yanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, ileile inayopigiwa kelele nyingi ikisemwa imeshapitwa na wakati na kandamizi, lakini ileile na vilevile inapotumika kusajilia magazeti hakuna anayedai au kusema kuwa ni kandamizi ama kwamba inatakiwa ibadilishwe.

Udikteta wa sheria hiyo na maneno mengine ya shutuma dhidi yake unakuja tu wakati gazeti linapochukuliwa hatua zote halali za kisheria na serikali ikiwemo kuonywa, kufungiwa au kufutwa kabisa kutoka kwenye orodha ya magazeti pindi linapokwenda kinyume cha weledi pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

Hapo ndipo kelele zinapoanza kutoka midomoni mwa baadhi ya watu wakiongozwa zaidi na wanasiasa na wanaharakati nchini, wote wakifanya hivyo siyo kwa nia njema isipokuwa kwa ujinga wa kutumiwa na magenge yanayoitwa wahisani na wafadhili kutoka nje ya nchi.

Wanafanya hivyo kwa kutaka kuivuruga serikali ili ishindwe kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kile ambacho katika ujumla wao wanapenda kiondoshwe madarakani mwaka 2015 huku chaguo lao hivi sasa likiwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachotaka kuleta ushoga nchini!

Nikirudi katika maudhui hasa ya makala yangu hii, napenda kuipongeza kampuni ya Tigo Tanzania ilivyochukua hatua za haraka kuwawajibisha watumishi wake kwa kuvujisha nje siri za wateja wake, jambo linaloweza kusababisha watu wengi waikimbie na kujiunga na mitandao mingine ya simu maana ipo mingi na tayari ushindani miongoni mwa makampuni hayo ni mkubwa kupindukia.

Tayari kuna kampuni mbalimbali zikiwemo kubwa za Vodacom, Airtel na Zantel huku nyingine zikianzishwa na kuingia sokoni, jambo ambalo litaongeza ushindani ambao ni pamoja na uaminifu, uadilifu, unyenyekevu; nafuu ya gharama za kupiga, kupokea ama kutumia ujumbe mfupi wa maneno na ubora wa mawasiliano kwa wateja wake.

Haiwezekani mwajiri aendelee kuwakumbatia watumishi waliokosa uaminifu na kufikia mpaka hatua ya kutoa nje siri za wateja wake ambao kimsingi uwepo wao ndio maisha yao ya kila siku, familia zao na ndugu zao wenyewe, lakini wanakuwa na ujinga wa kutumiwa na waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati kutenda kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

Sifahamu endapo kampuni hiyo ina utaratibu wa kuapisha watumishi wake iwe kwa mdomo au maandishi na kumbukumbu hizo kuhifadhiwa, lakini hata iweje ni ujinga na kinyume cha utumishi mahali popote duniani kwa mfanyakazi awe wa ndani au shambani kutangaza kitu chochote kinachofanywa na mwajiri mahali popote bila idhini yake mwenyewe.

Kama jambo hilo lingekuwa halina tatizo hakika wafanyakazi wenye mchezo huo wa ovyo wangekuwa wanavujisha kwanza siri zao wenyewe na wake zao nyumbani, waume zao au wapenzi wao, vinginevyo wangekuwa wanaeleza wanavyokiuka sheria na kanuni za ajira zao kwa hujuma zote wanazofanya.

Kila wakivujisha nyaraka zisizotakiwa kutoka nje ya ofisi au kwa watu wasiotakiwa siku zote wangekuwa wanatangaza walichofanya, lakini hawafanyi hivyo kwa vile wanaelewa kuwa hairuhusiwi katika hali zote na hilo ni kosa la jinai kwa sheria zote za kazi.

Ndiyo maana naipongeza kampuni hiyo kwa kuwachukulia hatua za haraka kuwang’oa na kuachana nao mara moja. Naishukuru kwa sababu imetimiza wajibu wake halali unaopaswa kufanywa na waajiri wote duniani kuanzia sekta binafsi hadi za umma ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mchezo wa kuvujisha siri za ofisi sehemu za kazi umegeuzwa kuwa mchezo wa kawaida kuanzia wizarani hadi bungeni, taasisi za fedha na idara takribani zote za serikali.

Leo utasikia “nyaraka tulizonazo” au “habari za ndani zilizopatikana kutoka” wizara hiyo, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na kadhalika.

Huko ndiko zinakotoka siri nyingi za serikali na kuangukia mikononi mwa wanaharakati wa masuala ya kijamii ingawa ukweli ni wanaharakati wa kisiasa, viongozi wa vyama vya siasa na makundi mengine yakiwemo haramu.

Ndiyo maana kwa mfano haishangazi kusikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa au Mwenyekiti wake, Freeman Aikaeli Mbowe wakitamba kukamata nyaraka za serikali na kuongeza uongo na uzushi juu yake.

Wanadai nyaraka hizo ni maelekezo maalum ya serikali kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa, Miji na Wilaya ya kuwashughulikia wapinzani huku wakijua ni uongo ila wanafanya hivyo kwa malengo ya kisiasa na kupotosha ukweli.

Wanatumia nyaraka hizo kufanya uchochezi kwa nia ovu, uchonganishi na ugombanishi ili wananchi waichukie serikali yao na CCM kwa kuwapandikizia majungu, uzushi na fitina zote wanazoweza kuzifanya wakati wowote na mahali popote.

Bila kujifunza kutoka kampuni ya Tigo na kuanza kuwafuatilia watumishi wote wa serikali na taasisi zake wanaovujisha nje siri za ndani ikiwemo kudurufu nyaraka, kuwakabidhi wanasiasa au watu wengine kinyume cha sheria na kanuni za ajira, kisha kuwatimua kazi na tena kwa haraka na kupoteza haki zao zote kamwe hawawezi kukoma.

Hiyo ndiyo kazi inayopaswa ianze sasa na kusimamiwa moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.

We mbwa tu mlamba makombo ya bwana zako watawala ! shwainiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii !?
 
Serikali ni ya kishenzi sana coz ninachojua kuhusu upelelezi hasa katika tuhuma kama hizi ni kua mlolongo wa mawasiliano ya Dr. Ulimboka ni chanzo cha kuwapata watekaji.Ilichokifanya MwanaHalisi ni kutoa habari za kiuchunguzi ambazo serikali imeona ni kuchochea ila ni kua wamewafichua watekaji kutoka Ikulu.
 
security guard tatizo la watu wengi hawajui sheria ya magazeti. Mimi nathubutu kusema kwamba serikali ikiamua kutumia sheria hiyo basi asilimia kubwa ya magazeti yatafungiwa. Huenda tukarudi kwenye Uhuru na MZalendo. Ndiriki kusema serikali imekuwa na huruma juu ya magazeti mengi. Magazeti yanaandika habari ambazo kwa mujibu wa sheria ni uchochezi. Badala ya kupigania sheria ibadilike wao wanaishia kusema serikali isifungie magazeti; kwa kauli nyepesi ni kwamba serikali isitekeleze sheria.

Common sense ni zaidi ya sheria, mbona watu wanahukumiwa kunyongwa na wanaotakiwa kutia sahihi hawatii ili wanyongwe ? akili yako inajua sheria ya magazeti tu na si sheria zingine? vipi kuhusu ziwa malawa a.k.a ziwa Nyasa una maana kwa kuwepo kwa mkataba wa kisheria unaopingana na ukweli basi sisi watz tusubili huruma ya Mungu walioko pwani ya ziwa kupata maji ? binadam wengine mkoje ? Sheria isiwe badala ya ubongo wako amka pigania haki yako wao ndiyo ikiwapain wakabadilishe hiyo sheria ya kishenzi,SIMAMA PIGANIA HAKI YAKO USIJALI WAO WAMEJIWEKEA KINGA GANI KISHERIA ZAO WENYEWE,HIYO NI SHERIA YA WAKATI WA UKOMUST/AUJAMAA UKIWA UMETAMALIKI TZ,MTU MZIMA BADO UNAISHABIKIA NA KUIONA KAMA NDIYO REJEA KWA UPUMBAVU WA WATAWALA. AMKA USICHAGULIWE NINI CHA KUSOMA,UHURU KWA KUFIKIRI KWA KILA BINADAM HAUNA MIPAKA,hivyo basi wao waache watu waandike then sisi wasomaji tutatumia uhuru wetu wa kufikiri kujua ipi pumba na upi ni ukweli. Mwanahalisi wametaja mtu na namba yake ya simu,mtu husika anatakiwa aibuke alippo au hao aliowasiliana nao waibuke wasema namna ambavyo mawasiliano yao yalikuwa nje ya uhalifu unaozungumziwa na kama hawataki waendae mahakamani,lakini si swala la wapuuzi kuamua upuuzi kul;ifungia gazeti ana kufukuza wafanyakazi kwenye makampuni ya simu. anyaway najua TUPO BINADAMU TULIOUMBWA NA MUNGU NA BINADAMU WENGINE WA EVOLUTION labda evolution bado haijakamilika kufikia ubinadam kama wetu. ACHA KUSHABIKIA MAOVU KWA KUREJEA SHERIA ZA KULINDA UOVU.
 
Kuvujishw kwa siri hizo ambazo ni muhimu ili haki ifanyike ni ujasri. Tunawataka sasa wafanyakazi hao wavujishe pia jinsi makampuni ya simu yanavyohujumu uchumi kwa kutotota taarifa sahihi za mapato ya vat kwa mauzo ya LKU, M- NA TIGO PESA etc wasiogope. Wakumbuke uzalendo aliofanya yule nfanayakazi wa benki moja ya uswisi kuhusu wakwepa kodi wa Ujerumani. Ndio kazi wamekosa lakini ushujaa na uzalendo wao utathaminiwa na wapenda Tanganyika
 
What a Shallow oppinion!
Yaani nimepata hadi hasira naweza kupata BAN hapa kwa ajili yako. Kwa ufupi sana mchango wangu ni huu:
1. Nakuombea Mungu yakukute wewe mwenyewe au wanao na atokee kiumbemaji mwingine kama wewe aandike hivi hivi na ufanikiwe kusoma.
2. Hizo unazodai kuwa ni 'Siri za Serikali' zinafichuliwa kama ni nzuri kwanini zifichuliwe? Makosa ni makosa tu haijalishi ni nani aliyeyatenda! Serikali haina uhalali wala mamlaka ya kufanya mambo kinyume kinyume halafu eti 'Wafanyakazi wawe wazalendo' kulinda uozo!..
3. Naomba kujua kama unatumia kifaa gani kufikiri.
 
Wewe binafsi unapenda kupelelezwa? Siri zako zikitolewa hadharani utamkumbatia aliyetoa siri zako? Angalia pande zote mbili. Wao ni wafanya biashara wasingependa siri za wateja wao zitoke nje kwa namna yo yote hiyo kwani inaathiri biashara. Na mimi Tigo kwa sasa bye bye!!!!

Sasa kama ndo hivyo Logic kusajili line ilikuwa ni nini kama mtu anaweza kufanya maovu kupitia simu yake asichunguzwe eti 'Kwakuwa ilikuwa ni siri yake'?.. Siri ina mipaka!
 
Mkuu Nkwesa Makambo tunapigania utawala wa sheria. Najua unafahamu ni nini maana ya utawala wa sheria. Huwezi kusema tuwe na utawala wa sheria bila kuwa na sheria ambazo si kandamizi. Inabidi sheria ziwe fair ndio kuwe na utawala wa sheria. Unakumbuka kuwa Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza kufutwa kwa sheria 40 ambazo tume yake iliziona ni kandamizi? Tume iliona kuwa ili kuwe na utangamano inabidi sheria hizo zifutwe. Mojawapo ya sheria hizo no sheria ya magazeti na sheria ya usalama wa taifa. Hizo hazijafutwa na ndizo zimetumika kulifungia gazeti. Kama zingebadilishwa ama kufutwa nadhani tusingekuwa hapa.Muhimu ni sheria kandamizi kufutwa badala ya kusema tu ni za kijamaa wakati ndizo zintumika kuhukumu.
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada nimekupata tatizo lako moja maslahii so ni vyema kuyalinda lakini sheria ipo kwa ajili ya pande zote bila kujali ni mazingira yaliopo kwa wakati huo lakini sheria haiko kulinda walifu,dhuluma nk but ipo kulinda haki na uhuru wa mawazo kwa kila mwenye kulitaka kulisema, nataka nikujuze kidogo marekani kuna uhuru mkubwa wamawazo kuliko nchi yeyote ile hapa duniani pia swala la kialifu kwa binadamu likitokea limegusa watu wengi basi kisheria maamuzi yanatakiwa kusikilizwa kwa kunzingatia manufaa ya watu mfano. swala osama bin laden kesi yake ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu limegusa watu wengi sana hivyo kifo chake ni stahili kisheria na swala la utekaji nyara kwa dk ulimboka limegusa interest za watu wengi hivyo basi ili kulinda haki yake kikatiba yani ya kuishi, kuabudu , kusema kwa manufaa ya wengi wadhalimu wale walistahili kuwekwa au kutambuliwa na kufikishwa mahakamani kwa manufaa ya wengi ili kulinda usalama wa nchii kutoka kwa mwajili wa serikali yani wananchii ,mfn kesi ya kikatiba mtikila vs serikali mahakama iliona ili kuyalinda manufaa ya wengi au watanzania wengi ili kuepusha mgongano kati ya serikali na wananchii basi ni vyema swala mgombea binafsi lilejeshwe kwa wawakilishi halali wa wananchii yani bunge au wabunge kwa kutumia hekima watoe mamuzi kwa manufaa ya wwakilishi wao.tigo wamelinda maslahii yao kisheria selikali ilitakiwa kwenda kuchukua taarifa za kipelelezi kujua mawasiliano yaliopo kati ya dk ulimboka na watuhumiwa mapema kabisa ili kuweka wazi kwa umma kusudi kuondoa sintofahamu, na hivyo hivyo kwa gazeti la uchunguzi la mwana halisi lilitakiwa kuomba taarifa halali za mawasiliano kti ya dk. stevin na mtuhumiwa ili umma utoe Hukumu kwani hukumu ya umma ndio yenye nguvu na msingi huo basi umma ndio mwamuzi wa mwisho juu ya mambo ya sitofahamu ndani ya serikali maamuzi ya maandamano ya umma yanaweka wazi kuchoka kwa utwala wa kimabavu,dhuluma na haki ya msingi kabisa ya kuishi, nimeeleza kilefu kwa kiswahili,na kutumia lugha ya kisheria zaidi na kasolo za lugha pia. naomba mwenye kuweka gepu au kukosoa atekeleze kwa manufaa ya wengi.
 
Back
Top Bottom