Serikali sasa ijifunze toka Tigo kwa wanaovujisha siri zake nje

kila serikali au makampuni duniani kuanzia marekani mpaka china...kunakuaga na vyanzo vya habari vya ndani hilo ni kitu cha kawaida...sasa sijui mnachoshangaa ni nini...america na intelligence yake yote ile lakini bado habari kutoka CIA FBI na WHITE HOUSE zinavuja...ndio itakuja kua TIGO/USALAMA MBOVU WA TAIFA?

Waambie Mkuu, wakamuulize Weakleaks!!! Na ile suti alibambua pia. Juzi Jumamosi/Jumapili Website ya Wizara ya Afya ilikuwa hacked. Hao ndo akina nanai walifanya? Wameshachukua info zote muhimu sembuse tiGo. Leo hii nikitaka tu kufahamu hawara wa mke/mume just send 1,000 mpesa or Tigo Pesa japo inawezekana watu kusajili magumashi but your get it real at 80% though!!! Sasa shida iko wapi? Eti Simu, hopeless kabisa.
 
Kutoa siri za mteja ni kitu hatari nadhani kama ni kweli Tigo wamefanya sahihi.

VIjana wasio waaminifu kama hao wanaweza hata kuvunja ndoa za watu bora wafukuzwe tu.

Is it the 1st time kwako kusikia ndoa imevunjika????
Ucjali utakuwa tu.
 
security guard tatizo la watu wengi hawajui sheria ya magazeti. Mimi nathubutu kusema kwamba serikali ikiamua kutumia sheria hiyo basi asilimia kubwa ya magazeti yatafungiwa. Huenda tukarudi kwenye Uhuru na MZalendo. Ndiriki kusema serikali imekuwa na huruma juu ya magazeti mengi. Magazeti yanaandika habari ambazo kwa mujibu wa sheria ni uchochezi. Badala ya kupigania sheria ibadilike wao wanaishia kusema serikali isifungie magazeti; kwa kauli nyepesi ni kwamba serikali isitekeleze sheria.
 
Last edited by a moderator:
security guard tatizo la watu wengi hawajui sheria ya magazeti. Mimi nathubutu kusema kwamba serikali ikiamua kutumia sheria hiyo basi asilimia kubwa ya magazeti yatafungiwa. Huenda tukarudi kwenye Uhuru na MZalendo. Ndiriki kusema serikali imekuwa na huruma juu ya magazeti mengi. Magazeti yanaandika habari ambazo kwa mujibu wa sheria ni uchochezi. Badala ya kupigania sheria ibadilike wao wanaishia kusema serikali isifungie magazeti; kwa kauli nyepesi ni kwamba serikali isitekeleze sheria.
 
Last edited by a moderator:
We mwenyewe umevaa siasa katika kulizungumzia hili suala, vinginevyo ungepeleka jukwaa la habari mchanganyiko
 
Hii imeandikwa na mtu mwenye akili zilizolala. Huu ni ule ule ulevi wa changanyiko na kuvimbiwa madaraka.
Unayo maswali mengi ya kutujibu ili uweze kukamilisha malalamiko yako.

Je kama isingekuwa kuvuja kwa habari huko Uingereza pesa ya Rada mnayotambia leo ingerudi??? Je kwanini leo kumechukuliwa hatua kuwasimamisha Wakurugenzi wa Wanyama Pori? Hivi unapoandika haya unakuwa umetokea ndani ya gunia lilioshonwa nini? Inaumiza akili kuwa bado tuna waTanzania wavivu kiasi hiki katika karne hii.
Come out clean! nataka nikutoe uvivu wa kufikiri, elewa kuwa nchi zilizoendelea zina sheria ya kuwakinga "Whistle Blowers" Unadhani ni kwanini wamaefanya hivyo? Tena mabunge yao ndiyo yaliyooidhinisha sheria hiyo.

Uliyeandika makala hii hapa ni wale wale mnaotaka kuishi kama Miungu hapa duniani na kutaka binadamu wengine waishi kama panya, wakidai haki zao, mnawatumia maharamia wa kwenda kuwaponda na kuwatupa porini. That is PATHETIC, ABSOLUTELY WRONG AND SINFUL. Sijui mnaamini katika Mungu yupi haswa? Ni ushetani kutetea uchafu kama huo. Nani aliwaambia kwamba Taifa haliwezi kutawalika kwa kufuata haki na usawa? Bila kuwaibia wananchi nk.
 
security guard, hizi pumba ulizomwaga humu hazitaweza kuwasafisha watuhumiwa wote wa unyama (barbaric acts) aliofanyiwa Dr. Stephen Ulimboka na serikali ikisimamiwa na Ikulu. Hazitasafisha tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa TISS Othman Rashidi, Naibu wake Jack Zoka, Ramadhani Ighondu (Rama) aka Abeid wa Ikulu, Moshi Mrungu Shabani, Buruani Ntilogwa, Abdallah Kunja, Mohamed Hasan, Shomari Kondo, Jacob Marandu, Mbega Hisbert, Abdi Abdi, Najma Damian, Wilson Sima, Zulfa Swalehe pamoja na maafande wa polisi Ahmed Msangi na bosi wake Suleiman Kova.

Kufungia magazeti au kufukuza wafanyakazi wa TIGO hakutasaidia kitu na sana sana kunazidi kuipaka matope hii serikali ya kifisadi na sasa imeamua kujihami kwa vitisho kuwataka raia wema kutotoa taarifa pindi wanaposhuhudia uhalifu. Kwa kweli serikali, kwa hivi vitendo vyake inazidi tu kujikanganya, akina security guard na zomba wanazidi kututhibitishia tu jinsi serikali ilivyoishiwa mbinu na sasa inatapatapa tu kama mfa maji. Serikali gani duniani inaweza kuwataka wananchi wake wafumbie macho vitendo vya kihalifu hata pale yanapofanyika mbele ya macho yao?
 
security guard, hizi pumba ulizomwaga humu hazitaweza kuwasafisha watuhumiwa wote wa unyama (barbaric acts) aliofanyiwa Dr. Stephen Ulimboka na serikali ikisimamiwa na Ikulu. Hazitasafisha tuhuma dhidi ya Mkurugenzi wa TISS Othman Rashidi, Naibu wake Jack Zoka, Ramadhani Ighondu (Rama) aka Abeid wa Ikulu, Moshi Mrungu Shabani, Buruani Ntilogwa, Abdallah Kunja, Mohamed Hasan, Shomari Kondo, Jacob Marandu, Mbega Hisbert, Abdi Abdi, Najma Damian, Wilson Sima, Zulfa Swalehe pamoja na maafande wa polisi Ahmed Msangi na bosi wake Suleiman Kova.

Kufungia magazeti au kufukuza wafanyakazi wa TIGO hakutasaidia kitu na sana sana kunazidi kuipaka matope hii serikali ya kifisadi na sasa imeamua kujihami kwa vitisho kuwataka raia wema kutotoa taarifa pindi wanaposhuhudia uhalifu. Kwa kweli serikali, kwa hivi vitendo vyake inazidi tu kujikanganya, akina security guard na zomba wanazidi kututhibitishia tu jinsi serikali ilivyoishiwa mbinu na sasa inatapatapa tu kama mfa maji. Serikali gani duniani inaweza kuwataka wananchi wake wafumbie macho vitendo vya kihalifu hata pale yanapofanyika mbele ya macho yao?

Unyama waliofanyiwa wagonjwa wetu huuoni?

Atarudia?
 
umeleta mada ya kipuuzi,sitaki hata kujadili upuuzi wako,unajipendekeza
 
Registration ya namba za simu si ndio matumizi yake haya, sasa kwa nini wafukuzwe? Hawakujua kama ku-register simu ingekula na kwao?!


Unafikiri watu wengine wanelewa maana ya Registration za simu? Walidhani ni kutumia Tigo pesa. Pole ukileta upuuzi kwenye mawasiliano, tunaenda kampuni ya simu uliyotumia na tutakupata tu.
 
mleta mada labda husomi alama za nyakati, tafsiri ya siri za sirikali ni kuvuja kiasi hiki ni kuwa imechokwa, labda nikutoe wasiwasi; mtapiga kelele sana lakini ukweli ni kuwa mmechokwa, imani kubwa sasa iko kwa M4C na hilo unalijua ndo maana ukaleta pumba hizi huku ukiwaita watu eti wajinga, mimi naona kama wewe ni mjinga zaidi kwa kushindwa kutambua WHAT TIME IS IT pole sana kamanda kadanganye wanao maana hata vijijini aint buy this ****.
 
sio siri ina maana Rweyemamu kaja na huku kwa jina la security guard?
 
Kumbe ni hivyo! Je, akirudia utamteka tena? (Nitumie PM uniambie wewe ni yupi kati ya waliotajwa na Mwanahalisi, nitatunza siri yako)

3670%20-%20action%20newton%20physics%20reaction.jpg

 
Mtoa mada una prove kuwa kumbe huo ulikuwa mpango wa CCM katika kuhakikisha ilani ya CCM inatimia. Asante kwa kutujuza lakini mju damu imwagikayo itawalilia.
 
Kama wafanyakazi wa TIGO wamefukuzwa kazi kwa kutoa siri za wateja, maana yake ni nini? Kwahiyo ni kweli kuwa wakina RAMA IGONDU na wenzake ndio waliomteka Ulimboka? Kama siyo serikali kwanini isitoe ushahidi mbadala? Nawashangaa waandishi wa habari walipoongea na JK siku ile kwanini hawakuuliza swali hili kuwa Serikali iwaeleze wananchi RAMA anayedaiwa kumteka Ulimboka ni nani? Iseme inamtambua au hapana? Je ni kweli ni afisa usalama? Waandishi nao bwana wanasubiri ukuu wa wilaya, maana siku hizi ukuu wa wilaya ni kazi ya waandishi wanafiki.
 
KUFUNGIWA kwa gazeti la MwanaHalisi, Jumatatu ya wiki iliyopita kumekwenda sambamba na kuwatambua na kufukuzwa kazi kwa maofisa 31 wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Tanzania jijini Dar es Salaam.

Katika toleo lake la mwisho wiki mbili zilizopita, gazeti hilo linatuhumiwa kuandika habari ya uchochezi dhidi ya serikali kwa kuichafua Idara ya Usalama wa Taifa, uchonganishi na ugombanishi kwa watu huku pia likihatarisha maisha kati yao kwa kuwatuhumu kuhusika na utekaji nyara, utesaji wa kikatili na jaribio la kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Stephen Ulimboka Juni 26, mwaka huu.

Sitaki kurejea habari hiyo wala kukumbushia machungu ya unyama aliofanyiwa daktari huyo hasa kwa vile suala hilo lenyewe linashughulikiwa na vyombo vya dola, halafu kuna kesi inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya mmoja kati ya watu wanaodaiwa kufanya ukatili huo kutiwa mbaroni mwezi uliopita.

Ninachotaka kuzungumzia hapa ni hatua iliyochukuliwa na kampuni ya Tigo ya kuwatimua kazi mara moja baadhi ya maofisa wake, wale ambao wanadaiwa kutoa nje siri za wateja wa mwajiri huyo kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

Wanatuhumiwa kuvujisha siri za mawasiliano yaliyofanywa na baadhi ya wateja wake na Ulimboka kwa gazeti hilo ikiwemo kutoa namba za simu zao, muda waliowasiliana naye kwa namna moja ama nyingine na majina yao, kisha wakahusishwa na madai ya kumteka, kumtesa, kujaribu kumuua na kumtelekeza katika Msitu wa Pande uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Tumesikia kelele nyingi zilizopigwa kijinga na baadhi ya watu wakiishutumu serikali kwa kulifungia gazeti hilo. Tumeona baadhi yao wanavyokwenda mbali zaidi kwa kutaka ilifungulie, wengine wakisema ifanye hivyo “mara moja na bila masharti yoyote” kwa madai kuwa adhabu hiyo ni ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari nchini.

Wanazungumza kipuuzi kwa kauli za kijinga dhidi ya mamlaka halali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wanajifanya eti hawafahamu kuwa vyombo vyote vya habari vinaendesha majukumu yake siyo kwa ridhaa zake vyenyewe isipokuwa kwa matakwa ya kisheria bila ya kujali kama ni mbovu kama wanavyodai na hata vinginevyo.

Magazeti yote nchini yanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, ileile inayopigiwa kelele nyingi ikisemwa imeshapitwa na wakati na kandamizi, lakini ileile na vilevile inapotumika kusajilia magazeti hakuna anayedai au kusema kuwa ni kandamizi ama kwamba inatakiwa ibadilishwe.

Udikteta wa sheria hiyo na maneno mengine ya shutuma dhidi yake unakuja tu wakati gazeti linapochukuliwa hatua zote halali za kisheria na serikali ikiwemo kuonywa, kufungiwa au kufutwa kabisa kutoka kwenye orodha ya magazeti pindi linapokwenda kinyume cha weledi pamoja na maadili ya uandishi wa habari.

Hapo ndipo kelele zinapoanza kutoka midomoni mwa baadhi ya watu wakiongozwa zaidi na wanasiasa na wanaharakati nchini, wote wakifanya hivyo siyo kwa nia njema isipokuwa kwa ujinga wa kutumiwa na magenge yanayoitwa wahisani na wafadhili kutoka nje ya nchi.

Wanafanya hivyo kwa kutaka kuivuruga serikali ili ishindwe kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kile ambacho katika ujumla wao wanapenda kiondoshwe madarakani mwaka 2015 huku chaguo lao hivi sasa likiwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachotaka kuleta ushoga nchini!

Nikirudi katika maudhui hasa ya makala yangu hii, napenda kuipongeza kampuni ya Tigo Tanzania ilivyochukua hatua za haraka kuwawajibisha watumishi wake kwa kuvujisha nje siri za wateja wake, jambo linaloweza kusababisha watu wengi waikimbie na kujiunga na mitandao mingine ya simu maana ipo mingi na tayari ushindani miongoni mwa makampuni hayo ni mkubwa kupindukia.

Tayari kuna kampuni mbalimbali zikiwemo kubwa za Vodacom, Airtel na Zantel huku nyingine zikianzishwa na kuingia sokoni, jambo ambalo litaongeza ushindani ambao ni pamoja na uaminifu, uadilifu, unyenyekevu; nafuu ya gharama za kupiga, kupokea ama kutumia ujumbe mfupi wa maneno na ubora wa mawasiliano kwa wateja wake.

Haiwezekani mwajiri aendelee kuwakumbatia watumishi waliokosa uaminifu na kufikia mpaka hatua ya kutoa nje siri za wateja wake ambao kimsingi uwepo wao ndio maisha yao ya kila siku, familia zao na ndugu zao wenyewe, lakini wanakuwa na ujinga wa kutumiwa na waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati kutenda kinyume cha sheria na kanuni za utumishi.

Sifahamu endapo kampuni hiyo ina utaratibu wa kuapisha watumishi wake iwe kwa mdomo au maandishi na kumbukumbu hizo kuhifadhiwa, lakini hata iweje ni ujinga na kinyume cha utumishi mahali popote duniani kwa mfanyakazi awe wa ndani au shambani kutangaza kitu chochote kinachofanywa na mwajiri mahali popote bila idhini yake mwenyewe.

Kama jambo hilo lingekuwa halina tatizo hakika wafanyakazi wenye mchezo huo wa ovyo wangekuwa wanavujisha kwanza siri zao wenyewe na wake zao nyumbani, waume zao au wapenzi wao, vinginevyo wangekuwa wanaeleza wanavyokiuka sheria na kanuni za ajira zao kwa hujuma zote wanazofanya.

Kila wakivujisha nyaraka zisizotakiwa kutoka nje ya ofisi au kwa watu wasiotakiwa siku zote wangekuwa wanatangaza walichofanya, lakini hawafanyi hivyo kwa vile wanaelewa kuwa hairuhusiwi katika hali zote na hilo ni kosa la jinai kwa sheria zote za kazi.

Ndiyo maana naipongeza kampuni hiyo kwa kuwachukulia hatua za haraka kuwang’oa na kuachana nao mara moja. Naishukuru kwa sababu imetimiza wajibu wake halali unaopaswa kufanywa na waajiri wote duniani kuanzia sekta binafsi hadi za umma ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mchezo wa kuvujisha siri za ofisi sehemu za kazi umegeuzwa kuwa mchezo wa kawaida kuanzia wizarani hadi bungeni, taasisi za fedha na idara takribani zote za serikali.

Leo utasikia “nyaraka tulizonazo” au “habari za ndani zilizopatikana kutoka” wizara hiyo, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na kadhalika.

Huko ndiko zinakotoka siri nyingi za serikali na kuangukia mikononi mwa wanaharakati wa masuala ya kijamii ingawa ukweli ni wanaharakati wa kisiasa, viongozi wa vyama vya siasa na makundi mengine yakiwemo haramu.

Ndiyo maana kwa mfano haishangazi kusikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Peter Slaa au Mwenyekiti wake, Freeman Aikaeli Mbowe wakitamba kukamata nyaraka za serikali na kuongeza uongo na uzushi juu yake.

Wanadai nyaraka hizo ni maelekezo maalum ya serikali kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa, Miji na Wilaya ya kuwashughulikia wapinzani huku wakijua ni uongo ila wanafanya hivyo kwa malengo ya kisiasa na kupotosha ukweli.

Wanatumia nyaraka hizo kufanya uchochezi kwa nia ovu, uchonganishi na ugombanishi ili wananchi waichukie serikali yao na CCM kwa kuwapandikizia majungu, uzushi na fitina zote wanazoweza kuzifanya wakati wowote na mahali popote.

Bila kujifunza kutoka kampuni ya Tigo na kuanza kuwafuatilia watumishi wote wa serikali na taasisi zake wanaovujisha nje siri za ndani ikiwemo kudurufu nyaraka, kuwakabidhi wanasiasa au watu wengine kinyume cha sheria na kanuni za ajira, kisha kuwatimua kazi na tena kwa haraka na kupoteza haki zao zote kamwe hawawezi kukoma.

Hiyo ndiyo kazi inayopaswa ianze sasa na kusimamiwa moja kwa moja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.

Acha umbumbumbu ww wakati wa kampeni kuna sms zilirushwa toka server za voda kukashifu kambi ya upinzani na zilikua za kichochozi zaidi mbona walikaa kimya?chama flani kikitumia mitandao ndo haki ila wananchi wakiomba information ndo kosa?au uliandika hii thread wakati umetoka baa?
 
Back
Top Bottom