Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Mamlaka zitusaidie kuboresha kituo cha daladala cha Nata mazingira ya kituo hicho sio rafiki kwa abiria wengi ambao wanakitegemea kusubiria usafiri wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu hasa mvua zikinyesha au wakati wa jua kali.
Kituo hicho ni kati ya vituo vinavyokusanya abiria wengi kwa wakati mmoja lakini cha kushangaza wahusika wameshindwa hata kujenga kibanda cha abiria kusubiria usafiri hali ambayo inatusababishia kadhia kubwa na abiria kusimama eneo lolote bila utaratibu.
Kwenye kituo hicho hakuna eneo rasmi ambalo abiria wanaweza kusubiria usafiri watu wengine wanasimama eneo ambalo ni hatarishi, lakini kuna wakati unakuta eneo hilo likiwa na msongamano zaidi kutokana na machinga kuweka meza zao za biashara sehemu ambazo wamezea kusimama huku mabasi ya baadhi ya kampuni wakati mwingine kupaki eneo hilo kwa muda mrefu jambo ambalo pia linapelekea msongamano wa daladala eneo hilo.
Ni vyema mamlaka kama hawana bajeti kwa sasa wanaweza kuwashawishi wadau wa sekta ya usafiri walioko eneo la Nata linalozunguka eneo hilo ambalo ni kero kwa abiria kujitolea kujenga kibanda kwa ajili ya abiria wengi ambao wengine ufika kwa ajili ya kukata tiketi au kusubiria magari baada ya kushuka, lakini pia wanaweza kushawishi wadau wengine ikiwemo kampuni kujenga kibanda hicho.
Hali ikiendelea kubakia ilivyo ni kuhatarisha usalama wa abiria ambao wanasimama maeneo ambayo sio rafiki lakini pia kwa namna watu wanavyokuwa wamesimama kiholela kwenye maeneo hayo inapelekea mandhari ya pale kuonekana katika taswira hasi.
Licha ya hivyo mamlaka za Jiji la Mwanza ni wakati wa kuwaza nje ya boksi namna ya kujenga vibanda vya abiria kwenye baadhi ya vituo muhimu ambavyo vimezoeleka kuwa na abiria wengi hii itasaidia kuwaondolea kero abiria na itafanya Jiji kuwa katika mandhari nzuri.